Skip to main content

Posts

Showing posts from November 24, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Rais Samia aweka Jiwe la Msingi la Msikiti Mkoani Morogoro

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan aweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa Msikiti wa Al Ghaith uliopo eneo la Kilakala Flats, Mkoani Morogoro tarehe 25 Novemba, 2024.

Waziri Kombo;Tanzania itaendelea Kuunga Mkono Juhudi za Kuleta amani na Usalama Ukanda wa Maziwa Makuu

Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo ameeleza kuwa Tanzania ikiwa ni mwasisi wa Jumuiya ya Ukanda wa Maziwa Mkuu (ICGLR) itaendelea kushirikiana na nchi Wanachama wa Jumuiya hiyo na Jumuiya ya Kimataifa katika juhudi za kutafuta amani ya kudumu kwenye ukanda huo. Waziri Kombo ameeleza hayo alipozungumza katika Mkutano wa Kawaida wa 18 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje (RIMC) wa Nchi Wanachama wa ICGLR uliofanyika jijini Luanda, Angola tarehe 24 Novemba 2024. Akizungumzia kuhusu msimamo, mchango na nafasi ya Tanzania katika kufatua amani na usalama kwenye ukanda wa Maziwa Makuu Waziri Kombo ameeleza kuwa, Tanzania chini ya uongozi mahiri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan itafanya kazi bila kuchoka kwa kushirikiana na nchi wanachama na Jumuiya ya Kimataifa kutatua migogoro iliyopo ili kuwa na ukanda wenye amani, ustawi na ustahimilivu. “Kama mwanachama mwanzilishi wa ICGLR, Tanzania inaamini kuwa ku...

Wakazi wa Misungwi Waaswa Kujitokeza kuchagua Viongozi wanaowataka Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza anawatangazia wananchi wa Halmashauri hiyo waliojiandikisha kwenye Daftari la Makazi Kujitokeza kupiga kura kwenye Uchaguzi wa serikali za Mitaa utakaofanyika Nchini Kote Novemba 27 Mwaka huu.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Missama,Zoezi la upigaji kura katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi litafanyika kwenye Vituo 736 Vilivyopo kwenye Vitongoji 723 pamoja na Vijiji 115. Taarifa hiyo imeeleza kuwa Vituo vya kupigia kura vitakuwa wazi kuanzia saa mbili kamili za asubuhi na vitafungwa ifikapo saa kumi kamili za Jioni.  Aidha Makundi maalum ya wazee,akinamama wenye watoto wachanga, wajawazito na watu wenye ulemavu watapewa kipaumbele wakati wa zoezi la uchaguzi.  Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi ina Jumla ya wapiga kura 267,260 ambao wanatarajiwa Kujitokeza kupiga kura kuwachagua Wenyeviti wa Vitongoji na Vijiji pamoja na Wajumbe wa Serikali za Vijiji.  Kauli mbiu ya Uchaguzi wa serikal...

CCM imesema haina huruma katika uchaguzi huu wa Serikali za mitaa

MNEC Biteko amesema tutabeba vyote Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa ambaye pia ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa CCM chini ya uongozi wa Rais Samia imejipanga kuifanya Geita kuwa na maendeleo zaidi na katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaofanyika Novemba 27, 2024 wananchi waichague CCM na kuipa ushindi wa heshima. Ametolea mfano wa jitihada za kuiletea maendeleo zilizofanywa na CCM kuwa ni pamoja na juhudi za Rais Samia za kuhakikisha Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) unawanufaisha zaidi wananchi kwa Geita. Dkt. Biteko amesema hayo Novemba 24, 2024 wakati akihutubia katika Kampeni zinazoendelea za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Wilaya ya Geita zilizofanyika katika Viwanja vya Nyankumbu mkoani Geita. “ Sasa tunaona miradi mbalimbali ikitekelezwa, Geita maendeleo yapo kila kona tunataka mchague viongozi watakaoshirikiana na viongozi wengine ili kutuletea maendeleo, CCM tunataka ushindi wa heshima...

Atunukiwa shahada ya udaktati wa heshima ya uongozi kutoka chuo kikuu cha Mzumbe

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametunukiwa Shahada ya Udaktari ya Heshima (PhD) katika uongozi, leo tarehe 24 Novemba 2024, kwenye mahafali ya 23 ya Chuo Kikuu cha Mzumbe, yaliyifanyika Kampasi Kuu ya Morogoro. Shahada hiyo aliyotunukiwa Mhe. Rais Dkt. Samia, imetokana na umahiri na uwezo aliouonesha kwenye uongozi katika nafasi mbalimbali alizotumikia taifa, kupitia Chama na Serikali na nje ya hapo. Pia Dkt. Samia leo ni mgeni maalum kwenye mahafali hayo yanayofanyika katika Viwanja vya Maekani.

Mhe. Kapinga Aendelea Kuhamasisha Wananchi Kushiriki Uchaguzi wa Serikali za mitaa Ruvuma

Na Mwandishi Wetu, Ruvuma.  MBUNGE wa Vijana Mkoa wa Ruvuma kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga ameendelea kuhamasisha Wananchi katika maeneo mbalimbali mkoani hapa ili waweze kujitokeza kwa wingi kupiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27 mwaka huu. Baada ya ziara ya mafanikio aliyoifanya wilayani Namtumbo, Mhe. Kapinga amefanya ziara pia wilayani Mbinga kwa kuanza na Vijiji vya Mkako na Kigonsera ambapo amewaasa Wananchi kuchagua Viongozi bora watakaosimamia shughuli za maendeleo katika Mitaa, Vijiji na Vitongoji hapa nchini. "Wananchi mliopo katika Kata ya Kigonsera, Mkako na maeneo yote ya Mbinga ifikapo Novemba 27, 2024 jitokezeni kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa ili mchague Viongozi makini kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM), " amesisitiza Kapinga.  Amesema kuwa, lazima umakini uwepo katika uchaguzi wa Viongozi kwani ndio watakuwa wasimamizi wakuu wa miradi ya maendeleo kwenye ma...