Skip to main content

Posts

Showing posts from January 22, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Watendaji Kituo Cha Uokozi Mwanza Watakiwa Kutoa Huduma za Dharura Kwa Saa 24

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, ametoa maagizo kwa watendaji wa Kituo cha Kuratibu Utafutaji na Uokozi cha Kikanda – Mwanza, chenye thamani ya takribani shilingi bilioni 19.8, kuhakikisha kituo hicho kinaendeshwa kwa saa 24 na kwa ufanisi wa hali ya juu. Amesema hayo leo Januari 23, 2026 baada ya kutembelea kituo cha Kuratibu Utafutaji na Uokozi, jijini Mwanza.  Amesisitiza kuwa huduma za uokozi ni kazi ya kuokoa maisha, hivyo hakuna uvumilivu kwa uzembe, kuchelewesha utoaji wa huduma za msaada pindi inapohitajika. “Hii ni kazi ya kuokoa maisha. Uzembe, kusinzia au kuchelewesha kutoa msaada ni kuhatarisha maisha ya Watanzania. Kituo hiki lazima kifanye kazi saa 24.” Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amesema ujenzi wa kituo hicho ni uthubitisho wa dhamira ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwatumikia watanzania na kujali changamoto mbalimbali nchini.  “Kituo hiki kilikuwa kijengwe mwaka 2018 kwenda Mwaka 2020, kilisimama baada ya wenzetu kujitoa, lakini Rais Dkt. Samia akasema tutak...

Waziri Mkuu Awasili Mwanza Kwa Ziara ya Kikazi

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Januari 23, 2026 amewasili mkoani Mwanza kwa ziara ya kikazi. Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu anatarajiwa kutembelea Kituo cha Kuratibu Utafutaji na Uokozi cha Kikanda, kukagua Meli ya Ambulance, kuweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Kusukuma na Kuhifadhi Maji, pamoja na kuzindua Meli ya MV Mwanza. Meli hiyo ya MV Mwanza inatarajia kufanya safari zake kati ya Mwanza na Bukoba huku ikitarajia pia kufanya safari zake kati ya Mwanza na nchi jirani ya Uganda. Taarifa ya serikali ilitolewa mwaka jana wakati meli hiyo ikitengezwa ilisema pia MV Mwanza itafanya safari nyingine kati ya Mwanza na Musoma baada ya kukamilika kwa kazi ya marekebisho ya bandari ya Musoma.

Dkt Joshua Maponga awataka vijana kulinda amani ya nchi zao

Mwanadiplomasia kutoka nchi ya Zimbabwe Dk. Joshua Maponga amewataka vijana wa Kitanzania na kiafrika kiujumla kuhamasika katika kupigania nchi zao ikiwa pamoja na kujenga fikra mpya katika mataifa yao. Hayo amezungumza mapema hii leo jijini dar es salaam katika mkutano mkuu wa habari ambapo amesema Mwalimu Julius Nyerere aliona ndoto ya baadae za vijana wa kiafrika akisema matatizo ya kiafrika ni matatizo ya Tanzania. Aidha Dkt Joshua amesema kuwa Umoja wa Ulaya ni wa pamoja ,Tanzania ni faida kwa Afrika ,Zimbambwe ni faida na afrika ni moja hivyo vijana kuwapenda maono ya viongozi waliowatangulia ili kujenga mustakqbqli mzuri wa mataifa yao. Dkt Joshua amesema kama vijana watafata miongozo iliyotanguliwa na waasisi waliotangulia kutakuwa na Taifa lenye Tija na manufaa kwa vizazi vijavyo. Hata hivyo Dkt. Joshua amesema afrika inaweza kusonga mbele kwa kuungana mkono zenyewe huku akizitaka kuchukua mfano kwa Rais Traole wa Burkinafaso. Aidha, pia Dk. Joshua amewataka viongozi wa kimatq...

Wabunge Wapongeza Nirc Kwa Mageuzi ya Kilimo Cha Umwagiliaji

📍 *Bungeni Dodoma.* Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, wameipongeza Tume ya Taifa ya Umwagiliaji na Mkurugenzi Mkuu Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) kwa juhudi kubwa zinazofanywa kuinua kilimo cha Umwagiliaji nchini kukuza uchumi kupitia sekta hiyo. Wajumbe wa kamati hiyo wamesema Tume inastahili heshima na pongezi za pekee zimfikie Mkurugenzi Mkuu Raymond Mndolwa kwa juhudi kubwa za kukamilisha miradi ya kimkakati ya Umwagiliaji nchini. Hayo yamebainika wakati wa kikao cha Kamati hiyo ya Bunge na Semina maalumu Mkoani Dodoma, ambapo kamati hiyo iliongozwa na Mwenyekiti wa Kamati Mheshimiwa Deodatus Mwanyika (Mb) Njombe Mjini. Mwanyika amesema, Tume inafanya kazi kubwa na nzuri na mabadiliko makubwa yamefanyika. Amesema pamoja na hatua hiyo Serikali inahitaji kuwapo na mpango maalumu wa kutenga fedha  na kuwa na mkakati wa Kitaifa wa kuiwezesha Tume kwa kuwa na vyanzo vingine vya mapato. “Ni muhimu Serikali kutafuta vyanzo vipya vyamapato na kuhak...

Mhe. Ndejembi Ahimiza Ushirikiano wa Wakuu wa Mikoa na Wilaya Katika Utekelezaji wa Miradi ya Nishati

Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, leo tarehe 22 Januari, 2026, amezungumza katika Mkutano wa Tathmini ya Utekelezaji wa Mkataba wa Lishe kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 unaofanyika katika Ukumbi wa Mabeyo, jijini Dodoma. Mkutano huo umeandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na umewahusisha Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri pamoja na Maafisa Lishe kutoka mikoa yote nchini. Akizungumza katika mkutano huo, Waziri Ndejembi amewasihi Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha wanatoa ushirikiano wa karibu katika utekelezaji wa miradi ya nishati inayotekelezwa katika maeneo yao, ili kufanikisha azma ya Serikali ya kusogeza huduma bora za nishati kwa wananchi.

Tunataka Kazi za Serikali Zifanyike Makao Makuu ya Nchi-Dkt. Mwigulu.

_Asisitiza Taasisi za Serikali zinapaswa kufahamu kwamba makao makuu ya nchi ni Dodoma_ WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kuwa Serikali inataka kazi zote zifanyike makao makuu ya nchi ili kusogeza huduma karibu na Wananchi. Amesema hayo leo Alhamisi (Januari 22, 2026) alipotembelea Ofisi za Wizara ya Maji na Wizara ya Madini zilizopo mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma. “Ninawapongeza sana, mmehamia Makao Makuu, taasisi zote za Serikali zinapaswa kutambua kwamba makao makuu ya nchi ni Dodoma, na huduma zote zinapaswa kutolewa hapa, hii sio kambi na wala hatutakuwa na Makao Makuu mbili zilizo sambamba”. Pia, Mheshimiwa Mwigulu ameziagiza Taasisi zote ambazo zimeshakamilisha ujenzi wa majengo katika makao makuu kuyatoa majengo hayo kwa Taasisi ambazo haziwajibiki kuhamia Dodoma lakini bado zimepanga. “Mheshimiwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu mwelekeze Katibu Mkuu atengeneze timu ifanye tathmini ya majengo yote ya Serikali yaliyoko Dar es Salaam ambayo hayana matumizi ili ...