Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania Dr. Samia Suluhu ameridhia malipo ya shilingi Milioni 800.65 kwa wananchi 429 wa Kata ya Mkange wanaopisha ujenzi wa Barabara ya Afrika Mashariki inayojengwa toka Tanga kupita Kata hiyo hadi Makurunge Bagamoyo. Akizungumza katika mkutano huo na wananchi wa vijiji Vitano vya kata hiyo, Mbunge wa jimbo la Chalinze ambaye pia ni Waziri Wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana,Ajira na wenye Ulemavu Ndugu Ridhiwani Kikwete aliishukuru serikali kwa kuendelea kutatua kero za wananchi na kumshukuru Mh. Rais kwa kuridhia fedha hizi zilipwe ili wananchi wapishe na kupata maendeleo. Akiishukuru serikali, Mbunge ameeleza shukrani zake kwa serikali kwa kutenga fedha kwa ajili ya barabara mbalimbali katika halmashauri hiyo ambazo zinakwenda kuongeza tija kiuchumi kwa wananchi wanaopitiwa na miundombinu hiyo. Pia Mbunge aliishukuru serikali kwa matayarisho ya ujenzi wa barabara toka Mandera hadi Saadan ambayo inakwenda kufungua fursa kiuchumi. Wakizungum...
Marato tv - Sauti ya Jamii