Skip to main content

Posts

Showing posts from September 18, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dc Itunda Amhakikishia Usalama, Mhubiri wa Kimataifa Mbeya

Na Mwandishi Wetu, Mbeya MKUU wa Wilaya ya Mbeya, Solomon Itunda, amemhakikishia Usalama wakati wote wa huduma za kiroho atakazofanya Jijini Mbeya, mhubiri wa Kimataifa kutoka nchini Kenya Pastor Ezekiel. Sambamba na kumhakikishi Usalama, DC Itunda alipongeza ujio wa Mhubiri huyo wa Injili wa Kimataifa kutoka nchini Kenya, ambaye atafanya mahubiri yake Jijini Mbeya. Pastor Ezekiel atamwombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Uchaguzi Mkuu ujao pamoja na amani ya Taifa, hatua ambayo DC Itunda ameieleza kuwa ni ya baraka kubwa kwa nchi. Akizungumza baada ya kupokea wageni hao, DC Itunda alisema ujio wa mhubiri huyo ni ishara ya upendo na mshikamano wa Kikristo unaovuka mipaka ya mataifa hayo jirani.  Aliongeza kuwa maombi kwa Taifa wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu ni muhimu kwa ajili ya kudumisha mshikamano na mshikamanifu wa Watanzania wote bila kujali imani zao. Katika hotuba yake, Pastor Ezekiel aliwahimiza waumini na viongozi wa dini kuendelea kusali kwa ajili ya amani...

Dkt Stergomena Tax Azindua Kampeni za Ccm Kata ya Kandawe

Mlezi wa kata ya Kandawe jimbo la Magu mkoani Mwanza ambaye pia ni waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,amezindua Kampeni za Uchaguzi katika Kata hiyo ambapo amemnadi na kumkabidhi Ilani ya Chama cha Mapinduzi Mgombea Udiwani wa Kata ya Kandawe ndugu Lucas Bomoa na viongozi wa Chama katika Kata hiyo. Katika Mkutano huo ambao umefanyika Septemba17 mwaka huu 2025, Dkt, Stergomena Tax, ametoa wito kwa wana CCM kushirikiana pamoja kufanya Kampeni mtu kwa mtu, nyumba kwa nyumba, Kitongoji kwa Kitongoji na Kijiji kwa Kijiji ili kukiletea ushindi Chama cha Mapinduzi kiendelee kushika dola. Pamoja na kumwombea Kura za Udiwani ndugu Bomoa, Dkt. Stergomena Tax, pia alitumia hadhira ya Mkutano huo kumnadi na kumwombea kura Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mgombea wa Kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na ndugu Boniventura Kiswaga anaegombea nafasi ya Ubunge wa Chama cha Mapinduzi Jimbo la Magu ili kuendelea kufaidika na uongozi unaowajali Wananchi. Akizungumza na Wananchi, Dk...

Kamishna Kuji Aipiga Msasa Kampuni Tanzu ya Tanapa (Til)

Na Mwandishi wetu- Arusha Kamishna wa Uhifadhi Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), CPA Musa Nassoro Kuji, amewataka Watumishi wa Kampuni Tanzu ya TANAPA (TANAPA Investment Ltd - TIL) kuongeza ubunifu na kuchapa kazi kwa ufanisi ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia katika utoaji wa huduma za ukandarasi ndani na nje ya Shirika. Kamishna Kuji ameyasema hayo leo Septemba 18, 2025 katika kikao chake na watumishi wa kampuni hiyo tanzu ya TANAPA. TIL ni Kampuni tanzu ya TANAPA iliyoanzishwa mnamo mwaka 2019 na lengo likiwa ni kutoa msukumo katika utekelezaji wa miradi ya Shirika pamoja na kuwa Kitega Uchumi cha Shirika katika kutekeleza miradi ya nje ya Shirika. Kamishna Kuji ametumia fursa hiyo kuipongeza kampuni hiyo kwa kazi ambazo imeshazifanya ikiwemo ukarabati wa barabara ya Hifadhi ya Taifa Arusha, ukarabati wa kiwango cha changarawe wa baadhi ya barabara za Jijini Arusha, ukarabati wa kipande cha barabara ya Hifadhi ya Taifa Serengeti na kazi nyingine ambazo zim...

Ccm Yaahidi Umeme, Huduma za Afya Namonge

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Bukombe kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Doto Mashaka Biteko amesema CCM imepanga kuongeza kasi ya maendeleo katika Kata ya Namonge kwa kusogesa karibu huduma za jamii. Dkt. Biteko amesema hayo Septemba 18, 2025 wakati wa mkutano wa kampeni katika Kata ya Namonge wilayani Bukombe mkoani Geita ikiwa ni sehemu Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika Oktoba 29, mwaka huu. “ Hapa tuna vitongoji sita kati yake vitatu havina umeme, mkituchagua tutakamilisha umeme katika vitongoji vyote, tunataka kila nyumba iwe na umeme, amesema Dkt. Biteko Akizungumzia huduma za afya amesema “ Nataka nimwambie Mtendaji wa Kata hii hatutaki vikao vya muda mrefu wananchi hawa wanahitaji huduma, nimenunua vifaa kwa ajili ya zahanati ningependa kuona imekamikika na inatoa huduma kwa wananchi ili wasitembee kilomita 12 kufuata huduma,”  Aidha, amesema Kata hiyo imepiga hatua kimaendeleo ambapo awali kulikuwa na shule saba za msingi na sasa zipo 1...

Mawakili wa Serikali Watakiwa Kuendelea Kuzingatia Sheria na Kanuni za Hifadhi ya Jamii

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Hamza S. Johari amewataka Mawakili wa Serikali kuyatumia mafunzo yanayotolewa kuhusu Hifadhi ya Jamii, katika kuhakikisha kuwa Sheria na Kanuni za Hifadhi ya Jamii zinalinda na kusimamia haki na maslahi ya Wanachama wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kuhusu Hifadhi ya Jamii kwa Mawakili wa Serikali yaliyoandaliwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PSSSF yanayofanyika kuanzia tarehe 18 hadi19 Setpemba, 2025 katika Chuo cha Uongozi Mwalimu Nyerere Kibaha, Mkoani Pwani.  Akizungumzia kuhusu mafunzo hayo, amesema kuwa Mawakili wa Serikali watanufaika kwa kuongeza ujuzi kwenye masuala mbalimbali husasan sheria zinazohusiana na Hifadhi ya Jamii ikiwemo , Sheria ya Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma [Sura ya 371], Sheria ya Mikataba [Sura ya 345], Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini [Sura ya 366], pamoja na Usimamizi wa Fedha na Uwekezaji. *“Ni matarajio yangu kuwa mafunzo h...