Skip to main content

Posts

Showing posts from August 11, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

WAFUNGWA ZAIDI YA 600 GEREZA KUU UKONGA KUPIMWA MOYO

Dar es Salaam Wafungwa zaidi ya 600 waliopo katika Gereza kuu Ukonga kufanyiwa uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo katika kambi maalumu ya siku sita inayofanywa na wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Kambi hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa JKCI kusogeza huduma za kibingwa za moyo karibu na wananchi huku ikitambua  kwamba afya ni haki ya kila binadamu na msingi muhimu wa maendeleo ya mtu na taifa kwa ujumla. Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kambi hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge alisema hii ni mara ya kwanza katika Serikali ya Awamu ya Sita kwa JKCI kufikisha huduma hizo za kibingwa katika mazingira ya gerezani.“Kusogeza huduma za afya karibu na wananchi ni sehemu muhimu ya utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050, badala ya kusubiri wananchi wenye changamoto za moyo kusafiri umbali mrefu kuifuata JKCI, imechukua hatua ya kuwafikia wananchi katika maeneo walipo ikiwemo wafungwa wa g...

CHALAMILA ATUMIA SHERIA HIZI KUWAPELEKA WENYE MABASI STENDI YA MAGUFULI

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewataka wamiliki na waendeshaji wa mabasi ya mikoani yanayofanya shughuli za usafirishaji katika maeneo ya katikati ya jiji kurejesha huduma zao katika Stendi Kuu ya Mabasi ya Magufuli, Ubungo, akiwapa hadi Jumatatu, Agosti 17, 2026, kutekeleza agizo hilo. Chalamila amesema hatua hiyo inalenga kupunguza msongamano wa magari katikati ya jiji, kurejesha utaratibu wa matumizi ya vituo rasmi vya mabasi na kuhakikisha fursa za kiuchumi zinawafikia pia watoa huduma wengine wa usafiri, wakiwemo waendesha daladala, mabasi ya mwendokasi, bajaji na bodaboda. Amesema Dar es Salaam ina Stendi ya Magufuli iliyojengwa kwa gharama ya zaidi ya Sh bilioni 80 na yenye uwezo wa kuhudumia mabasi mengi kwa wakati mmoja, hivyo hakuna sababu kwa mabasi makubwa ya mikoani kuendelea kuzagaa katika maeneo ya katikati ya jiji, ikiwemo Shekilango na maeneo yanayounganisha barabara kuelekea Magomeni. “Stendi yetu ile imejengwa kwa zaidi ya bilioni 80. Ni sten...

WAZIRI WA ULINZI NA JKT DKT. NYANSAHO AKAGUA UTENDAJI WA SHIRIKA LA NYUMBU, ASISITIZA KUONGEZA MCHANGO KATIKA UCHUMI

 WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Rhimo Nyansaho (Mb), amefanya ziara ya kikazi ya siku moja katika Shirika la Tanzania Automotive Technology Centre (TATC), maarufu kama NYUMBU, lililopo Wilaya ya Kibaha, Mkoa wa Pwani, kwa lengo la kujionea utendaji wa shirika hilo na namna linavyotekeleza majukumu yake ya kimkakati. Katika ziara hiyo, Waziri Nyansaho ametembelea maeneo mbalimbali ya shirika hilo linalomilikiwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), akipata fursa ya kuona shughuli zinazotekelezwa katika uzalishaji, ukarabati na ubunifu wa kiteknolojia, hususan katika sekta ya vyombo vya moto, vipuri na vifaa vya uhandisi. Akizungumza na uongozi na menejimenti ya Shirika la NYUMBU, inayoongozwa na Mwenyekiti wake, Luteni Jenerali na Balozi mstaafu Paul Meela, Waziri Nyansaho amesema ziara hiyo imelenga kupata uelewa wa kina kuhusu utendaji wa shirika, changamoto zinazolikabili pamoja na fursa zilizopo za kuongeza ufanisi na mchango wake katika maendeleo...

RC SENYAMULE AKAGUA UWANJA WA DODOMA, AWATAKA VIJANA KULINDA FURSA ZA AJIRA

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, amefanya ziara katika Uwanja wa Mpira wa Miguu wa Dodoma unaojengwa kwa thamani ya Sh bilioni 300 akieleza kuridhishwa na maendeleo ya ujenzi na kuwataka vijana wanaonufaika na ajira kupitia mradi huo kulinda fursa hizo kwa kuhakikisha wanatunza miundombinu na rasilimali zinazowekezwa na Serikali. Mhe. Senyamule ametoa kauli hiyo leo, Agosti 11, 2026, baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo, ambapo pia amepata fursa ya kuzungumza na kusikiliza changamoto za wafanyakazi wanaoshiriki katika utekelezaji wa mradi huo. Amesema uwanja huo ni miongoni mwa miradi mikubwa na ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali, ukiwa na umuhimu mkubwa kwa Mkoa wa Dodoma na Taifa kwa ujumla kutokana na uwezo wake wa kuchochea maendeleo ya michezo, ajira na shughuli mbalimbali za kiuchumi. “Mradi huu ni wa kimkakati kwa Mkoa wa Dodoma na kwa nchi yetu kwa ujumla. Ndiyo maana tumeona kuna sababu ya kuja kutembelea na kujua ujenzi unavyoe...

PAMPU 52 ZAFUNGUA FURSA MPYA ZA KILIMO KATAVI

 Na Mwandishi Wetu, Katavi SERIKALI imekabidhi pampu 52 za umwagiliaji zenye thamani ya zaidi ya Sh500 milioni kwa vikundi 46 vya wakulima mkoani Katavi, hatua inayolenga kuongeza tija katika kilimo, kupanua eneo linalolimwa na kuimarisha usalama wa chakula. Pampu hizo zimekabidhiwa kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) katika hafla iliyofanyika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi, ikiwa ni sehemu ya awamu ya kwanza ya mpango wa Serikali wa kuimarisha matumizi ya teknolojia ya umwagiliaji katika kilimo. Mradi huo unatarajiwa kuongeza eneo la umwagiliaji kwa takribani ekari 2,080, huku ukitoa fursa kwa wakulima kuongeza uzalishaji wa mazao mbalimbali na kuboresha kipato cha kaya. Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Onesmo Buswelu, aliwataka wanufaika kutumia pampu hizo kwa malengo yaliyokusudiwa badala ya kuzigeuza kwa shughuli nyingine zisizohusiana na kilimo. Buswelu alitoa tahadhari kwa baadhi ya wakulima dhidi ya kutumia vifaa hivyo k...

MWENGE WAZINDUA MRADI WA MAJI SH585 MILIONI MWANZA, KATA NNE KUNUFAIKA

Na Mwandishi Wetu, Mwanza MWENGE wa Uhuru Kitaifa 2026 umezindua rasmi Mradi wa Ujenzi wa Mtambo wa Kuchuja Maji Igombe–Kabangaja mkoani Mwanza, wenye thamani ya Sh585 milioni, unaolenga kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wa maeneo manne. Mradi huo umetekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA), kwa kushirikiana na Shirika la Maji la Uholanzi, Vitens Evides International (VEI), na umekamilika kwa asilimia 100. Uzinduzi huo umefanyika Agosti 11, 2026, wakati wa ziara ya Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wa Mwanza, ambapo Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026, Wazo Mwango’nda, alisema mradi huo ni sehemu ya jitihada za Serikali na wadau wa maendeleo katika kuboresha huduma muhimu za kijamii. Mradi huo unatarajiwa kunufaisha wananchi wa Kata za Bugogwa, Sangabuye, Kahama na Shibula, kwa kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama, hatua inayolenga kuboresha afya, usafi na ustawi wa jamii. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mwango’nd...

NCHIMBI AFUNGUA DAKHALIA, AAHIDI MAPINDUZI YA ELIMU ZANZIBAR

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema Serikali itaendelea kutenga rasilimali za kutosha ili kuhakikisha skuli zote zinakuwa na miundombinu ya kisasa, walimu wenye sifa, na vifaa stahiki vya kufundishia na kujifunzia. Makamu wa Rais amesema hayo, wakati wa hafla ya Ufunguzi wa Jengo la Dakhalia katika Skuli ya Sekondari ya Hasnuu Makame iliyopo Kibuteni Unguja, Zanzibar, ikiwa ni shamrashamra ya Tamasha la Kizimkazi (Kizimkazi Festival 2026). Amesema jitihada za Serikali katika kuimarisha miundombinu ya elimu ni endelevu ambazo zinajumuisha upatikanaji wa vifaa vya kufundishia, samani na upatikanaji wa walimu wenye sifa. Makamu wa Rais amesema lengo la uwekezaji huo, ni kuandaa vijana wenye maarifa, ubunifu na ujuzi utakao wawezesha kujitegemea na kuchangia kikamilifu katika ujenzi wa Taifa. Amewasihi kutunza Dakhali hiyo na miundombinu mingine ya elimu kwa umakini mkubwa. Ametoa rai kwa Wananchi, Wazazi na walezi wa eneo hilo ...