Skip to main content

Posts

Showing posts from December 25, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt Mwigulu: Viongozi wa Dini Endeleeni Kutoa Elimu ya Umoja na Amani

_Atoa wito kwa Watanzania kuhimiza umoja na amani_. Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba ametoa wito kwa viongozi wa dini kuendelea kushirikiana na Serikali katika kutoa elimu ya umoja na amani, kupinga chuki, migawanyiko na vitendo vyovyote vinavyoweza kuvuruga mshikamano waTaifa. Amesema kuwa vita yoyote inayohusisha wenyewe kwa wenyewe huwa haina mshindi bali ina kupoteza wote na mgawanyiko ndani ya taifa hauna mshindi bali una matokeo ya kushindwa wote kama Taifa. Ametoa wito huo leo (Alhamisi, Desemba 25, 2026)  aliposhiriki ibada ya Sikukuu ya Krismasi iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Kiinjili la Kilutheri la Azani Front jijini Dar es Salaam. “Manufaa ya amani ni makubwa: huleta maendeleo ya kiuchumi, huimarisha ustawi wa jamii, na huwezesha kila Mtanzania kushiriki kikamilifu katika kujenga Taifa.” Amesema kuwa Serikali inaendelea kutekeleza wajibu wake wakulinda amani na usalama wa nchi pamoja na kuwajenga Watanzania na hususani vijana kuthamini dhana ya uzalendo kwa nchi yet...