Skip to main content

Posts

Showing posts from September 25, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt Lekashingo awataka Watanzania kuchangamikia fursa katika sekta ya madini

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Dkt. Janet Lekashingo, amewataka Watanzania kuchangamkia fursa mbalimbali zinazopatikana katika Sekta ya Madini ili kujiongezea kipato na kuongeza mchango wa sekta hiyo katika Pato la Taifa. Akizungumza mara baada ya kumaliza ziara ya kutembelea mabanda kwenye Maonesho ya Nane ya  Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika Viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Bombambili mkoani Geita, Dkt. Lekashingo amesema: “Sekta ya Madini ni injini muhimu ya uchumi wa taifa letu. Hatuwezi kuiacha mikononi mwa wageni pekee, ni lazima sisi kama Watanzania tujitokeze kwa wingi, tuchangamkie fursa zilizopo kuanzia utafiti, uchimbaji, uchenjuaji hadi kwenye biashara na utoaji wa huduma migodini. Tukifanya hivyo, tutajipatia kipato na kuisaidia nchi kuongeza Pato la Taifa.” Ziara hiyo imehusisha pia viongozi mbalimbali wa Tume ya Madini wakiwemo Makamishna wa Tume, Mhandisi Theonestina Mwasha na Dkt. Theresia Numbi; Mkurugenzi wa Ukaguzi na Biashara ya Madini, ...

Rais Samia Asaini Kitabu Cha Maombolezo Kufuatia Kifo Cha Abass Ali Mwinyi

  Mgombea nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akimfariji Mama Siti Mwinyi kufuatia Kifo cha Mtoto wake Hayati Mhe. Abass Ali Mwinyi alipofika nyumbani kwa Marehemu Bweleo Wilaya ya Magharibi (B) Mkoa wa Mjini Unguja tarehe 26 Septemba 2025. Mgombea nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Viongozi na Wanafamilia ya Hayati Mzee Mwinyi wakati alipofika Bweleo Wilaya ya Magharibi (B) Mkoa wa Mjini Unguja kwa ajili ya kuifariji Familia hiyo kufuatia Kifo cha Kaka yao Hayati Abass Ali Mwinyi, tarehe 26 Septemba 2025.

Angela wa Chauma Aja na Mkakati Mkubwa wa Chuo Cha Maendeleo Jamii- Buhare Musoma Mjini

Na  Jovina Massano- Musoma. Mgombea ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Ukombozi wa Umma CHAUMA Jimbo la Musoma mjini Angela Derick Lima amesema upandishaji hadhi chuo Cha Maendeleo ya Jamii kilichopo Kata ya Buhare Jimbo la Musoma mjini kutawezesha Maendeleo na ukuaji wa uchumi katika Kata. Ameyasema hayo Septemba 25,2025 wakati akinadi Sera za chama hicho katika kata ya Buhare Jimbo la Musoma mjini mkoani Mara. Anjela amesema endapo serikali ingepandisha hadhi Chuo Cha Maendeleo ya Jamii kilichopo Kata ya Buhare ingewezesha ukuaji wa uchumi katika eneo hilo na kuongeza Maendeleo  ya wananchi. Amesema upandishaji hadhi utawezesha ongezeko la watu ambapo wakazi wa eneo hilo watafanya shughuli na kutoa huduma Mbalimbali na kuwezesha upatikanaji wa ajira na kujiajili  na kujiletea Maendeleo. Kata hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ukoaefu wa soko la pamoja, miundombinu mibovu ya barabara na ukosefu wa wodi ya akina mama. "Kwa kushirikiana na serikali nitakwenda kusuku...

Wasira Awanyooshea Kidole Wanaojipanga Kwa Umeya, Uenyekiti wa Halmashauri Badala Kusaka Ushindi wa Ccm

Na Mwandishi Wetu, Mkinga MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira amewaonya baadhi ya wagombea udiwani katika maeneo mbalimbali ambao wameanza harakati za kusaka uenyekiti wa halmashauri na umeya, kabla ya uchaguzi. Amesema wanachotakiwa kufanya wana CCM wote kwa sasa ni kuhakikisha wanasaka kura za kishindo kwa Chama hususan za mgombea urais Dk. Samia Suluhu Hassan. Amesema hayo leo Septemba 25, 2025 alipokuwa akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM katika kikao cha ndani kilichofanyika wilayani Mkinga Mkoa wa Tanga, jana. Kikao hicho ni mfululizo wa vikao anavyoviendesha kwa kukutana na viongozi na wana CCM kumwombea kura Dk. Samia, wagombea ubunge na udiwani waliosimamishwa na Chama kwa uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, mwaka huu. "Kwa madiwani ninawaomba sana sio hapa Mkinga, hapa sijaambiwa lakini huko nilikotoka madiwani wameanza kutafuta mwenyekiti wa halmashauri na huku wao wenyewe hawajachaguliwa, sasa wewe utajuaje kama utachaguliwa wew...

Hili la Kongani za Viwanda kila wilaya, Dkt. Samia Umepiga Penyewe

Na: Dkt. Reubeni Lumbagala, Tanga Viwanda ni moja ya sekta za kiuchumi zenye mchango mkubwa katika kuchechemua maendeleo ya watu na ya Taifa. Uwekezaji wa viwanda unakwenda sambamba na uboreshaji wa sekta nyingine kama vile kilimo, umeme, maji, barabara, biashara ili kwa pamoja viwezeshe ufanisi wa viwanda. Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeipa msukumo mkubwa sekta ya viwanda. Ndiyo maana kumefanyika maboresho makubwa ya sheria zinazosimamia uwekezaji na biashara, uboreshaji wa mazingira ya kufanyia shughuli za viwanda na biashara pamoja na uwekaji wa kodi rafiki ili kuvutia shughuli za viwanda na ustawi wake. Moja ya ahadi iliyomo katika Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) 2025-2030 ni uanzishwaji wa kongani za viwanda (industrial parks) kila wilaya hapa nchini ili kuchochea huduma za kijamii, maendeleo ya kiuchumi na Taifa kwa ujumla. Kongani za viwanda ni maeneo maalum yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli za viwanda. Katika maeneo hayo huwep...

Mavunde Aendelea na Kampeni za Mtaani Kwa Mtaani Kata ya Ihumwa

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Mtumba kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Anthony Mavunde, ameendelea na awamu ya kwanza ya kampeni zake kwa kuzungukia mitaa mbalimbali ya Kata ya Ihumwa. Katika ziara hiyo,Ndugu  Mavunde alikutana na wananchi wa Mitaa ya Chang’ombe, Chilwana, Ilolo na Ihumwa ambapo alisikiliza changamoto zao na kuwasilisha sera za chama chake. Akizungumza na wananchi leo Septemba 25,2025, ndugu Mavunde amesema: “Nimekuja kusikiliza maoni na changamoto zenu ili tuzitatue kwa pamoja. Kura zenu kwangu na kwa wagombea wa CCM zitasaidia kuendeleza kasi ya maendeleo katika Jimbo la Mtumba, " amesema Aidha, alitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi kumpa kura za ushindi pamoja na kumuombea kura Mgombea Urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, na Mgombea Udiwani wa Kata ya Ihumwa, Edward Magawa. “Naomba tushirikiane kumpa kura za kishindo Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa urais, diwani wenu Edward Magawa, na mimi kwa ubunge, ili kwa pamoja tuendelee kuwaletea maendeleo yenye tija,...

Hili la Kongani za Viwanda Kila Wilaya, Dkt.Samia umepiga Penyewe

Na: Dkt. Reubeni Lumbagala, Tanga Viwanda ni moja ya sekta za kiuchumi zenye mchango mkubwa katika kuchechemua maendeleo ya watu na ya Taifa. Uwekezaji wa viwanda unakwenda sambamba na uboreshaji wa sekta nyingine kama vile kilimo, umeme, maji, barabara, biashara ili kwa pamoja viwezeshe ufanisi wa viwanda. Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeipa msukumo mkubwa sekta ya viwanda. Ndiyo maana kumefanyika maboresho makubwa ya sheria zinazosimamia uwekezaji na biashara, uboreshaji wa mazingira ya kufanyia shughuli za viwanda na biashara pamoja na uwekaji wa kodi rafiki ili kuvutia shughuli za viwanda na ustawi wake. Moja ya ahadi iliyomo katika Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) 2025-2030 ni uanzishwaji wa kongani za viwanda (industrial parks) kila wilaya hapa nchini ili kuchochea huduma za kijamii, maendeleo ya kiuchumi na Taifa kwa ujumla. Kongani za viwanda ni maeneo maalum yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli za viwanda. Katika maeneo hayo huwep...

Mradi wa Tactic Manispaa ya Kibaha Kuongeza Fursa za Uchumi Kwa Wananchi

Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA ) inatarajia kuleta manufaa makubwa kwa Manispaa ya Kibaha Mkoani Pwani na Miji mingine nchini, kupitia Mradi wa Uboreshaji Miundombinu ya Miji Tanzania (TACTIC) ukitajwa kuongeza fursa za ajira kwa Vijana na kuchochea uchumi wa Manispaa ya Kibaha chini ya Maboresho makubwa ya mazingira ya ufanyaji wa biashara yatakayofanyika. Kauli hiyo imetolewa leo Alhamisi Septemba 25, 2025 katika Soko la Mnarani, Kibaha na Mhandisi Emmanuel Manyanga, Muwakilishi wa Mtendaji Mkuu wa TARURA ambaye pia ni mratibu msaidizi wa mradi wa TACTIC wakati wa utiaji saini Mkataba wa mradi wa TACTIC kwa Manispaa ya Kibaha ukihusisha Uboreshaji wa Miundombinu ya Barabara, Soko kuu la Mnarani, Bustani ya Mapumziko na burudani pamoja na ujenzi wa Jengo la Usimamizi wa mradi ukigharimu shilingi Bilioni 19.83 bila jumuisho la kodi ya ongezeko la thamani (VAT) "Mradi huu kwa Manispaa ya Kibaha utaongeza fursa za ajira, kuchochea ukuaji wa uchumi, kuboresha hali z...