Na Emmanuel Chibasa. Mkuu wa mkoa wa Mara Kanali Evance Alfred Mtambi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika semina ya maswala ya uwekezaji na vivutio vinavyotolewa na serikali kwa wawekezaji kupitia kituo cha uwekezaji Tanzania(TIC), Semina iliyoandaliwa na kituo cha uwekezaji Tanzania kwa kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mara inatarajiwa kufanyika siku ya Jumanne 23 Julai,2024 katika ukumbi wa uwekezaji uliopo Musoma mkoani Mara. Kwa mujibu wa Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022, Mkoa wa Mara una idadi ya watu 2,372,015 kutoka 1,743,830 wa sense ya mwaka 2012. Mkoa wa huu umebarikiwa fursa nyingi za uchumi na uwekezaji kupitia sekta mbalimbali kutokana na uwepo wa hifadhi ta Taifa ya Serengeti ambayo asilimia 70 inapatikana mkoa wa Mara, Ziwa Victoria ambalo ni Ziwa la tatu kwa ukubwa duniani na visiwa vinavyo patikana pia katika ziwa hili vinatoa fursa kubwa za kijamii, kiuchumi, uvuvi, Utalii na umwagiliziaji. Jamii ya wakazi wa mkoa wa Mara wanajishughulisha na s...
Marato tv - Sauti ya Jamii