Solar Freezer Zinavyoweza Kusaidia Kupunguza Upotevu na Kuharibika Kwa Mazao ya Chakula Baada ya Mavuno
Na Emmanuel Chibasa Tanzania sawa na nchi nyingine zinazoendelea Duniani, inakabiliwa na upotevu mkubwa wa mazao kati ya asilimia 20 hadi 30 ya mazao ya mkulima, hupotea baada ya mavuno kutokana na wakulima kuwa na uelewa mdogo wa uhifadhi na matumizi ya teknolojia nafuu na safi kama vile nishati ya jua kwa ajili ya kuhifadhi mazao. Upotevu wa chakula kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO), hutokea kuanzia shambani baada ya mavuno bila kujumuisha mauzo. Upotevu huo unaweza kufanywa na wakulima, katika mchakato wa uandaaji pamoja na usafirishaji kwa ajili ya uuzaji wa chakula na utupwaji, kwa upande mwingine hutokea sokoni baina ya muuzaji na mtumiaji. Wakati hali hii ikitokea kwa wakulima hapa nchini na duniani Kwa chakula kupotea baada ya mavuno au kuharibika na kutupwa inakadiliwa kuwa kuna watu takribani Milioni 820 duniani kote wanakabiliwa na njaa. Shirika la umoja wa mataifa la chakula na kilimo linaeleza kuwa, ni muhimu kuzuia upotevu na utupwa...