Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo amezindua meli nne mpya za mizigo katika Ziwa Tanganyika na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha Tabora hadi Kigoma, yenye urefu wa kilomita 506. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amezindua meli hizo leo Jul 20,2026 Mkoani kigoma ambapo amesema kuwa Serikali inaendelea kujenga mfumo jumuishi wa uchukuzi nchini unaounganisha reli, bandari, barabara na viwanja vya ndege ili kupunguza gharama za usafirishaji, kuongeza ushindani wa biashara na kufungua masoko mapya. "Kigoma haitakuwa tena mwisho wa reli. Itakuwa mwanzo wa kufunguka kwa fursa za biashara na uwekezaji," amesema Rais Dkt. Samia. Ameongeza kuwa, reli ya Tabora-Kigoma, itakapokamilika, itaunganisha mkoa huo na Bandari ya Dar es Salaam pamoja na mtandao wa bandari za kisasa katika Ziwa Tanganyika, hivyo kurahisisha usafirishaji wa mizigo ndani na nje ya nchi. Rais Dkt. Samia amesema uwekezaji unaoendelea kufany...
Marato tv - Sauti ya Jamii