Skip to main content

Posts

Showing posts from May 31, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Tanapa Yatunukiwa Tuzo ya Juu Ulaya Kwa Mara ya Sita Mfululizo

  Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limetunukiwa tuzo ya hadhi ya juu kwa mara ya sita mfululizo iitwayo European Quality Choice Diamond ya mwaka 2025 katika hafla iliyofanyika usiku wa tarehe 29 Mei, 2025, jijini Stockholm, nchini Uswidi, kwa kutambua utendaji wake mahiri katika utalii na uhifadhi. Tuzo hiyo ilikabidhiwa na Mshauri Mtendaji Mkuu wa taasisi ya European Society for Quality Research (ESQR), Bw. Michael Harris,  kwa Balozi wa Tanzania nchini Uswidi, Mhe. Mobhare Matinyi, ambaye aliambatana na Kamishna wa Uhifadhi wa TANAPA, Bw. Mussa Nassoro Kuji; Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Rodwell Ole Meing'ataki; Afisa Mkuu wa Uhifadhi, Eunice Msangi; Afisa Uhifadhi Andrew Mbai; na Afisa Mwandamizi wa Ubalozi wa Tanzania, Malik Hassan. TANAPA ilikuwa kampuni pekee ya utalii na uhifadhi kati ya 49 kutoka nchi 42 duniani zikiwemo zingine sita za Afrika iliyotunukiwa tuzo hiyo. TANAPA ni moja ya taasisi kadhaa nchini zenye usajili wa ISO 9001:2015 ambacho ndicho ...

Ilani ya Uchaguzi ya Ccm 2025/2030 Italeta Maendeleo Makubwa Vijijini"Mbunge Ghati Chomete

Na Shomari Binda-Musoma  ILANI ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ( CCM) ya mwaka 2025/2030 kugusa kasi ya maendeleo vijijini imemgusa mbunge wa Viti maalum mkoa wa Mara Ghati Chomete  Akizungumza kwa njia ya simu na GMTV kutoka mkoani Dodoma baada ya kuzinduliwa kwa ilani hiyo na Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho Dkt.Samia Suluhu Hassan amesema maendeleo yatazidi kupaa maeneo ya Vijijini. Amesema maendeleo yamekuwa yakifanyika Vijijini na kutajwa kwenye ilani kufanyika kwa kasi ni jambo jema linalokwenda kuwasaidia wananchi wa maeneo hayo. Ghati amesema ilani imezungumzia kuhusiana na kufikisha umeme kila kitongoji suala linalokwenda kuinua uchumi wa wananchi kwenye maeneo yao. Amesema umeme ni uchumi na utakapofika vitongojini zipo shughuli za kiuchumi zitakazofanywa na wananchi na kujiongezea kipato. Mbunge huyo amesema ilani iliyozinduliwa na CCM ni bora zaidi ambayo kwa asilimia kubwa imezungumzia masuala ya maendeleo. " Tumeona ilani moja ya mambo muhimu iliyoyazungumzi...

Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan apokea Tuzo ya Heshima

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo Maalum ya Heshima ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson katika viwanja Bunge Jijini Dodoma tarehe 31 Mei, 2025.

Bunge la Tanzania lampa Tuzo ya Heshima Rais Samia

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo Maalum ya Heshima ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson katika viwanja Bunge Jijini Dodoma tarehe 31 Mei, 2025.