Skip to main content

Posts

Showing posts from February 15, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mkuu Akagua Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta

_Aonya wageni wanaoanzisha makampuni kwa kutumia kivuli cha wazawa_ WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Jumatatu (Februari 16, 2026) amekagua mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima (Uganda) hadi Chongoleani mkoani Tanga na amesema kuwa amefurahishwa na utekelezaji wake. Amesema kuwa mradi huo ni wa kimkakati ambao utagharimu Dola za Marekani bilioni 5.65 ni kielelezo cha undugu kati ya Tanzania na Uganda. “Ninatambua msisitizo uliowekwa na viongozi wetu, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mheshimiwa Rais Yoweri Kaguta Miseveni katika utekelezaji wa mradi huu.”   Mheshimiwa Dkt. Mwigulu ambaye yuko mkoani Tanga kwa ziara ya kikazi amesema kuwa Serikali itaendelea kuweka uzito unaostahili katika kutekeleza mradi huo ambao  umefikia asilimia 81 ya utekelezaji kwa heshima ya undugu kati ya Tanzania na  Uganda. “Lakini tutaendelea kuweka uzito unaostahili kwa heshima ya kulinda uhuru wetu kwa kuwa ni nchi huru ambayo inaweza kujitegemea kutekeleza mradi wa kiwa...

Daraja la Mto Pangani ni Kichocheo cha Uchumi-Dkt. Mwigulu

_Asema ameridhishwa na kiwango cha uwekezaji kilichofanywa na Rais Dkt. Samia kwenye daraja hilo_ WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kuwa mradi wa ujenzi wa daraja la Pangani na barabara unganishi utasaidia kukuza shughuli za kiuchumi kwa wananchi wa maeneo hayo. Ameongeza kuwa ameridhishwa na kiwango cha uwekezaji kilichofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika daraja hilo ambalo “Si kila kiongozi anakuwa na maono na ujasiri wa kuweza kuchukua hatua za kujenga miundombinu ya aina hii”  Amesema hayo leo Jumapili (Februari 15, 2026) wakati alipokagua Miradi wa Ujenzi wa Daraja la Pangani lenye urefu wa mita 525 na barabara unganishi zenye urefu wa kilomita 25.6. Gharama ya mradi ni Shilingi bilioni 124.9. Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amesema kuwa ujenzi wa barabara na daraja hilo utaweka alama ya kudumu katika wilaya hiyo “Tuendelee kumkumbuka na kumuombea Mheshimiwa Rais Dkt. Samia, hii ni kazi ya kiongozi mwenye maono.” Kadhalika Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amewataka viongozi ...

HESLB yaanza kupokea maombi ya mikopo Diploma

Na: Mwandishi Wetu, DAR Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imeanza rasmi kupokea maombi ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ngazi ya Stashahada (Diploma) katika kozi za vipaumbele wanaotarajiwa kudahiliwa mwezi Machi, 2026. Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Dk. Bill Kiwia, Jijini Dar es Salaam ambapo dirisha la maombi ya mikopo hiyo limefunguliwa Februari 15, 2026 hadi Machi 15, 2026.  "Niwahimize wale wote wanaotarajiwa kudahiliwa mwezi Machi, 2026, katika kozi za vipaumbele kutumia vyema dirisha hili la uombaji mikopo ili waweze kutimiza malengo yao ya kielimu," amesema Dk. Kiwia. Katika hatua nyingine, Dk. Kiwia amewasisitiza waombaji wote kusoma vyema mwongozo wa utoaji mikopo kwa wanafunzi wa ngazi ya Stashahada unaopatikana katika tovuti ya Bodi ya Mikopo ili kuzingatia vigezo muhimu vilivyoainishwa. Kimsingi, serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan imeweka mkazo wa kuhakikisha vijana wa Kitanzania wanapata...

Dkt. Mwigulu Agusa Maisha ya Bw. Shabani

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba akizungumza na mlemavu wa miguu, Nassor Shaban Sabuni ambaye alijitokeza katika mkutano wa hadhara wa Waziri Mkuu uliofanyika katika Uwanja wa Lemore Tanga mjini leo Februari 15, 2026.  Ndugu Shabani alimuomba Waziri Mkuu msaada wa Pikipiki ya Matairi Matatu (Bajaji)  ambapo Dkt. Mwigulu aliridhia ombi hilo na kuagiza Ofisi yake kumnunulia aina ya bajaji anayoitaka.

Rais Samia Akiondoka Nchini Ethiopia

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiondoka katika Uwanja wa Ndege wa Bole Jijini Addis Ababa Nchini Ethiopia leo February 15, 2026 kurejea Nchini Tanzania baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Umoja wa Afrika (AU).

Rais Samia Afanya Mazungumzo na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bi. Amina Mohammed , tarehe 15 Februari, 2026 jijini Addis Ababa Ethiopia Rais Dkt. Samia yupo nchini humo kwa ziara ya kikazi ya siku nne ambapo, pamoja na shughuli nyingine, alishiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika tarehe 14 na 15 Februari 2026.

Dkt. Mwigulu Aweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Chuo Kikuu Mzumbe, Kampasi ya Tanga

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Februari 15, 2026 ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa miundombinu ya Chuo Kikuu Mzumbe kampasi ya Tanga ambayo hadi kukamilika kwake kutagharimu zaidi cha shilingi bilioni 12  Chuo hicho kinachojengwa katika kata ya Gombero, Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga, unatekelezwa kupitia mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi” (“Higher Education for Economic Transformation” – HEET”) Miradi inayoendelea kutekelezwa kupitia mpango huo ni Ujenzi wa Jengo la Taaluma lenye jumla ya madarasa 6, Maktaba ndogo, Ukumbi wa mihadhara, maabara mbili zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 80 kila moja, pamoja na ofisi 36 zitakazohudumia wafanyakazi 72. Aidha majengo mengine ni Hosteli 2 za wanafunzi, Bwalo la Chakula, Kituo cha afya kitakachohudumia wanafunzi, wafanyakazi na wananchi wa vijiji vilivyopo jirani na Chuo, Nyumba 4 za Wafanyakazi, Mfumo ya majitaka na dampo la kuhifadhia taka ngumu pamoja na Tenki la kuhifadhi Maji Safi la ujazo wa lita la...