Skip to main content

Posts

Showing posts from November 12, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mkuu afanya Mazungumzo na Dkt.Mehmet

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Novemba 13, 2024 amefanya mazungumzo na Balozi wa Uturuki ambaye anamaliza muda wake Nchini Tanzania Dkt. Mehmet Gulluoglu, Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu Magogoni jijini Dar es Salaam. Katika mazungumzo yao Mheshimiwa Majaliwa amemsihi Balozi Mehmet kuendelea kuwa balozi mzuri wa Tanzania popote atakapokuwa sababu tayari anajua fursa za uwekezaji na utalii zilizoko nchini. Kwa upande wake Balozi huyo ameshukuru Ushirikiano ambao ameupata kutoka Serikalini katika kipindi chake jambo ambalo limechangia kuimarisha Ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.

Majaliwa Kufungua Mkutano Mkubwa wa Biashara na Uchumi Dodoma

 .Majaliwa kufungua mkutano wa biashara na uchumi Dodoma ·Utakutanisha wataalamu kujadili biashara na maendeleo ya kiuchumi Na Mwandishi Wetu WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, anatarajiwa kufungua mkutano wa Tano wa Biashara na Maendeleo ya Kiuchumi (BEDC) 2024) ambao umeandaliwa na Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) utakaofanyika kuanzia tarehe 22 mkoani Dodoma. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa chuo cha CBE, Profesa Edda Lwoga, alisema lengo la mkutano huo ni kujadiliana kuhusu masuala muhimu yanayohusu biashara na maendeleo ya kiuchumi. Alisema mkutano kama huo ulianzishwa mwaka 2020, na tangu wakati huo umejidhihirisha kuwa jukwaa muhimu la mijadala ya kibiashara na kiuchumi, likiwakutanisha washiriki kutoka sehemu mbalimbali za dunia. “Lengo kuu la Mkutano wa Tano wa Biashara na Maendeleo ya Kiuchumi (BEDC 2024) ni kuwaleta pamoja wataalamu, wajasiriamali, watafiti, na wadau wa maendeleo kutoka sehemu mbalimbali za dunia kujadili masuala muhimu ya...

Meja Jenerali Mabele aongoza Maafisa na Askari katika Mazishi ya Msaidizi wake

Mkuu wa jeshi la kujenga Taifa (JKT) meja Jenerali Rajab Mabele ameongoza maafisa,askari na mamia ya wananchi katika mazishi ya mmoja ya wasaidizi wake meja Ayub Ally Pazi aliyefariki kwa ajali ya gari Novemba 9 mwaka 2024 katika maeneo ya Nanenane mjini Dodoma. Akitoa neno la pole kwa mamia ya waombolezaji nyumbani kwa wazazi wa wa marehemu Kiwalani jijini Dar es salam kabla ya kufanyika kwa mazishi hayo,mkuu huyo wa JKT amesema taarifa za kifo cha meja Pazi alizipokea kwa mshtuko mkubwa. "Siku ya ijumaa tarehe 8 mwaka 2024 alikuja nyumbani kuniletea nyaraka ili nizifanyie kazi kabla ya jumatatu,ilipofika jumamosi tarehe 9 niliambiwa kuna ajali imetokea eneo la Nanenane na Meja Pazi amefariki! Kwa kweli taarifa zile nilizipokea kwa mshutuko mkubwa hasa ukizingatia tulikua nae jana yake na jinsi alivyokuwa karibu nami kama msaidizi wangu"alizungumza Meja Jenerali Mabele kwa masikitiko makubwa. "Mimi nilimkuta ofisini alikuwa msaidizi wa mtangulizi wangu,nami niliendelea ...

Rais Samia azungumza na Rais Mwinyi akiwemo Mkuu wa Majes

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi. Katika mangunzo hayo ambayo yamefanyika Ikulu ndogo Tunguru Zanzibar yamemhusisha pia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Mahmoud Thabit Kombo pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini (CDF) Jenerali Jacob John Mkunda kwenye Kikao maalum cha maandalizi ya Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) leo tarehe 12 Novemba, 2024.