Skip to main content

Posts

Showing posts from May 21, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Lindi mbioni kuwa lango kuu la uchimbaji madini

  · *Makusanyo yafika 105%* MKOA wa Lindi unatarajiwa kuwa lango kuu la uchimbaji wa madini kutokana na kuonekana kuwa na aina zaidi ya 10 za madini mbalimbali yanayopatikana kwa wingi ikiwemo madini ya kimkakati kama Kinywe (Graphite) na Nickel. Akizungumza katika mahojiano maalum, Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Lindi, Mhandisi Emmanuel Shija amesema utafiti uliofanywa na Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) mwaka 2024 kwa kutumia ndege nyuki umebaini uwepo wa kiasi kikubwa cha madini mkakati ya Kinywe katika eneo la Ruangwa katika Mkoa wa Lindi.  Aina nyingine ya madini yanayotambuliwa kuwepo ni pamoja na madini  yenye asili ya Chuma, kama Nickel, Dhahabu, Shaba, Manganese  na Madini ya viwandani ambayo ni Jasi, Chokaa, Chuma na Chumvi. Mhandisi Shija amesema pia Mkoa wa Lindi unazalisha kwa wingi madini ya viwandani ya Gypsum ambayo yanatumika zaidi kwenye viwanda vya saruji na 'gypsum board' vilivyopo ndani ya nchi na nchi jirani. “Mkoa  wa...

Wanachama wa Ccm Watoa Kilio Chao Kwa Rais Samia

  Na Shomari Binda-Musoma  WANACHAMA wa Chama cha Mapinduzi ( CCM) wamekuja na maombi ya mabadiliko kuruhusiwa kupiga kura za maamuzi kuwachagua wabunge na madiwani. Maombi hayo wameyatoa leo mei 22 2025 kwa nyakati tofauti nje ya kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Mara kilichofanyika makao makuu ya mkoa. Wamesema mabadiliko ya kwanza ya kuongeza wigo wa wajumbe ni nazuri lakini kwa kuboresha waruhusiwe wanachama wote wenye kadi za Kielektroniki wapige kura hizo. Mmoja wa wanachama hao aliyekitambulisha kwa jina la Baraka Mfungo kutoka Kata ya Kwangwa manispaa ya Musoma amesema wakiruhusiwa wanachsma wote itakuwa tiba sahihi ya kudhibiti Rushwa. Amesema hakutakuwa na ugumu wowote wa upigaji kura hizo ikiwa utawekwa utaratibu mzuri kuanzia ngazi ya Kata. Baraka amesema wao wamekuwa kama wametengwa wakati ni wanachama hivyo maombi yao ni kuruhusiwa kushiriki upigaji kura Amesema vikao vya chama vya taifa vitakavyofanyika mwishoni mwa mwezi huu jijini Dodoma makao makuu ya ...

Wasiolipia Vibanda Vya Biashara Manispaa Ya Musoma Watakiwa Kuondokaa Shomari Binda-Musoma

WAFANYABIASHARA wapangaji wa vibanda vinavyomilikiwa na halmashauri ya manispaa ya Musoma wasiolipia wametakiwa kuondoka. Kauli hiyo imetolewa leo mei 21,2025 na Naibu Meya wa manispaa hiyo Naima Minga alipokuwa akihitimisha kikao cha robo ya tatu ya baraza la madiwani. Amesema halmashauri inapaswa kukusanya mapato ya ndani ili kuweza kuwahudumia wananchi hivyo hawawezi kuwavulimia wasiolipia mapato hayo. Naima amesema moja ya chanzo cha mapato hayo ni vibanda vya biashara vilivyopangishwa na inashangaza kuona watu wanafanya biashara na kutokulipa kwa wakati. Naibu Meya huyo kupitia baraza hilo amemuagiza mkurugenzi wa manispaa ya Musoma kuiandaa timu yake kupitia afisa biashara kuweza kukusanya mapato. " Ndugu zangu kila mmoja wetu aende kuhimiza kwenye eneo lake kila chanzo cha mapato kikusanywe ili tuweze kuwahudumia wananchi wetu. " Kama alivyotuelekeza mkuu wa Wilaya twende tukakusanye mapato maana kwenye kipindi chote tumekuwa tukikusanya mapato kwa asilimia mia moja...

Bandari Chanzo Kingine cha Biashara ya Kaboni

Na Ada Ouko, Dodoma.  Ujumbe kwa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Masauni umetembelea bandari Oslo,Nchini Norway kwa lengo la kujifunza namna Bandari hiyo inavyohifadhi mazingira na  kuzuia uzalishaji wa gesi joto. Akizungumza na Ujumbe huo,Mkurugenzi Mkuu wa Bandari ya Oslo Ingvar Mathisen amesema kuwa ifikapo mwaka 2030, Bandari hiyo itakuwa imepunguza gesi joto kwa asilimia 85. Mathisen ameueleza Ujumbe wa Tanzania kuwa Bandari ya Oslo ni bandari mtambuka na haizalishi gesi joto na kwamba Bandari hiyo ni ya tatu kwa ukubwa duniani kwa kuwa na teknolojia janja ya bahari. Amesema kuwa lengo kuu la bandari hiyo ni kuhakikisha kuwa inapunguza gesi joto kwa 85% ifikapo mwaka 2030 ambapo Serikali ya Norway imeanzia kufikia lengo hilo kwa kutumia teknolojia. "Kuanzia mwaka 2018,Bandari ya Oslo, Norway imeacha kupokea na kuendesha meli zake kwa kutumia mafuta, badala yake meli zote iwe za kisafirisha abiria, m...

Kauli ya Rais Samia kuhusu kufurushwa kwa wanaharakati yagonganisha maafisa wakuu wa Serikali ya Kenya

 RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ameibua mjadala nchini Kenya, kufuatia onyo lake kwa wanaharakati wa haki za binadamu kutoka Kenya na Uganda waliotimuliwa Tanzania kwa kuhudhuria kesi ya kiongozi wa upinzani, Tundu Lissu. Huku waliotimuliwa wakiapa kushtaki serikali ya Tanzania, Waziri wa mashauri ya kigeni wa Kenya Musalia Mudavadi ameonekana kugongana na katibu wake Korir Arap Sing’oei.  Huku Mudavadi akiunga Rais Suluhu Dkt Sing’oei alihimiza Tanzania kuheshimu misingi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Akizungumza kwenye Citizen TV usiku wa Jumanne, Mudavadi alionekana kuunga mkono kauli za Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu kile alichokitaja kuwa ‘kuingilia masuala ya ndani’ ya Tanzania na kuonyesha wasiwasi wake kuhusu ‘ukosefu wa maadili’ wa Wakenya katika mienendo yao ya hivi karibuni. Tofauti na Mudavadi,Katibu Sing’oei, aliitaka serikali ya Tanzania kuwaachilia mara moja Jaji Mkuu Mstaafu Willy Mutunga na ujumbe wake, Sing’oei alisisitiza kuw...

Bunge la Uganda Labariki Raia Kushtakiwa katika Mahakama ya Kijeshi

Bunge la Uganda limepitisha mswada wa sheria kuhusu UPDF, mswada ambao sasa utaruhusu mahakama za kijeshi kusikiliza kesi za kiraia, hatua ambayo imeenda kinyume na uamuzi wa hivi karibuni wa mahakama ya juu ambayo ilisema mahakama hizo hazina hadhi kikatiba kusikiliza kesi za kiraia. Moja ya marekebisho muhimu yaliyofanywa na bunge ni kulitaka jeshi kuweka alama kwenye vyombo vyao vyote na mavazi ili kuvitenganisha na vile vya raia. Pia, sasa ni sharti kwa mkuu wa mahakama ya kijeshi kuwa wakili katika cheo cha Jaji wa mahakama kuu na kwamba aliyehukumiwa anaweza kukata rufaa katika mahakama ya juu zaidi ya kiraia. Sheria hii imepingwa na watetezi wa haki za binadamu na upinzani wekisema kwamba itatumika kuwalenga wakati nchi inakaribia uchaguzi ujao