Skip to main content

Posts

Showing posts from September 4, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Mhe. Kikwete Aongoza Timu ya Wizara Kuwasilisha Taarifa ya Ulipaji wa Taarifa ya Wastaafu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Welemavu), Mhe. Ridhwani Jakaya Kikwete, ameongoza timu ya Wizara @WMKVAU kuwasilisha taarifa ya mwenendo wa Ulipaji wa mafao ya Wastaafu Bungeni Septemba 4, 2024.  Katika kikao hicho, Mhe. Ridhwani, ameihakikishia Kamati ya Bunge kuwa changamoto zilizokuwa zinakabili mifuko yetu zimeendelea kutatuliwa huku wanachama wakiendelea kulipwa ndani ya Muda wa Siku 60.

Vijana wa JKT Waapa Kulinda Nchi Yao na Rais Wake

UAMUZI Serikali ya Tanzania wa kuanzisha mafunzo ya jeshi la kujenga Taifa(JKT) umetajwa kuwa  utaongeza uzalendo  na uchungu kwa vijana katika kulitumikia na kulilinda Taifa lao. Akisoma risala  ya utii wakati wa kufunga mafunzo ya JKT  kwa mujibu wa sheria opareshini miaka 60 ya Muungano kikosi 832 KJ Ruvu mkoani Pwani,mmoja wahitimu wa mafunzo hayo Hilda Salvatory Edward,amesema pamoja na mafunzo hayo kuwafunza nidhamu, ujasiri  pia yamewafanya kuwa wazalendo wa kweli kwa nchi yao. Kwa sababu hiyo  vijana hao katika risala yao hiyo pamoja na kulipongeza jeshi la kujenga taifa kupitia mkuu wa kikosi hicho,wamempongeza Rais na AMIRI jeshi mkuu mh Dr Samia Suluhu Hassan  kwa kuwezesha uwepo wa mafunzo hayo huku wakitoa ahadi kuwa watalilinda Taifa lao na Rais wake na kamwe  hawezi kwenda kushiriki katika vitendo viovu vinavyohatarisha amani ya nchi. Naye mkuu wa kikosi  cha 832 Ruvu JKT  kanali  Peter Elias Mnyani,amesema mafunzo ha...

Jumuiya ya Wazazi Mara Yapongeza Kasi ya Ujenzi wa Maabara Shule za Sekondari Musoma Vijijini

  Na Shomari Binda-Musoma UJENZI wa maabara 3 za masomo ya sayansi kwenye shule za sekondari jimbo la Musoma vijijini ili kuwafanya wanafunzi kusoma masomo hayo. Kasi hiyo imefanya kutolewa pongezi na kamati ya utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi wa CCM mkoa wa Mara iliyofanya ziara kwenye jimbo hilo jana Septemba 3 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Mara Julias Kambarage Masubo aliyeongoza kamati hiyo ametoa pongezi kwa jitihada za mbunge wa jimbo hilo Profesa Sospeter Muhongo kwa kushirikiana na wananchi kwenye ujenzi huo. Amesema masomo ya sayansi yana umuhimu mkubwa katika soko la ajira hivyo maabara hizo zitawafanya wanafunzi kusoma kwa vitendo. Masubo amesema jitihada za mbunge Muhongo na wananchi zinaonekana na kuwataka viongozi wengine kwenye maeneo yao kufanya hivyo. Amesema jimbo la Musoma Vijijini lenye Kata 21 kwa sasa lina sekondari 26 za Kata na 2 za madhehebu ya dini huku ujenzi wa sekondari mpya 11 unaendelea kwenye baadhi ya Kata. "Ujenzi wa maabara tatu za maso...

TANZANIA KUJIIMARISHA ZAIDI KIDIPLOMASIA - MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kujiimarisha kidiplomasia na itaongeza nguvu zaidi ili kuwawezesha Watanzania wengi kupata fursa mbalimbali katika jumuia za kimataifa. Amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanikisha kuimarisha ushirikiano baina ya nchi washirika na sasa mafanikio yanaonekana. "Rais wetu ameonesha nia njema katika kipindi chake cha miaka mitatu na nusu amefanya kazi kubwa ya kujenga diplomasia na mahusiano katika sekta mbalimbali na nchi nyingi duniani." Ameyasema hayo leo (Jumatano, Agosti 4, 2024) alipokutana na Mkurugenzi Mkuu Mteule wa Shirika la Afya Duniani kanda ya Afrika (WHO) Dkt Faustine Ndungulie, Ofisini kwake Mlimwa Jijini Dodoma. Jitihada hizo za Serikali ya awamu ya sita zimeiwezesha Tanzania kuendelea kupaa kidiplomasia kuiwezesha nchi kupata viongozi wakubwa ndani ya Taasisi za kimataifa. "Tunaamini kazi kubwa tulizozifanya katika kipindi hiki cha miaka mita...

MNADHIMU WA JESHI AISHUKURU KAMATI YA BUNGE KWA KUUTAMBUA MCHANGO WA JWTZ

  Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Salum Haji Othuman ameishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge, Ulinzi na Mambo ya Nje ya Kisiwa cha Ushelisheli kwa kuthamini mchango mkubwa uliotolewa na JWTZ katika harakati za ukombozi barani Afrika. Luteni Jenerali Othuman ameyasema hayo alipotembelewa na kamati hiyo Makao Makuu ya JWTZ Msalato jijiji Dodoma tarehe 03 Septemba 2024. Naye Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe Francois Adelaide amesema JWTZ limekuwa msaada mkubwa sana kwa nchi nyingi za kusini kwa Afrika. Amesema nchi yake itaendelea kukuza diplomasia ya Ulinzi hasa kwenye mafunzo, mazoezi pamoja na kubadilishana ujuzi katika kukabiliana na uhalifu unaovuka mipaka pamoja na kukabiliana na majanga.

Luteni Jenerali Salum Haji Othuman Aishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ushelisheli

Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Salum Haji Othuman ameishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge, Ulinzi na Mambo ya Nje ya Kisiwa cha Ushelisheli kwa kuthamini mchango mkubwa uliotolewa na JWTZ katika harakati za ukombozi barani Afrika. Luteni Jenerali Othuman ameyasema hayo alipotembelewa na kamati hiyo Makao Makuu ya JWTZ Msalato jijiji Dodoma tarehe 03 Septemba 2024. Naye  Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe Francois Adelaide amesema JWTZ limekuwa msaada mkubwa sana kwa nchi nyingi za kusini kwa Afrika. Amesema nchi yake itaendelea kukuza diplomasia ya Ulinzi hasa kwenye mafunzo, mazoezi pamoja na kubadilishana ujuzi katika kukabiliana na uhalifu unaovuka mipaka pamoja na kukabiliana na majanga.