Walimu Wakuu na Wakuu wa Shule Zote za Sekondari na Msingi Jimbo la Mtumba Kupatiwa Kompyuta Mpakato
Mgombea ubunge wa Jimbo la Mtumba kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Anthony Mavunde, ameendeleza kampeni zake katika Kata ya Ihumwa kwa kueleza mikakati ya kuboresha sekta ya elimu na kuinua uchumi wa wananchi kupitia uwekezaji katika miundombinu ya kijamii na biashara. Katika mikakati yake ya kuboresha elimu, Mavunde amepanga kutoa kompyuta mpakato (laptop) kwa shule zote za msingi na sekondari katika jimbo hilo, kwa ajili ya shughuli za kuchapisha mitihani na matumizi ya walimu wakuu. Mpango huo unatarajiwa kukamilika kufikia mwezi Januari, na unatajwa kuwa ni wa kipekee katika historia ya elimu nchini. "Kila Mwalimu Mkuu na Mkuu wa shule ofisini kwake atakuwa na kompyuta mpakato kwa shule zote za jimbo la Mtumba, pamoja na Kompyuta na mashine za kudurufu mitihani zile gharama za mtihani mnazotoa wazazi nitazibeba mimi mbunge wenu" amesema Mavunde Kwa upande wa Mtaa wa Chang’ombe, Mavunde amesema kuwa Shule ya Msingi Jenerali Msuguri, ambayo ni miongoni mwa shule kongwe k...