Na Mwandishi Wetu WAZAZI ambao watoto wao wanakwenda kusoma nje ya nchi kwa mwaka wa masomo wa 2025/2026 wametakiwa kufuatilia kwa karibu mwenendo wa watoto wao kitaaluma na tabia. Wito huo ulitolewa jana na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Elimu Nje ya Nchi, Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel alipokutana na wazazi na wanafunzi hao siku ya Jumapili kwenye ofisi za GEL jijini Dar es Salaam ambapo wazazi na wanafunzi hao walipewa taratibu za mambo ya kuzingatia kabla, wakati na baada ya kufika nchi wanazokwenda. Katika mkutano huo, ambao ulihudhuriwa na wawakilishi kutoka vyuo vikuu mbalimbali duniani, wanafunzi wengi walikabidhiwa viza zao tayari kwa ajili ya safari ya kuelekea vyuoni, huku wazazi wakipata fursa ya kuzungumza ana kwa ana na baadhi ya wawakilishi wa vyuo hivyo. Akizungumza wakati wa mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link, Abdulmalik Mollel, alisema wazazi wanalipolipa ada wasidhani kwamba wamemaliza jukumu lao na badala yaake bado wa...
Marato tv - Sauti ya Jamii