Na Shomari Binda-Rorya SERIKALI imepongeza uwekezaji uliofanywa na muwekezaji Nyihita Wilfred wa uanzishaji wa kiwanda na mashamba kwaajili ya uzalishaji wa mafuta ya alizeti. Pongezi hizo zimetolewa jana februari 26 na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exauds Kigahe alipotembelea mashamba na kiwanda cha Nyihita Sunflower wilayani Butiama na Rorya. Akizungumza mara baada ya kutembelea maeneo hayo amesema Tanzania bado ina upungufu wa viwanda vya mafuta ya kula hivyo wawekezaji wakiwemo wa ndani wanapaswa kulindwa. Amesema mkurugenzi Nyihita amefanya jitihada kubwa kwani licha ya kufanya uzalishaji lakini amekuwa msaada wa kwa kuanzisha programu za kuwasaidia wakulima kupitia kiwanda alichoanzisha. Kigahe amesema serikali itaendelea kuunga mkono jitihada za uwekezaji unaofanyika kuhakikisha viwanda vilivyoanzishwa vinaendelea. Amesema suala la upatikanaji wa mali ghafi kwaajili ya uzalishaji ni muhimu hivyo suala la kilimo cha umwagiliaji ni muhimu. " Nimshukuru na k...
Marato tv - Sauti ya Jamii