Skip to main content

Posts

Showing posts from January 10, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Tawa yawasilisha Taarifa ya Utendaji wake Kwa Kamati ya Bunge (Pic)

📍 Kamati yaridhishwa na Kasi ya ukuaji wa Taasisi hiyo. Na Beatus Maganja, Dodoma  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA Mej. Jen. (Mstaafu) Hamis R. Semfuko akiambatana na Menejimenti ya TAWA leo Januari 10, 2025 amewasilisha taarifa ya utendaji kazi wa TAWA kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) inayoongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Augustine Vuma Holle (Mb) katika kikao kilichofanyika Ofisi za Bunge jijini Dodoma. Akiwasilisha taarifa hiyo Semfuko amesema TAWA imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali katika kuhakikisha inaongeza mapato  Serikalini huku akibainisha  uwindaji wa kitalii  kuwa chanzo kikuu cha mapato ya TAWA ambapo huchangia takribani 70% ya mapato. Semfuko amesema baada ya UVIKO 19 mapato ya TAWA yamekuwa yakiongezeka mwaka hadi mwaka kutoka Shillingi Billioni 25.75 mwaka 2020/21 hadi shillingi bilioni 55.57 mwaka 2022/23 na kuongeza kuwa mapato hayo yalizidi kuongezeka kufik...

Mbunge Ghati Chomete ashiriki Katika Dua ya Kumuombea Rais Samia

 -Dua hiyo maalum ya kumombea Rais Samia imefanyika katika msikiti wa Masjidi- Fisabillah Kurwaki Kusoma vijijini  Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara Mhe.Ghati Zephania Chomete, Leo tarehe 10 Januari 2025 ameshiriki Swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Masjidi-Fisabillah iliyoko Kijiji cha Kurwaki, Kata ya Mugango, Wilaya Musoma Vijijini mkoani Mara.  Swala hiyo ya ijumaa imekuwa maalum kwa ajili ya kumuombea Dua Maalum Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri na Viongozi wote wa Serikali pamoja na kuliombea amani na utulivu Taifa letu la Tanzania.  Aidha, Uongozi wa Msikiti huo umemuombea pia Dua Maalum Mhe.Ghati Zephania Chomete (Mb), Mhe.Prof.Sospeter Muhongo (Mb), pamoja na Wahe.Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya Musoma Vijijini.  Mhe.Ghati Chomete, aliambatana na M/Kiti wa UWT Wilaya Musoma Vijijini (Bi.Jane Joseph Chongo) na Wahe.Madiwani wa Viti Maalum (Mhe.Kadogo Kapi na Mhe.Florah Magwa). Mh Ghati amekuwa akishirik...

Waziri Mkuu awasili Uganda Kumwakilisha Rais Dkt. Samia Mkutano wa Kilimo

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Januari 10, 2025 amewasili Kampala nchini Uganda ambapo kesho Januari 11, 2025 atamwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika Mkutano  kuhusu Mpango wa Kilimo Afrika utakaofanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Speke Resort and Conference Centre Munyonyo.  Mheshimiwa Waziri Mkuu alipokelewa na Waziri wa Nchi anayeshugulikia Kilimo, Mifugo na Uvuvi  wa Uganda, Fredrick Bwino, Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Meja Jenerali Paul Kisesa, Balozi wa Uganda nchini, Kanali Mstaafu, Fredy Mwesigye.

Bodi ya Psssf imesema itafanya Vizuri zaidi Katika Uendeshaji Wa Mfuko Huo

 Na Derek Murusuri, Kibaha, Pwani Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi Joyce Mapunjo ameihakikishia Menejimenti ya Mfuko huo ushirikiano wake ili kufikia malengo. Bi Mapunjo alikuwa anaongea katika mkutano wake wa kwanza na Wakurugenzi na Mameneja Mfuko huo, mwanzoni mwa wiki hii, baada ya kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya ya Wadhamini PSSSF, Desemba 2, 2024. “Niwahakikishie kuwa tutafanya vizuri zaidi, niko transparent na huwa sipendi majungu,” alisema na kuipongeza Menejiment ya Mfuko huo kwa kuwakutanisha Wakurugenzi pamoja na Mameneja wao, kwa mara ya kwanza toka Mfuko huo uanzishwe chini ya Sheria ya Hifadhi ya Jamii Kwa Watumishi wa Umma ya Mwaka 2018, wakakaa pamoja na kupitia mipango na bajeti zao pamoja. Bi Mapunjo alimpongeza Mkurugenzi Mkuu na Menejimenti ya PSSSF kwa kikao kazi [retreat] kinachoasisi mpango wa mabadiliko na kusema kuwa alijisikia vizuri sana kuanza majukumu yake kwenye Mfuko huo katika kipindi mu...

Rais Mwinyi:Smz Imevuka Lengo La Ilani Kwa Ujenzi Wa Barabara

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti  wa  Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein  Ali Mwinyi  amesema  Serikali imevuka  lengo la Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025 ilioainisha Ujenzi wa Kilomita 275 za barabara. Ameeleza kuwa Serikali   imeamua Kuongeza  idadi ya barabara  zitakazojengwa  Kwa kiwango cha lami hadi kufikia Kilomita 300 Mijini na Vijijini. Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo alipoifungua Barabara ya Ukutini  -Bandarini  Wilaya ya Mkoani Mkoa wa  Kusini Pemba tarehe 10 Januari 2025. Aidha , Rais Dk.Mwinyi amesema Mkataba wa Wananchi na Serikali yao ni Ilani ya Uchaguzi  hivyo kuna kila sababu ya  kujivunia  kwa yote yaliofanyika Katika Ujenzi wa Barabara. Akizungumzia barabara  ya Ukutini -Mtangani Bandarini  alioifungua amesema ni hatua muhimu ya kufungua fursa za Kiuchumi. Ameeleza kuwa mbali na Usafiri barabara hiyo ya Ukutini - Bandarini  itafungua Fursa za Ajira  kwa kuwa kuna Ban...

Nishati ya Uhakika inakuza Uchumi wa Nchi - Dkt. Biteko

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko Januari 10, 2025 amesema kuwa ukuaji wa uchumi wa nchi yoyote unategemea upatikanaji wa nishati ya uhakika na yenye gharama nafuu. "Kwa nchi yoyote inayotaka kukua kwa kiasi kikubwa inategemea Nishati inayopatikana kwa hakika na yenye bei nafuu, Bila nishati ya gharama nafuu, uchumi utabadilika na bidhaa zitazalishwa kwa gharama kubwa zaidi," amesema Dkt. Biteko. Dkt. Biteko amesisitiza kuwa serikali imejipanga kuhakikisha umeme wa uhakika unapatikana kwa gharama nafuu ili kuchochea Maendeleo ya kiuchumi na kuboresha maisha ya wananchi.