_▪️Asema mfumo huo utarahisisha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi_ _▪️Aonya tabia ya wagonjwa kupelekwa kununua dawa nje_ _▪️Asisitiza hospitali kutokuzuia miili ya marehemu kwa madai ya bili_ WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema utekelezaji wa mpango wa Bima ya Afya kwa Wote utaondoa changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi katika kupata huduma za matibabu nchini. Amesema hayo leo Jumamosi, Mei 16, 2026 alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kondoa Mjini katika Uwanja wa Puma mkoani Dodoma ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi. Waziri Mkuu amesema kupitia mfumo huo wananchi hawatalazimika tena kutumia gharama kubwa katika hatua mbalimbali za matibabu ikiwemo kumuona daktari, vipimo pamoja na ununuzi wa dawa. “Kwa kuwa tunakwenda kwenye utaratibu wa Bima ya Afya kwa Wote, baadhi ya haya mambo yaliyokuwa yanawasumbua wananchi yataenda kupata jawabu la kudumu,” amesema. Aidha, Waziri Mkuu amesema Serikali imeendelea kuboresha hudum...
Marato tv - Sauti ya Jamii