Skip to main content

Posts

Showing posts from October 6, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Tanroads na Benki ya Dunia Waimarisha Ushirikiano Katika Miradi ya Tantips

Dar es Salaam, 06 Oktoba 2025 Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), kupitia Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imepongeza ushirikiano thabiti kati yake na Benki ya Dunia katika kufadhili na kusimamia utekelezaji wa miradi saba ya maendeleo ya miundombinu ya barabara na viwanja vya ndege katika baadhi ya mikoa nchini. Akizungumza leo tarehe 06 Oktoba 2025 katika kikao cha ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi inayoendelea chini ya programu ya Tanzania Transport Integration Project for Sustainability (TANTIPS), Mkurugenzi wa Miradi ya Maendeleo wa TANROADS, Mhandisi Japherson Nnko, alisema ushirikiano huo ni mfano bora wa namna Tanzania na Benki ya Dunia wanavyotekeleza miradi ya kimkakati kwa pamoja ili kuboresha huduma za usafiri na usafirishaji kwa kuzingatia athari za mabadiliko ya tabianchi. Mhandisi Nnko alieleza kuwa miradi hiyo saba inafadhiliwa kwa jumla ya Dola za Marekani milioni 550, sawa na shilingi trilioni 1.3 za Kitanzania, ambapo mi...

Dkt. Nchimbi Ahitimisha Kampeni za Kumuombea Kura Dk.Samia Mkoani Tabora

Na Mwandishi Wetu MGOMBEA mwenza wa Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel John Nchimbi amehitimisha mikutano yake ya hadhara ya kampeni katika Mkoa wa Tabora huku akiacha ujumbe kuwa ifikapo Oktoba 29 mwaka huu wananchi wa mkoa huo wampigie kura mgombea urais wa Chama hicho Dk.Samia Suluhu Hassan. Dk.Nchimbi amehitisha ziara leo  Oktoba 6, 2025  katika Mkoa wa Tabora ambapo katika mikutano ya kampeni mbali ya kumuombea kura mgombea urais Dk.Samia Suluhu Hassan, wabunge na madiwani pia ametumia mikutano hiyo kunadi sera na Ilani ya uchaguzi mkuu ambayo imelenga kuleta maendeleo ya watanzania.  Akiwa katika mkutano wa kampeni Dk.Nchimbi kabla ya kuanza kuwahutubia Wananchi amesimikwa kuwa msaidizi wa Mtemi, kimila akiitwa 'MTONGI' baada ya mkubwa wake Chifu  Hangaya ambaye ni Raisi Dkt. Samia Suluhu Hassan. Dkt. Nchimbi amesimikwa na viongozi wa kimila wa Unyanyembe (Tabora) kwenye mkutano wake wa mwisho wa kampeni mkoani humo,katika kata ya Kigw...

Umoja wa Mataifa Walitunukia Jwtz Nishani ya Ulinzi Wa Amani Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati

Kikosi Cha Nane cha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (TANBAT 08), kinacholinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kimetunukiwa  Nishani za Ulinzi wa Amani na Umoja wa Mataifa (UN) kutokana na mchango wake mkubwa katika operesheni ya kulinda amani nchini humo chini ya mwavuli wa MINUSCA. Katika sherehe ya gwaride la heshima iliyofanyika tarehe 06 Oktoba 2025 mjini Berberati, wanajeshi zaidi ya 500 wa TANBAT 08 wametunukiwa nishani hizo ikiwa ni ishara ya kutambua michango yao  katika kuwalinda raia, kusaidia shughuli za kibinadamu, na kuimarisha utulivu katika maeneo yaliyoathiriwa na migogoro. Uvishwaji wa nishani hizo uliongozwa na  Naibu Mkuu wa Vikosi vya Kulinda Amani vya Umoja wa Mataifa nchini CAR,  Meja Jenerali Maychel Asmi, ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo.  Katika hotuba yake, Meja Jenerali Asmi ametoa pongezi kwa uongozi, nidhamu na mshikamano mkubwa uliodhihirishwa na TANBAT 08 wakati wa operesheni zao. > “Wanajeshi wa...

Dkt Nchimbi Asimikwa Kimila Kuwa 'mtongi' Msaidizi Wa Mtemi, Apewa Jina la 'nyungu ya Mawe'.

Mgombea mwenza wa kiti cha Uraisi kupitia chama cha mapinduzi Dkt. Emmanuel  John Nchimbi amesimikwa kuwa msaidizi wa Mtemi, kimila akiitwa 'MTONGI' baada ya mkubwa wake mtemi Hangaya ambaye ni Raisi Dkt. Samia Suluhu Hassan. Dkt. Nchimbi amesimikwa na viongozi wa kimila wa Unyanyembe (Tabora) kwenye mkutano wake wa mwisho wa kampeni mkoani humo,katika kata ya Kigwa jimbo la Igalula, wilaya ya Uyui nakupewa jina la "NYUNGU YA MAWE".