Skip to main content

Posts

Showing posts from November 10, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Jeshi la Polisi Kagera Limefanikiwa Kumkamata Mwalimu Anayetuhumiwa Kwa Ubakaji

 Na Angela Sebastian-Bukoba  Jitihada za waandishi wa habari za kupinga ukatili wa kijinsia zimezaa matunda mtuhumiwa  wa ubakaji  akamatwa. Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Blasius Chatanda  amethibitisha kukamatwa kwa   mwalimu wa taaluma Lameck Jonas wa shule ya msingi Rulanda kata ya Rulanda wilaya ya Muleba mkoani humo ambaye anatuhumiwa  kumbaka mwanafunzi wake muhitimu wa darasa la saba (13)  Akiongea kwa njia ya simu kamanda Chatanda,amesema  kwa jitihada za jeshi hilo wamefanya msako na kufanikiwa kumkamata na sasa yuko mikononi mwa jeshi hilo kwa ajili ya mahojiano zaidi. Kamanda Chatanda,anasema taratibu nyingine za kisheria zinaendelea na muda wowote mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayomkabili. Tukio hilo lilitokea Oktoba 30, mwaka huu majira ya jioni baada ya mtoto huyo akiwa na wanafunzi wenzake kufika shuleni hapo majira ya mchana kwa ajili ya kuomba mwalimu huyu awaangalizie matokeo ya mtihani wa darasa la...

Wakala wa Nishati Vijijini- REA Kuwanufaisha Wananchi Kupitia Programu ya Nishati Safi ya Kupikia

WANANCHI wa vitongoji elfu 20,000 kati ya 31,0000  ambavyo havijapata nishati ya umeme hapa nchini wanatarajia kunufaika na programu maalum ya kuwezeshwa huduma ya hutumia nishati safi yq kupikia,kupitia wakala wa nishati vijijini (REA), ambapo itasaidia kuchechemua shughuli za maendeleo. Hayo yamebainishwa na mkurugenzi mkuu wa REA, mhandisi Hassan Said katika kikao cha pili cha mwaka cha wadau wa maendeleo ya nishati vijijini kilicholenga kufanya tathimini ya mipango ya utekelezaji wa miradi kwa mwaka huu wa fedha. Kikao hicho kimefanyika  Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera ambapo Mhandisi Said amesema program hiyo imetokana na ubunifu wa Rais Samia Suluhu Hassan amba yeye anatamkwa kuwa kinara wa kampeni ya nishati safi hivyo Serikali yake na wafadhiri mbalimbali wamewezesha kufikia vitongoji 20,000.  Naye Mkuu wa mkoa wa Kagera Hajjat Fatma Mwassa amewahakikishia wadau wa maendeleo ya nishati kuwa fedha zinazotolewa zitaendelea kutukika kwa usahihi na uwepo wa umeme wa ...

Bashungwa achangisha Millioni 272 Jimbo Katoliki Bunda

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameshiriki Misa Takatifu katika Parokia ya Mtakatifu Paulo na kuongoza harambee ya kumalizia ujenzi wa jengo la ofisi za Jimbo Katoliki la Bunda ambapo jumla ya  Shilingi Milioni 272.6 imekusanywa. Harambee hiyo imefanyika leo Novemba 10, 2024 Wilayani Bunda Mkoani Mara ambapo pamoja na mambo mengine, Waziri Bashungwa amezindua ofisi ya Askofu wa Jimbo Katoliki la Bunda, Mhashamu Simon Chibuga Msondole ambayo itaanza kutoa huduma za kijamii na kiroho. “Jimbo letu la Bunda ni changa lina miaka 13, tunahitaji kubadilisha sura ya Jimbo letu, ili itakapofika Jubilei ya miaka 25, Jimbo liwe limepiga hatua kubwa na lenye kupendeza, lenye miundombinu mbalimbali kwa ajili ya huduma kwa watu wa Mungu na nchi yetu”, amesema Bashungwa Bashungwa amelishukuru Kanisa Katoliki nchini kwa kuendelea kushirikiana na Serikali katika shughuli za ustawi na maendeleo ya jamii katika Sekta ya Elimu, Afya, na Sekta za uzalishaji hususani kilimo, uwekezaji katika viwand...

Arafat aagwa Serengeti

  Na. Brigitha Kimario- Serengeti  Naibu Kamishna wa Uhifadhi na Maendeleo ya Biashara, Massana  Mwishawa ameongoza wadau wa uhifadhi, wananchi, ndugu wa marehemu, marafiki, maafisa na askari wa Hifadhi ya Taifa Serengeti kuuaga mwili wa Askari wa Uhifadhi daraja la tatu *CR III ARAFAT SAIDI MIYIMBA* (27) aliyefariki kwa kukanyagwa na Tembo jana tarehe 09.11.2024 wakati akitekeleza majukumu yake ya kuwarejesha tembo hifadhini baada ya kuvamia kijiji cha Mrito wilayani Tarime. Kwa niaba ya Kamishna wa Uhifadhi -TANAPA, Naibu Kamishna Mwishawa alisema kuwa kifo hicho cha ghafla kimeleta simanzi kubwa kwa TANAPA na wadau wa Uhifadhi nchini na ametoa pole kwa familia na watumishi wote wa Jeshi la Uhifadhi kwa kuondokewa na askari hodari na mchapakazi. Aidha, shirika linatambua mchango wake katika uhifadhi na sekta nzima ya utalii na itaendelea kuuenzi na kuuthamini. Pia Kamishna Mwishawa alitoa tahadhari kwa maafisa na askari kufanya kazi kwa uangalifu mkubwa ili kuepuka madh...

Waziri Mkuu atoa wito kwa viongozi wa vyama vya siasa

*_Awataka wawe vinara wa kulinda amani na kukemea viashiria vya uvunjifu wa amani_* WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa wito kwa Viongozi wa Vyama vya Siasa vitakavyoshiriki katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa, kuwa vinara katika kulinda amani na kukemea viashiria vyote vya uvunjifu wa amani. “Hamasisheni wanachama wenu kushiriki katika uchaguzi huo huku wakizingatia kudumisha amani iliyopo. Wananchi wote waliojiandikisha katika orodha ya wapigakura wa Uchaguzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa wajitokeze kwa wingi kupiga kura katika vituo vyao siku ya Jumatano tarehe 27 Novemba, 2024. Siku hiyo itakuwa ya mapumziko maalum kwa ajili ya uchaguzi huo.” Ametoa wito huo leo (Jumapili, Novemba 10, 2024) wakati alipomwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano Mkuu na Kongamano la Umuhimu wa Amani kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, jijini Dar es Salaam. “Mheshimiwa Rais Dkt. Samia amewasihi Watanzania na viongozi wa dini kuendelea kuitangaza amani ndani na nje.” Kati...