Skip to main content

Posts

Showing posts from March 12, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Majaliwa Azindua Kituo cha Mabasi Nzega Mjini

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Machi 13, 2025 amezindua kituo kipya cha Mabasi cha Nzega mjini,katika wilaya ya Nzega mkoani Tabora ambacho ujenzi wake umegharimu shilingi bilioni 4.327. Akizungumza baada ya kuzindua kituo hicho ambacho utekelezaji wake umefikia asilimia 100, Mheshimiwa Majaliwa ameipongeza halmashauri hiyo kwa uamuzi wa ujenzi wa kituo hicho kwani kitaibua fursa za biashara kwa wakazi wa eneo hilo. “Kituo hiki ni kizuri na kimejengwa kwa ubora, kituo hiki kinatakiwa kianze kutumika ili wananchi waanze kunufaika nacho, Watumishi wa halmashauri ongozeni Wana-Nzega kunufaika na fursa katika eneo lenu” Aidha, Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa halmashauri hiyo kuongeza vibanda vya wafanyabiashara badala ya vichache ambavyo vimejengwa mpaka sasa. “Tunataka wananchi wengi zaidi wanufaike, ongezeni vibanda, huu ni ubunifu mzuri sana utasababisha wengi wanufaike, waleteni wajasiriamali hapa wapate rizki zao, mkifanya hivyo mtaongeza mzunguko wa fedha” Kadhalika, Mheshimiwa...

Dkt. Biteko Awasili Barbados Kunadi Nishati Safi Kimataifa

  Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewasili nchini Barbados kushiriki Mkutano wa Kimataifa kuhusu matumizi ya Nishati endelevu utakaofanyika katika jiji la Bridgetown kuanzia tarehe 12 hadi 14 Machi, 2025. Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Grantley Adams nchini humo, Dkt. Biteko amepokelewa na Waziri wa Nishati wa Nchi hiyo Mhe. Lisa Cummins pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Cuba na mwakilishi katika eneo la Caribean, Mhe. Humphrey Polepole Aidha, Dkt. Biteko atashiriki katika majadiliano mbalimbali kuhusu matumizi ya Nishati endelevu kimataifa ikiwemo Nishati safi ya kupikia ambayo ni ajenda muhimu kwa ajili ya kuwakomboa wananchi dhidi ya matumizi ya nishati isiyokuwa safi. Dkt. Biteko ameongozana na Mshauri wa Rais masuala ya Wanawake, Mhe. Angellah Kairuki, Waziri wa Maji, Nishati na Madini Zanzibar, Mhe. Shaib Hassan Kaduara na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mha. Felichesmi Mramba.

Wachimbaji wadogo wampa Tano Rais Samia

  · *Umeme mgodini ‘kicheko’* · *Uzalishaji waongezeka 70%* WACHIMBAJI wadogo wa Mgodi wa Dhahabu wa Basia uliopo kijiji cha Mwanubi Wilaya ya Shinyanga Vijijini wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapelekea huduma ya umeme katika mgodi huo. Akizungumza Mwenyekiti wa Mabroka Mkoa wa Shinyanga (CHAMATA) Masanja Meja  amesema kupitia Tume ya Madini imewasaidia  kupata miundombinu ya umeme katika mgodi huo na wameweza kuokoa  gharama za uendeshaji kwa zaidi ya asilimia 70. “Umeme unatusaidia sana katika uchenjuaji, siku za nyuma kwa siku  tulikuwa tunatumia lita 20 za dizeli ambayo kwa siku si chini ya shilingi  70,000  kwa mwezi ni Shilingi  milioni 2.1 lakini kwa sasa tunatumia umeme wa Shilingi 15,000 kwa siku kwa mwezi ni Shilingi 450,000 kwetu ni nafuu kubwa,”amesema Meja. Aidha, amesema kutokana na miundombinu hiyo ya umeme uzalishaji umeongezeka kutoka  gramu 300 kwa mwezi  mpaka g...

Majaliwa: Serikali utaendeleza Mikakati ya Kukuza Sekta ya Mifugo

 *Asisitiza kuwa mifugo ni uchumi, ajira na biashara *Atoa wito kwa wakulima na wafugaji wawe wamoja   WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali inaendelea kuweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha sekta ya mifugo inakuwa endelevu na yenye tija. Amesema kuwa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan mara zote ameweka msisitizo katika kuiendeleza sekta hiyo kwa kuwa mifugo ni uchumi, ajira na ni biashara. Ameyasema hayo kwa nyakati tofauti alipozungumza na wananchi katika mikutano aliyoifanya jana Jumatano (Machi 12, 2025) Wilayani Igunga, mkoani Tabora ambapo yupo kwenye ziara ya kikazi ya siku mbili. “Tunawahamasisha wafugaji, fugeni mifugo ni uchumi, mifugo ni maisha na mifugo ni pesa na wakulima limeni tupate mazao mengi ya chakula na biashara na ni lazima wafugaji na wakulima tuelewane.” Katika hatua nyingine Mheshimiwa Majaliwa amezitaka halmashauri zote nchini kuweka mikakati ya kuhakikisha wanakuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na kuzisimamia fursa zilipo kwenye maeneo ya...

Kamati ya Bunge yapongeza Jwtz kwa Ujenzi wa Makao Makuu

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama imefanya ziara kutembelea ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa, Dodoma Machi 12-2025 na kupongeza mafanikio yaliyofikiwa. Akizungumza kwa niaba ya Kamati, Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni  Mbunge wa Namtumbo Mheshimiwa Vita Kawawa amempongeza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali Salum Haji Othman kwa mafanikio makubwa ya ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa. Kamati hiyo imelipongeza JWTZ kwa kukidhi vigezo vya ujenzi, ubora wa jengo na imeahidi kuendeleza ushirikiano ili kufikia lengo lililokusudiwa. Kwa upande wake Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali Salum Haji Othman ameishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwezesha ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa kwani ni mafanikio makubwa kwa JWTZ kuwa na Makao Makuu ya Jeshi yaliyojengwa kwa kiwango cha Kimataifa....

Aliyeangua Kilio Akisubiri Hukumu, Afungwa Miaka 30 Jela Kwa Kubaka Mwanafunzi

  Na Dawati la Habari Polisi ;Mwanza Katika hali isiyo ya kawaida, mkazi wa Kijiji cha Mwanekeyi, Wilaya ya Kwimba, mkoani Mwanza, Shaban  Lyahasi (24), ameangua kilio mahakamani alipotakiwa kujitetea kabla ya kusomewa hukumu katika kesi ya ubakaji iliyokuwa inamkabili. Lyahasi amesomewa hukumu hiyo katika Mahakama ya Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza na kupewa adhabu ya kifungo cha miaka 30 jela baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wa darasa la saba, (15), (jina linahifadhiwa kwa sababu za kisheria). Hukumu hiyo katika kesi namba 26610/2024 imesomwa leo Machi 12,2025 na Hakimu mkazi mwandamizi, John Chai Jagadi wa mahakama hiyo  mbele ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Juma Kiparo. Imedaiwa mahakamani hapo kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo tarehe 05. 09. 2024 huko katika Kijiji cha Mwamanga Wilayani humo ndani ya chumba chake huku akimuahidi binti huyo kuwa atamuoa kinyume na kifungu 130 (1)(2)(e) na 131(1) vya kanuni ya Adhabu, sura ya 16 ya sheria mareje...

Rc Mtambi Ahamasisha Wanawake Kukopa Mikopo isiyo na Riba Kwenye Halmashauri

  Na Shomari Binda-Musoma  MKUU wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi amewahamasisha wanawake wajasiliamali kukopa mikopo isiyokuwa na riba kutoka kwenye halmashauri. Kauli hiyo imetolewa leo machi 12,2025 kwa niaba yake na Kaimu Katibu Tawala wa mkoa wa Mara Omary Gamuya alipokuwa akifunga kongamano la wanawake wajasiliamali kwenye ukumbi wa uwekezaji.  Amesema hadi sasa kupitia halmashauri zake 9 tayari mikopo ya zaidi ya shilingi bilioni 2 imetolewa kwa makundi ya wanawake,vijana na wenye ulemavu na kuendesha biashara zao. Mtambi amesema mkoa wa Mara unazo fursa nyingi za biashara ambazo wanawake wajasiliamali wanaweza kuzifanya na suala la mitaji ni vyema kufatilia mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri. Amesema mikopo ya mitaani yenye riba kubwa imekuwa ikiwarudisha nyuma wanawake wengi na kushauri kuachana nayo kwa kuwa haina faida. Aidha amesema yapo masoko ya nchi jirani ambayo Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ameweka mazingira mazuri ya kufanya biashara ambay...