Skip to main content

Posts

Showing posts from September 4, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt Nchimbi Aitikisa Kahama Aeleza Sababu ya Dkt Samia Kuchaguliwa Tena

Mgombea Mwenza wa Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi  akiwahutubia Wananchi wa Kahama mjini, jimbo la Kahama, leo Alhamis Septemba 4,2025,mkoani Shinyanga. Dkt Nchimbi akihutubia Maelfu ya Wana kahama amesema Dkt Samia anayo kila Sababu ya kupigiwa kura ya ndio katika Uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, kwa Sababu amejipambanua katika Kushughulikia kero na Changamoto mbalimbali za Wananchi, pamoja na kufungua fursa kwa Watanzania. Pamoja na mambo mengine Dkt Nchimbi pia aliwanadi wagombea Ubunge,akiwemo Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kahama mjini,Benjamin Lukubha Ngayiwa ,pamoja na Madiwani. Balozi Dkt.Emmanuel Nchimbi anaendelea na mikutano yake ya Kampeni Mkoani Shinyanga ya kuinadi Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030, ambayo inalenga kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa Maendeleo katika miaka mitano ijayo huku akitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais wa CCM, Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan, Wabunge na Madiwani wa Chama hicho kwa ...

Nld Yamtaja Rais Samia Kama Kiongozi Mwenye Kujali Haki na Usawa

  Na MASHAKA MHANDO, Tanga NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha National League for Democracy (NLD) Zanzibar Ahmed Salim Hamad amesema wanamshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwapa magari wagombea wa vyama vingine ili wajinadi katika kampeni zinazoendela kabla ya uchaguzi Mkuu Oktoba 29 mwaka huu. Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni za chama hicho zilizofanyika kwenye uwanja wa Komesho Jijini Tanga,  Leo Septemba 4 Hamad alisema kitendo kilichofanywa na mgombea wa Chama Cha Mapinduzi ni kitendo cha kuimarisha demokrasia nchini ukomavu wa kisiasa. Alisema Rais Dkt Samia kwa kitendo hicho ameonesha kwamba anakwenda kufanya uchaguzi wa haki na usawa kwa wagombea wote na chama hicho kinampongeza kwa uwamuzi huo. "Mama yetu mama Samia (Dkt Samia Suluhu Hassan) amekusudia kufanya uchaguzi wa haki, nampongeza sana, haijawahi kutokea mgombea unashindaba naye kutaka nafasi yake halafu anakupa gari linalofanana na analopanda yeye, huku ni kuinarisha demokrasia nchini," alisema Hama...

Rais Mwinyi Afungua Soko la Kisasa Chuini

Zanzibar | 04 Septemba 2025 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amefungua rasmi Soko na Kituo cha Mabasi cha Kisasa Chuini, Wilaya ya Magharibi A, Mkoa wa Mjini Magharibi. Katika hotuba yake, Rais Dkt. Mwinyi ameagiza kuimarishwa kwa usafi, kuzuia biashara nje ya maeneo rasmi, kutoza kodi nafuu, na kufanya ukarabati wa mara kwa mara ili masoko yabaki katika hali nzuri.  Halikadhalika, amesisitiza uharakishwaji wa kuwaingiza wafanyabiashara sokoni na kuanza mara moja kwa huduma za kituo cha mabasi. Aidha, amezitaka taasisi za kifedha kuwawezesha wajasiriamali kupata mikopo na kuahidi kuwa Serikali itaendelea kujenga masoko ya kisasa katika maeneo mengine ikiwemo Mombasa, Kibanda Maiti na Malindi. Soko la Chuini lina maduka 98, maghala, maegesho ya magari na vyoo 26, na limejengwa na Kikosi cha Zimamoto na Uokozi.

Dkt. Biteko Amwakilisha Rais Samia Mazishi ya Hayati Askofu Shao

📌 Awataka Watanzania kuacha alama katika utumishi wao 📌 Asema Serikali iko pamoja na wafiwa katika kipindi hiki cha majonzi 📌 Askofu Malasusa ataka waumini kumshuhudia Kristo kwa vitendo Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ibada ya mazishi ya Askofu Mstaafu Dkt. Martin Fatael Shao aliyefariki Dunia Agosti 25, mwaka huu. Akizungumza katika ibada ya mazishi Septemba 4, 2025 yaliyofanyika katika kijiji cha Lole, Wilaya ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro Dkt. Biteko amesema Hayati Askofu Shao wakati wa uhai wake alifanya mambo mengi mazuri ya kukumbukwa hata baada ya kifo chake. “ Mzee wetu, Hayati Askofu Shao ameanza kazi za kanisa akiwa kijana na amefanya kazi kubwa ambayo kila mmoja anaishuhudia leo, ameacha alama inayotokana na kazi aliyoifanya, amesema “Mheshimiwa Rais amenituma niwaletee salamu zake za pole nyingi sana Wanafamilia, Viongozi wote wa Ka...