Skip to main content

Posts

Showing posts from July 18, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

OPARESHENI YA UHAMIAJI YALALAMIKIWA KYERWA

 Na Na Angela Sebastian ;Kagera  Wananchi wa Kijiji cha Kaitambunzi, Kata ya Isingiro wilayani Kyerwa, wameiomba Serikali kuchunguza utaratibu unaotumiwa na baadhi ya maafisa wa Uhamiaji wakati wa operesheni za usiku za kusaka wahamiaji haramu, wakidai zimekuwa zikisababisha hofu hata kwa raia wasiokuwa na makosa. Kero hiyo iliwasilishwa katika mkutano wa hadhara wa Mbunge wa Jimbo la Kyerwa, Khalid Nsekela, ambapo wananchi walisema wanaunga mkono juhudi za Serikali za kudhibiti uhamiaji haramu, lakini wakasisitiza operesheni zifanyike kwa kuzingatia sheria, taratibu na haki za wananchi. Alistidia Mbatina ni mkazi wa kijiji hicho amesema kuwa licha ya kuunga mkono juhudi za Serikali za kudhibiti uhamiaji haramu, wanahitaji operesheni hizo kufanyika kwa kuzingatia sheria, taratibu na haki za wananchi ili kuepusha taharuki na hofu isiyo ya lazima ambayo inawakabili kwa sasa. "Operesheni zinazofanyika nyakati za usiku wa manane zimekuwa zikitutia hofu,wanakuja watu wanakamat...

MATAIFA YA TANZANIA NA MISRI YAKUBALIANA MAKUBWA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, na Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Abdel Fattah El-Sisi, wamefungua ukurasa mpya wa ushirikiano wa kimkakati kwa kusaini makubaliano yatakayoongeza kasi ya maendeleo katika sekta za biashara na uwekezaji, kilimo, uchukuzi, afya, elimu na nishati. Makubaliano ambayo yanatarajiwa kuimarisha uchumi wa mataifa yote mawili na kufungua fursa mpya za maendeleo kwa wananchi. Akizungumza Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya mazungumzo rasmi na mgeni wake aliyekuwa katika ziara ya kikazi ya siku moja nchini, Rais Samia amesema ushirikiano kati ya Tanzania na Misri tayari umezaa matokeo makubwa, ikiwemo kuwapatia huduma za upasuaji wa kwa wagonjwa wa moyo wa kitanzania wapatao  420 pamoja na utekelezaji wa Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) wenye thamani ya takribani shilingi trilioni 7.4. Rais Samia pia amesema viongozi hao wamekubaliana kuendeleza maboresho ya Bandari ya Bagamoyo kwa kuiunganisha na mtandao w...

VIJANA 400 WAPEWA LESENI ZA UCHIMBAJI MADINI WILAYANI KWIMBA MKOANI MWANZA

 ▪️Ni Maelekezo ya Rais Samia kufuta Leseni zisizo fanyiwa kazi na kuwapa wachimbaji wadogo ▪️Ni Leseni kubwa ya Utafiti (Ekari 5,441) iliyofutwa na kurudishwa Serikalini  ▪️Waziri Mavunde aelekeza STAMICO kupeleka Mtambo wa kuchoronga Mwanza ▪️ Zoezi la Kufuta Leseni zisizofanyiwa kazi kuendelea nchi nzima Kwimba,Mwanza Serikali imeendeleza jitihada zake za kukuza Sekta ya Madini na kuwasaidia wachimbaj wadogo chini ya uongozi wa Rais Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kugawa Leseni ndogo za Uchimbaji Madini (PML) kwa wachimbaji wadogo ili kuwapa fursa ya kuchimba kwenye maeneo yao wenyewe jambo ambalo litapunguza migogoro ya uvamizi wa Leseni na kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na uchumi wa jumla. Zoezi hilo limeongozwa na Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde (Mb) Leo tarehe 18 Julai 2026 Wilayani Kwimba Mkoani Mwanza, ambapo Jumla ya Leseni 30 za uchimbaji zimegawiwa kwa wachimbaji wadogo wapatao 400 wa Wilaya ya Kwimba na Leseni hizo zinatokana na Leseni kubwa ya utafiti...

RC MTAKA: MALEZI YENYE MAADILI NI UWEKEZAJI WA TAIFA LA KESHO

MKUU wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, amewataka wazazi na walezi nchini kuweka kipaumbele katika malezi ya watoto kwa kuzingatia maadili, mila na desturi za Kitanzania, akisisitiza kuwa familia ndiyo msingi wa kujenga kizazi chenye nidhamu, uzalendo na uwezo wa kuliletea taifa maendeleo endelevu. Akizungumza wakati wa ziara yake ya kikazi katika Halmashauri ya Mji Njombe, Mhe. Mtaka amesema wazazi na walezi wana wajibu mkubwa wa kuhakikisha watoto wanalelewa katika mazingira salama, yenye upendo, nidhamu na maadili mema yatakayowawezesha kukua wakiwa raia wema, wenye kuwajibika na kuheshimu sheria za nchi. Amesema malezi bora hayaishii katika kuwapatia watoto mahitaji ya msingi kama chakula, mavazi, makazi na elimu, bali yanapaswa kuambatana na kuwafundisha heshima, uwajibikaji, uzalendo, uadilifu, uchapakazi na kuheshimu utu wa wengine ili waweze kuwa nguzo ya maendeleo ya jamii na taifa. "Mtoto mwenye malezi bora anakuwa mwananchi mwema na kiongozi bora wa kesho. Ni jukumu...

MAKONDA: UWEKEZAJI WA AFYA WAIFANYA DIRA YA TAIFA 2050 KUWA HALISI

Na Mwandishi Wetu, Arusha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, ambaye pia ni Mbunge wa Arusha, Paul Christian Makonda, ameridhishwa na maboresho yanayoendelea katika Hospitali ya Arusha Lutheran Medical Center inayotoa huduma kwa ushirikiano na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete, ALMC–JKCI Arusha. Maboresho hayo yanafanyika kwa uwezeshaji wa Global Medicare, kwa lengo la kuongeza ubora wa huduma za afya, kuboresha mazingira ya matibabu, kuimarisha utalii tiba na kuiandaa hospitali kutoa huduma zinazokidhi viwango vya kimataifa kuelekea mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2027. “Lengo kubwa ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora kabisa na katika mazingira mazuri. Vilevile tunataka kuimarisha utalii tiba na kutengeneza mazingira mazuri kwa ajili ya AFCON 2027,” alisema Mhe. Makonda.  Makonda alimshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwekeza katika sekta ya afya na kuruhusu taasisi za kibingwa kama JKCI kupanua huduma zake hadi mikoani. Kwa upand...

SIKIA! POLISI YAKAMATA WATU 200, WATATU WAHUKUMIWA JELA MIAKA 30

Na MASHAKA MHANDO,Tanga JESHI la Polisi Mkoa wa Tanga limewakamata watuhumiwa 200 wanaodaiwa kufanya makosa mbalimbali ya jinai, huku wengine 51 wakihukumiwa vifungo gerezani, wakiwemo watatu waliohukumiwa miaka 30 kwa makosa ya kulawiti, kuzini na maharimu, na kusafirisha dawa za kulevya. Akitoa taarifa ya hali ya ulinzi na usalama kwa waandishi wa habari mkoani humo jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, ACP Almachius Mchunguzi, amesema mafanikio hayo yametokana na operesheni na doria zilizofanyika kuanzia Juni Mosi hadi Julai 16, mwaka huu.  Kamanda Mchunguzi amebainisha kuwa, licha ya matukio hayo, hali ya usalama mkoani Tanga ni shwari na Jeshi hilo linaendelea kutoa elimu kupitia falsafa ya Polisi Jamii. Akifafanua kuhusu watuhumiwa 51 waliohukumiwa baada ya upelelezi kukamilika, Kamanda Mchunguzi amewataja waliohukumiwa kifungo cha miaka 30 gerezani kuwa ni Julius Mustafa aliyepatikana na hatia ya kulawiti, Kilimo Issaya aliyepatikana na hatia ya kuzini na maharimu, na Sadik...