Skip to main content

Posts

Showing posts from June 27, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

WAZIRI MBARAWA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MRADI WA MATANKI YA KUHIFADHIA MAFUTA KIGAMBONI*

Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Prof. Makame Mnyaa Mbarawa, leo Juni 27,2026 ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa matanki ya kuhifadhia mafuta katika eneo la Kigamboni, Dar es Salaam, ambapo ameridhishwa na kasi na ubora wa utekelezaji wa mradi huo.  Mradi huo unafadhiliwa kwa asilimia 100 na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ukiwa ni sehemu ya uwekezaji mkubwa unaolenga kuimarisha miundombinu ya bandari na sekta ya nishati ili kuongeza ufanisi wa uchumi wa Taifa. Baada ya kukamilika, matanki hayo 15 yatakuwa na uwezo wa kuhifadhi takribani mita za ujazo 378,000 za mafuta, hatua itakayoongeza uwezo wa nchi kuhifadhi mafuta ya akiba, kupunguza muda wa kusubiri kwa meli bandarini, kupunguza gharama za usafirishaji wa mafuta, kuimarisha usalama wa nishati nchini na kuongeza mapato ya Serikali kupitia huduma za bandari. Mradi huo pia unatarajiwa kuifanya Tanzania kuwa kitovu muhimu cha biashara ya mafuta katika ukanda wa Afrika Mash...

DKT. MWIGULU: SERIKALI YAHAKIKISHA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO SINGIDA

 WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali itaendelea kutekeleza miradi ya maendeleo iliyoahidiwa katika Mkoa wa Singida, ikiwemo barabara, reli ya kisasa (SGR), uwanja wa ndege pamoja na miradi ya maji, afya na elimu kwa lengo la kuchochea maendeleo ya wananchi na kukuza uchumi wa Taifa. Ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Juni 27, 2026) alipohutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Maonesho wa Mandewa, wilayani Ikungi, mkoani Singida, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani humo. Waziri Mkuu amesema Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amemtuma kuwahakikishia wananchi wa Mkoa wa Singida kuwa miradi yote ya maendeleo iliyoahidiwa itaendelea kutekelezwa hatua kwa hatua kwa kuzingatia vipaumbele vya Serikali. "Mheshimiwa Rais amenituma niwahakikishie kwamba mambo ambayo wabunge wenu wamekuwa wakiyasema na ambayo aliwaahidi wananchi wa Singida yatakwenda kutekelezwa," amesema. Amesema Serikali itaendelea kutekeleza miradi ya barabara ikiwemo Saba...

WAZIRI WA FEDHA AONGOZA MBIO ZA SHUKRANI KWA MLIPAKODI KUELEKEA TUZO YA RAIS KWA MLIPAKODI BORA NA MAADHIMISHO YA MIAKA 30 YA TRA

 Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) leo tarehe 27 Juni 2026 imefanya Mbio na Matembezi ya Shukrani kwa Mlipakodi katika mikoa yote nchini ikiwa ni sehemu ya shughuli za kuelekea Utoaji wa Tuzo ya Rais kwa Mlipakodi Bora na Maadhimisho ya Miaka 30 ya TRA yatakayofanyika Julai 1, 2026. Katika Mkoa wa Dar es Salaam, mbio hizo zimefanyika katika Viwanja vya Gymkhana na kuhudhuriwa na watumishi wa TRA, wadau mbalimbali, wafanyabiashara na walipakodi. Mgeni rasmi alikuwa Mheshimiwa Balozi Khamis Mussa Omary, Waziri wa Fedha, ambaye aliongoza mbio hizo na kushiriki matembezi ya shukrani pamoja na mamia ya washiriki. Mbio na matembezi hayo yamefanyika kwa lengo la kutoa shukrani kwa walipakodi kwa mchango wao mkubwa katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali na maendeleo ya Taifa, sambamba na kuhamasisha ushiriki wa wadau katika Maadhimisho ya Miaka 30 ya TRA na hafla ya Tuzo ya Rais kwa Mlipakodi Bora. 

CG MWENDA AWATAKA WASTAAFU WA TRA KUWA MABALOZI WA KODI

 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Yusuph Juma Mwenda amewataka watumishi wastaafu wa Mamlaka hiyo kuwa Mabalozi wa Kodi ili kuongeza uelewa wa umuhimu wa kulipa kodi kwa jamii na kuhamasisha ulipaji wa kodi kwa hiari.  Ameyasema hayo Juni 26, 2026 jijini Dar es Salaam katika hafla ya kuwashukuru Wastaafu kwa mchango wao wa kuijenga TRA ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 30 ya Mamlaka hiyo tangu kuanzishwa kwake na utolewaji wa Tuzo za Rais kwa Mlipakodi Bora zinazotarajiwa kutolewa Julai Mosi mwaka huu kwenye ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.  Akizungumza katika hafla hiyo Kamishina Mkuu amesema TRA inatambua na kuthamini mchango wa wastaafu hao kwa kujenga msingi imara wa mafanikio ya miaka 30 ya taasisi hiyo. Amesema mafanikio yaliyofikiwa leo hayawezi kutenganishwa na kazi kubwa iliyofanywa na watumishi waliowahi kuitumikia taasisi hiyo. “Leo tumewaalika ili kuwashukuru kwa kazi kubwa mliyoifanya katika kipindi cha miaka 30 ya TRA, ...

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA AHITIMISHA MAFUNZO YA CHUO CHA UKAMANDA NA UNADHIMU DULUTI

 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Rhimo Nyansaho (Mb), tarehe 27 Juni, 2026 amehitimisha rasmi mafunzo ya mwaka mmoja ya Kozi ya Ukamanda na Unadhimu katika Mahafali ya 40 ya Chuo cha Ukamanda na Unadhimu Tanzania, yaliyofanyika katika chuo hicho kilichopo Duluti, mkoani Arusha. Mahafali hayo, ambayo Dkt. Nyansaho alikuwa Mgeni Rasmi, yalihusisha jumla ya maafisa wahitimu 82 kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) pamoja na maafisa kutoka nchi mbalimbali rafiki. Mbali na kuhitimu Kozi ya Ukamanda na Unadhimu, wahitimu hao pia walitunukiwa Shahada za Umahiri na Stashahada katika Masuala ya Ulinzi na Usalama, mafunzo yaliyotolewa sambamba na kozi hiyo ili kuwawezesha kupata maarifa ya kina kuhusu masuala ya ulinzi, usalama na uongozi wa kimkakati. Akizungumza katika mahafali hayo, Waziri wa Ulinzi na JKT aliwapongeza wahitimu kwa mafanikio yao, akieleza kuwa kuhitimu kozi hiyo ni ushahidi wa bidii, nidhamu, ujasiri, uthabiti na kujitolea kwao katika kipindi chote ...