Skip to main content

Posts

Showing posts from August 24, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

SERIKALI YATAKA DAWA ZINAZOTENGENEZWA NA WABUNIFU WA NDANI, ZISIITWE ZA ASILI

 Na MASHAKA MHANDO, Tanga  Serikali imetoa maagizo kwa wizara na taasisi za utafiti nchini kuhakikisha zinakamilisha taratibu zote za kimataifa za kupata ithibati, ili dawa zinazotokana na mimea zikishapita maabara na kuzalishwa viwandani ziache kuitwa 'dawa za asili' na badala yake zitambulike kama dawa za kisasa kutoka Tanzania. Maagizo hayo yametolewa leo Augosti 24 na Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, jana wakati akifunga kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi, na Ubunifu yaliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara jijini Tanga kuanzia Agosti 18 hadi 24, mwaka huu.  Akifafanua kuhusu dhana hiyo, Dkt. Mwigulu alitolea mfano dawa ya kutibu tezi dume iliyotengenezwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), akieleza kuwa kuendelea kuziita 'dawa za asili' kunawafanya baadhi ya watu kuwa na ukakasi na mashaka nazo, licha ya kuwa zimepitia michakato yote ya kimaabara kama dawa nyingine za kigeni. "Tuendelee kufanya ...

PAMPU 113 ZA UMWAGILIAJI ZAKABIDHIWA KWA WAKULIMA WADOGO MARA.

 Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mheshimiwa Kanali Evans Alfred Mtambi, leo tarehe 24 Agosti 2026, amezindua na kuongoza hafla ya ugawaji wa pampu 113 za umwagiliaji kwa wakulima wadogo wa Mkoa wa Mara, iliyofanyika katika viunga vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara. Hafla hiyo imeandaliwa na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali za kuimarisha kilimo cha umwagiliaji na kuongeza uzalishaji wa mazao. Akizungumza katika hafla hiyo, Mheshimiwa Kanali Mtambi amewahimiza wananchi wa Mkoa wa Mara, hususan wakulima, kutumia kikamilifu fursa zinazotolewa na Serikali kwa kuwekeza katika kilimo cha umwagiliaji ili kuongeza uzalishaji wa mazao, kuimarisha usalama wa chakula na kuinua uchumi wa wananchi. Aidha, amemshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuupa kipaumbele Mkoa wa Mara kupitia uwekezaji katika sekta mbalimbali za maendeleo ikiwemo kilimo, afya, elimu, miundombinu na hu...

WAZIRI MKUU ATAKA UBUNIFU UPELEKWE SOKONI*

 WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba ameitaka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na taasisi zake kuhakikisha bunifu zinazozalishwa na Watanzania haziishii kuonyeshwa kwenye maonesho, bali zinaendelezwa, zinalindwa na kupelekwa sokoni ili zitoe suluhisho kwa changamoto mbalimbali na kuchangia ukuaji wa uchumi wa Taifa. Waziri Mkuu ametoa maelekezo hayo leo, Jumatatu, Agosti 24, 2026, jijini Tanga wakati akihitimisha Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu, akisisitiza umuhimu wa kujenga mfumo unaowawezesha wabunifu kubadilisha mawazo yao kuwa bidhaa na huduma zenye tija. Amesema Tanzania ina wabunifu wenye uwezo mkubwa katika maeneo mbalimbali, hivyo hatua inayohitajika sasa ni kuhakikisha ubunifu huo unavuka hatua ya kuoneshwa kwenye maonesho na kufikia hatua ya kutumika, kuzalishwa kwa wingi na kuuzwa sokoni. “Ni lazima tuvuke kwenye maonesho, twende kwenye uhalisia wa maisha kwamba hivi vitu ambavyo tunavionyesha kwenye maadhimisho kama haya sasa viende kwenye utarati...

CHRISTIAN BELLA KUTIKISA THE EMBASSY HALL IJUMAA HII

 Na Mwandishi Wetu MSANII maarufu wa muziki Christian Bella akiwa sambamba na bendi yake ya Malaika wanatarajiwa kukonganyogo za wananchi wa Dar es Salaam siku ya Ijumaa tarehe 28 katika ukumbi wa The Embassy Mbezi Kimara kwa Msuguri. Akizungumza na waandishi wa habari jana, Edwin Bagenyi ambaye ni Meneja wa Embassy Hall alisema maandalizi yote yamekamilika na wananchi watakaofika watapata burudani ya kutosha kutoka kwa mwanamuziki huyo. Alisema kwa muda mrefu wananchi wa Kimara Mbezi na maeneo mengine ya jijini Dar es Salaam wamekuwa na shauku ya kumwona msanii huyo akitumbuiza maeneo hayo. “Kwa muda mrefu tumepokea maombi ya wananchi wakitaka kumwona Christian Bella akitumbuiza kwenye ukumbi wetu wa kisasa kabisa wa Embassy kwa hiyo tumeona tusiwanyime raha wateja wetu tumeona aje tushirikiane kupendezesha siku hiyo” alisema  “Tumejiandaa vya kutosha watu watapata burudani ambayo wameililia kwa muda mrefu sana tunawaahidi wateja wetu kuwa burudani wanayoitarajia wataipata...