Skip to main content

Posts

Showing posts from August 21, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Kombo Awakaribisha Wawekezaji wa Japan

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo amewakaribisha wawekezaji wa Japan kuja Tanzania kufanya uwekezaji mkubwa kupitia mfumo wa Ushirikiano wa Sekta Binafsi na Umma (PPP) katika sekta za kilimo, uzalishaji, madini, uunganishaji wa vifaa na miundombinu ikiwemo miradi mikubwa ya uendelezaji wa bandari ya Dar es Salaam na reli ya kisasa (SGR) awamu ya sita na saba.  Mheshimiwa Balozi Kombo ametoa mwaliko huo Agosti 21, 2025 nchini Japan alipokutana na kuzungumza na Shirikisho la kampuni za wawekezaji wa miundombinu la Japan (JAIDA) ambalo linajumuisha takriban kampuni 190 na Wenyeviti wenza wa Kamati ya Afrika ya Shirikisho la wawekezaji la KEINDAREN ambalo linajumuisha takriban kampuni 1,500.  Katika mazungumzo yake na wawekezaji hao, Mheshimiwa Waziri Kombo amesisitizia nia ya Tanzania ya kutumia ushirikiano wa Tanzania na Japan katika sekta za kimkakati kama alama kuu ya ushirikiano wa Japan na Afrika. Vilevile, amesisitizia umuh...

Rais Mwinyi:Zanzibar Inahitaji Fursa za Uwekezaji

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema kuwa Zanzibar inahitaji fursa za uwekezaji katika sekta mbalimbali ikiwemo Uchumi wa Buluu, sekta ya miundombinu, afya pamoja na fursa za kibiashara kwa ajili ya kuongeza thamani ya bidhaa za karafuu na mazao ya baharini. Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo alipokutana na Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk, aliyefika Ikulu Zanzibar tarehe 19 Agosti 2025 kumuaga baada ya kuteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Aidha, Rais Dkt. Mwinyi ameeleza kuwa sera ya diplomasia ya uchumi ndiyo iliyopewa kipaumbele hivi sasa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo ni vema Balozi huyo kuifanyia kazi sera hiyo ili uchumi wa Tanzania hususan Zanzibar uendelee kuimarika. Naye Balozi Mbarouk amemhakikishia Rais Dkt. Mwinyi kwamba ataendelea kuimarisha zaidi mahusiano pamoja na kutafuta fursa mbalimbali za ushirikiano.

Maabara ya Kisasa Geita Kuwainua Wachimbaji Kanda ya Ziwa – Mavunde

  ❖ Baada ya Miaka 100 GST Yajielekeza kwenye Ujenzi wa  Maabara za Kisasa ❖ Kuhudumia mikoa ya kimadini ya Geita, Mbogwe, Kagera, Mwanza, Kahama na Shinyanga  ❖Maabara nyingine kujengwa Chunya na Dodoma  📍Geita. Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Peter Mavunde, amesema ujenzi wa maabara ya kisasa ya utafiti na uchambuzi wa madini katika mkoa wa Geita ni hatua kubwa itakayosaidia kuwainua wachimbaji wa madini Kanda ya Ziwa na kuimarisha mchango wa Sekta ya Madini katika uchumi wa taifa. Akizungumza leo Agosti 21, 2025 wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa maabara hiyo, Mhe. Mavunde amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kukubali ombi la Wizara la kujenga maabara tatu za kisasa nchini.  Amesema mbali na maabara hiyo inayojengwa Geita itakayogharimu kiasi cha shilingi bilioni 3.5, maabara nyingine itajengwa Chunya mkoani Mbeya na maabara kubwa zaidi kimataifa itajengwa jijini Dodoma. “Maabara hizi zitakuwa ...

Agizo La Dkt.Biteko La Minada Yote Nchini Kutumia Nishati Safi ya Kupikia Laanza Kutekelezwa

📌 Wachoma nyama na Mama Lishe katika mnada wa Msalato Dodoma waanza kuonja matunda ya Nishati Safi ya Kupikia 📌 Dkt. Biteko asema ni matunda ya Rais, Dkt. Samia ambaye anayefahamu machungu ya kutumia Nishati isiyo safi ya Kupikia 📌 Atoa maagizo kwa Mkurugenzi Jiji la Dodoma kuweka miundombinu itakayohakikisha majiko ya Nishati Safi ya Kupikia ya Wachoma nyama yanakuwa salama 📌 Apongeza REA, Wizara ya Nishati kutekeleza agizo alilolitoa: STAMICO yatakiwa kuweka kituo cha kudumu cha mkaa mbadala Mnada wa Msalato 📌 Kituo kikubwa cha kusambaza umeme na kusimamia gridi ya Taifa kujengwa Dodoma Agizo la Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko alilolitoa kwa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuhakikisha kuwa minada yote nchini inakuwa na miundombinu itakayowawezesha Wachoma nyama, Mama Lishe na Baba Lishe kutumia nishati Safi ya Kupikia limeanza kufanyiwa kazi ikiwa ni utekelezaji wa ajenda ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha wananchi wote wanatumia Nish...

Wabunge kenya Walipiza kisasi,Waangusha Muswada Muhimu wa Serikali

  SIKU moja baada ya Rais wa Kenya William Ruto kudai bunge ni ngome ya ufisadi, wabunge, kwa hasira wameanza kuonyesha kucha zao kwa kuangusha miswada na maamuzi ya kisera ya Serikali Kuu. Jumatano,Kamati ya Usalama kuhusu Bunge ilitupilia mbali Muswada wa sheria mpya ya kuongoza shughuli ya kumkabidhi mamlaka rais mpya baada ya uchaguzi. Mswada huo uliodhaminiwa na Kiongozi wa Wengi bungeni, Kimani Ichung’wah unapendekeza Rais Mteule ateue mwenyekiti mwenza wa Kamati ya Kusimamia Mpito wa Mamlaka ya Urais. Aidha, mswada huo unapendekeza kuwa Rais mteule ateue Katibu wa kamati hiyo ya wanachama 25, tisa kati yao wakiwa wawakilishi wake. Mswada huo pia unapanua sheria hiyo ya kuongoza shughuli ya kumpatia rais mpya afisi ili kujumuisha maafisa wengine kama Mawaziri, Mwanasheria Mkuu na Makatibu wa Wizara. Kulingana na sheria ya sasa, Rais aliye mamlakani ndiye huonekana kuwa na usemi mkubwa katika kamati hiyo inayoongozwa na Mkuu wa Utumishi wa Umma. Lakini Kamati ya Bunge kuhusu U...

Türkiye – Tanzania Steel Trade Mission 2025 set to strengthen bilateral trade relations

By Prosper Makene The Türkiye – Tanzania Steel Trade Mission 2025 will be held on 4th September 2025 at the Hyatt Regency Hotel, Dar es Salaam, bringing together leading Turkish steel exporters and Tanzanian businesses for a day of strategic trade engagement and pre-arranged B2B meetings. Organized by the Turkish Steel Exporters’ Association in partnership with the Turkish Embassy in Dar es Salaam, the mission is designed to strengthen bilateral trade relations and explore new business opportunities in the steel, construction, and infrastructure sectors. The event will connect Turkish manufacturers with Tanzanian importers, construction firms, hardware suppliers, industrial players, and procurement professionals—facilitating direct discussions on sourcing, distribution, and long-term partnership development. “Participation in the B2B meetings is free, but online registration is required through the link below: https://forms.gle/JnxxB96W8ywBZEsn7. interested businesses are encouraged to...

Umoja na Mshikamano Vyatawala Hotuba za Viongozi Mkutano wa Sadc

Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) umehitimishwa jijini Antananarivo Agosti 17, 2025, huku viongozi hao wakihimizana, umoja, mshikamano na ushirikiano  kama njia ya msingi ya kujikwamua kiuchumi na kukabiliana na changamoto zinazoibuka kila siku ulimwenguni. Katika mkutano huo, Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan aliwakilishwa na Makamu wa Rais, Dkt. Philip Isdor Mpango, na kama ilivyo ada, mwenyeji wa mkutano huo, Madagascar alikabidhiwa uenyekiti wa jumuiya hiyo kutoka Zimbabwe. Mkutano huo ulihudhuriwa na wakuu wa nchi 9 ambapo Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, mwenyekiti aliyopekea kijiti, Katibu Mtendaji wa SADC na wakuu wa nchi wanne wa Botswana, Namibia, Msumbiji na Mauritius kutokana na kushiriki kwao kwa mara ya kwanza kama wakuu wa nchi walipata fursa ya kuhutubia mkutano huo. Hotuba za viongozi hao ziligusia maeneo makubwa manne ambayo ni amani na usalama, ujenzi wa miundombinu, uchumi, demokrasia na mtangamano. Mwenyekiti aliyemaliza mu...