Skip to main content

Posts

Showing posts from September 13, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Wana Ruangwa Kumpa Zawadi Kubwa Rais Dkt. Samia 2024-2025

  WANANCHI wa jimbo la Ruangwa mkoani Lindi, wamesema zawadi pekee ya kumlipa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo katika jimbo hilo, ni kushinda uchaguzi wa Serikali za mitaa. Wamesema wamejipanga kushinda vitongoji na vijiji vyote tisini  vya jimbo hilo katika uchaguzi huo wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka huu . Akizungumza baada ya mapokezi makubwa na ya aina yake katika viwanja vya madini jimbo la   Ruangwa katika siku ya Hamasa maarufu kama HAMASA DAY, ambayo imeshirikisha vijana wa CCM wa kata 22 za jimbo hilo,mbunge wa Ruangwa ambaye pia ni waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Kassim Majaliwa,amesema Rais Samia,ametoa fedha nyingi za utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika jimbo hilo. Amesema hivi sasa kata 22 zina shule za Sekondori na huku baadhi zikiwa na shule zaidi ya moja huku Rais Samia akitoa fedha zaidi za...

Serikali imedhamiria kulibadili Jeshi la Polisi nchini.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni amezindua Bodi ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi huku akiipa majukumu bodi hiyo kulisimamia shirika ambalo linaenda kutekeleza miradi mbalimbali ambayo inaenda kuleta mabadiliko makubwa kwa Jeshi la Polisi katika kukabiliana na matukio ya kihalifu kwa kutumia dhana za teknolojia ya kisasa ili kuweza kustawisha amani na utulivu kwa wananchi katika mikoa mbalimbali nchini. Ameyasema hayo leo wakati wa Uzinduzi wa Bodi hiyo yenye jumla ya wajumbe tisa ikiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo,Omar Issa ambae alikua Mjumbe wa Tume ya Haki Jinai iliyoteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan kufuatilia Mfumo na Utendaji wa Taasisi za Haki Jinai likiwemo Jeshi la Polisi,Magereza,Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU),Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Mamlaka ya Kudhibiti na Kuzuia Dawa za Kulevya. ‘Serikali imedhamiria kufanya mabadiliko makubwa katika Jeshi la Polisi sasa huwezi kuwa...

Waziri Bashe na Mbunge Mpina Wakubaliana Kuweka Kando Tofauti zao

Serikali imeahidi kurejesha kitalu cha kuzalisha mbegu za pamba kwenye Jimbo la Kisesa Wilayani Meatu Mkoani Simiyu pamoja na kuwapatia wakulima wa Jimbo hilo Ruzuku ya pembejeo ikiwemo dawa ya viududu wanaoshambulia pamba pamoja na mbegu bora za pamba.  Waziri wa Kilimo Hussein Bashe  amebainisha hayo wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha mwandoya wilayani Meatu.  Bashe pia amekabidhi Matrekta 40 kwenye Jimbo la Kisesa na kuwataka Maafisa Ugani kuacha Kukaa mijini na Badala yake waende vijijini kuwasaidia wakulima utaalam utakaowawezesha kufikia malengo ya serikali ya kuzalisha Mazao ya chakula na biashara kwa tija.  Akiwa Jimboni Kisesa,Waziri Bashe amekutana na Mbunge wa Jimbo hilo Luhaga Mpina ambaye amesema yuko tayari kuweka kando tofauti zake na Bashe na kuungana naye katika masuala ya maendeleo pamoja na shughuli za serikali.  Mpina ametumia fursa hiyo kueleza kuwa yeye na Bashe wanazo tofauti zao  iliyowafikisha hadi Mahakamani Lak...