Skip to main content

Posts

Showing posts from May 30, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Timu ya Ras Mara Biashara United Veteran Zatoshana Nguvu Uwanja wa Karume

Na Shomari Binda-Musoma  TIMU ya Biashara United Veteran na RAS Mara zimetoshana nguvu baada ya kufungana bao 1-1 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika uwanja wa Karume. Kocha mpya wa Biashara Veteran aliyechukua mikoba ya kuinoa timu hiyo Frumence Tungaraza amesema huo ni mchezo wake wa kwanza wa kiushindani tangu kuanza kuifunddisha timu hiyo na matokeo hayo sio mabaya kwake. Amesema anaendelea kuona makosa ya timu hiyo anapopata michezo mbalimbali na lengo lake ni kuondoa jinamizi la kufungwa kwa timu hiyo. Frumence ambaye aliwahi kuzichezea timu mbalimbali kwenye ligi ikiwemo Polisi Mara na Biashara United amesema timu anayoifundisha ina wachezaji wazuri ambao wanahitaji maelekezo kidogo ili wafanye vizuri. Amesema ataendelea kuiandaa timu hiyo ili yatakapokuja mashindano mbalimbali waweze kufanya vizuri. " Nashukuru mchezo umemalizika salama na naendelea kuiandaa timu yangu kwaajili ya mashindano mbalimbali. " Yapo makosa ambayo nimeyaona na ntaenda kuyafanyia kazi kweny...

Biashara ya Kaboni Kuwekezwa Tanzania

Na mwandishi wetu Jovina Massano Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Japan zimetia saini Hati ya Makubaliano ya Biashara ya Kaboni Kuwekezwa Tanzania. katika mpango wa pamoja wa uwekezaji katika Biashara ya Kaboni. Mpango huo utakaowezesha kampuni za nchi hizi mbili kuwekeza katika Biashara ya Kaboni nchini Tanzania. Utiaji saini wa makubaliano hayo umefanyika Mei 28, 2025   Tokyo, Japan kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni na Serikali ya Japan ikiongozwa na Waziri wa Mazingira, Mhe. Asao Keiichiro (Kei). Waziri Masauni amesema Makubaliano ya Mashirikiano yaliyosainiwa yamekusudiwa kuimarisha uhusiano kati ya Japan na Tanzania kwa maendeleo endelevu ikiwemo hatua za kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi. "Ushirikiano huu utaongeza fursa ya kupanua soko la Biashara ya Kaboni kutoka kwa wawekezaji wa Japan watakaowekeza kati...

Balozi Matinyi Akutana Na Watanzania Wanaoishi Nchini Uswidi

Balozi wa Tanzania katika Ufalme wa Uswidi, Mhe. Mobhare Matinyi, tarehe 29 Mei, 2025, alifanya kikao na Watanzania wanaoishi nchini humo katika viwanja vya ofisi za ubalozi jijini Stockhom. Katika kikao hicho kilicholenga kufahamiana na kujadiliana kuhusu masuala ya Diaspora, Mhe. Balozi Matinyi alielezea tafsiri ya neno "diaspora" kwa mujibu wa Sera ya Mambo ya Nje ya mwaka 2001, toleo la mwaka 2024, iliyozinduliwa tarehe 19 Mei, 2025, jijini Dar es Salaam na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan. Mheshimiwa Balozi alieleza kuwa sera hii inawatambua Diaspora kuwa ni raia wa Tanzania wanaoishi nje (Citizen Diaspora) na raia wa nchi zingine wenye asili ya Tanzania (Non-Citizen Diaspora).  Mhe. Balozi Matinyi aliwaeleza Watanzania hao waliotoka miji mbalimbali ya Uswidi, kwamba sera hiyo imetambua ushiriki wa Diaspora katika maendeleo ya nchi yetu huku akirejea wito wa Mhe. Rais Dkt. Samia wa kuwataka Diaspora wawekeze nchini ili kuchangia maen...

Wajumbe Wa Mkutano Mkuu Ccm Wakiburudika Kuelekea Kuzindua Ilani

Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakiburudika burudani ya mziki kutoka Kikundi cha Sanaa cha Tanzania One Theatre (TOT), kikiongozwa na Malkia wa Mipasho na Mziki wa Taarab, Bi. Khadija Omar Abdallah Kopa, leo Ijumaa tarehe 30 Mei 2025, jijini Dodoma.  Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Taifa huo ukiongozwa na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ulianza jana Alhamis, tarehe 29 Mei 2025, na leo unaendelea katika siku yake ya pili, katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma, ambapo mojawapo ya agenda itakuwa ni kuzindua Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2025 - 2030.