Skip to main content

Posts

Showing posts from February 21, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Kampuni ya Songoro Marine yakabidhi Kivukoni nchini Uganda

Kampuni ya kizawa ya Songoro Marine iliyojikita katika ujenzi wa meli ndani na nje ya Tanzania imekamilisha ujenzi wa kivuko kikubwa kitakachokuwa na uwezo wa kubeba abiria 310. Kampuni hiyo imekamilisha ujenzi wa kivuko hicho kitakachokuwa kinafanya safari zake kati ya Bukungu - Kagwara - Kaberamaido nchini Uganda. Songoro marine ambayo imejikita na ujenzi wa vivuko, imeendelea kuaminiwa na serikali ya uganda katika ujenzi wa vivuko kadhaa nchini humo. Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo, Meja Songoro akizungumza wakati wa kukabidhi kivuko hicho, amesema ujenzi wa kivuko hicho ulianza februari 2020 na kukabidhiwa Februari 20 mwaka huu.  Kampuni ya Songoro Marine, ilisaini  mkataba wa ujenzi wa vivuko viwili pamoja na mashine ya kuondoa uchafu ziwani (dredger) kwa fedha za Uganda shilingi, 41,974,226,085. Baada ya siku ya jana kampuni hiyo kukabidhi kivuko hicho kwa serikali ya Uganda, inaendelea na kivuko kingine kimoja ambacho kitakabidhiwa muda wowote. Mwisho

Dkt. Mwigulu: Someni Kwa Bidii Kumuenzi Rais Samia, Wazazi Wenu*

_Asema Dkt. Samia amewapa elimu kuwa urithi watoto wa Kitanzania_ WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amewataka wanafunzi wanaosoma shule ya sekondari ya wasichana ya mkoa wa Kilimanjaro wasome kwa bidii ili kuwaenzi wazazi wao pamoja na jitihada za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. “Wanangu someni kwa bidii, kitu pekee cha kuwalipa wazazi wenu na furaha tutakayompa Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kufaulu vizuri sana,” amesisitiza wakati akiongea na wanafunzi zaidi ya 600 wa shule hiyo pamoja na wananchi waliofika kushuhudia uwekaji wa jiwe la msingi uliofanyika leo (Jumamosi, Februari 21, 2026) kwenye shule hiyo iliyopo katika kijiji cha Mawasiliano, Kata ya Gararagua, Wilayani Siha. “Nilipofika hapa Kilimanjaro Girls’ nilifurahi kusikia kwamba ni shule ya masomo ya sayansi tena ina tahsusi ya PCM. Hii imenifanya nikumbuke pure mathematics inayoanza na quadratics, inakuja functions, inakuja coordinate geometry ... na tunamaliza na calculus, differentifation and integration,” alitaja baadhi ya t...

Tume ya uchunguzi yaongezewa muda hadi April 3, 2026

*DAR ES SALAAM:*  MAMLAKA ya Uteuzi imeongeza muda wa siku arobaini na mbili (42) kuanzia tarehe 20 Februari, 2026 Tume ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 ili Tume iweze kukamilisha uchunguzi wa matukio ya uvunjifu wa amani ya wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa tarehe 29 Oktoba, 2025 na kuitaka ikamilishe kazi na kuwasilisha Taarifa yake kabla au ifikapo tarehe 3 Aprili, 2026.  Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa katika gazeti la serikali Tume imeongezewa muda huo ili kutoa fursa na muda wa kutosha kwa kila mwenye taarifa, ushahidi au maoni, aliyepo nchini au nje ya nchi, kuwasiliana na Tume ili kuhakikisha kuwa hakuna mtu yeyote, au taasisi yoyote, itakayokosa nafasi ya kusikilizwa.  Sababu nyingine za kuongeza muda ni pamoja na zifuatazo Wingi na mchanganyiko wa taarifa zilizokusanywa, na zinazoendelea kukusanywa, na Tume ambazo zinahitaji muda zaidi wa kufanyiwa uchambuzi wa kina, Tume kulazimika kutumia Wataa...

Dkt. Mwigulu Awapongeza Viongozi Wilaya ya Hai Kusimamia Vizuri Sekondari ya Mbatakero

WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amewapongeza viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai kwa kusimamia vizuri mradi wa ujenzi wa shule mpya ya sekondari ya Mbatakero na kubakiza ziada ya sh. milioni 4.33. Ametoa pongezi hizo leo (Jumamosi, Februari 21, 2026) wakati akizungumza na wakazi wa Kata ya Weruweru mara baada ya kuzindua shule mpya ya sekondari ya Mbatakero, wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro ambayo imejengwa kupitia mradi wa SEQUIP. Viongozi waliopongezwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Dionis Myinga, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Hai, Edmund Rutaraka, Mhandisi wa Wilaya, Arnold Matandiko na Afisa Elimu wa Wilaya sehemu ya sekondari, Margaret Muro. Dkt. Mwigulu amesema ujenzi wa shule hiyo unatokana na dhamira ya dhati aliyonayo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuondoa kero zinazowasumbua wananchi. “Tunaposema Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa kuna watu huwa hawatuelewi. Lakini hawa waliokuwa wakitembea km. 18 kwenda na kurudi shuleni, wao na ...

Waziri Mavunde azindua Kiwanda cha Kuzalisha mkaa mbadala mkoani Tabora

*Ni utekelezaji wa maelekezo ya Mhe. Rais Samia juu ya nishati mbadala kukaushia Tumbaku* *Tumbaku sasa kukaushwa kwa mkaa badala ya kuni* *Waziri Mavunde awataka STAMICO kuongeza uzalishaji zaidi wa makaa ya mawe Kiwira* *Kamati ya Bunge yapongeza ushiriki wa Stamico kwenye Nishati Safi* 📍 Tabora Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, amezindua Kiwanda cha Rafiki Briquettes mkoani Tabora na kuielekeza Bodi ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kuongeza uzalishaji wa makaa ya mawe katika Mgodi wake wa Kiwira. Amesema hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kupanua matumizi ya nishati safi ya kupikia na kupunguza utegemezi wa kuni na mkaa. Akizungumza Februari 21, 2026 wakati wa uzinduzi wa kiwanda hicho chenye uwezo wa kuzalisha tani 20 kwa siku, Waziri Mavunde, amesema kitasaidia kupunguza ukataji wa miti na kusaidia ukaushaji tumbaku mkoani Tabora. Ameongeza kuwa, uzinduzi huo ni utekelezaji wa maelekezo ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,...

SONGORO MARINE UBORA WA KIMATAIFA UJENZI WA MELI

Kampuni ya kizawa ya Songoro Marine iliyojikita katika ujenzi wa meli ndani na nje ya Tanzania inatajwa ni kampuni inayojenga meli kwa viwango vya kimataifa. Kampuni hiyo, imekuwa ikipewa zabuni na serikali za ujenzi wa vivuko, kutokana na kuonyesha uzalendo katika kutekeleza miradi kwa viwango vya kimataifa. Kwa miaka zaidi ya 30 Tangu kuanza kwa kampuni hii ya kizalendo imeonyesha dira kwa kampuni za kizawa baada ya kuaminiwa na serikali katika ujenzi wa vivuko. Kampuni hii iliyoanza kazi mwaka 1993 kwa sasa imeendeleza mizizi ya ujenzi wa meli za kisasa zinazotumiwa ziwani na baharini kwa kufungua matawi nje ya mipaka ya Tanzania. Inaelezwa kuanza kufungua matawi nje ya mipaka ya Tanzania ni hatua iliyotokana na kazi iliyotukuka kwa kujenga meli na vivuko vya umma na binafsi kwa viwango vya kimataifa. Serikali ya Tanzania mara kwa mara imekuwa ikitangaza zabuni za ujenzi wa meli, ambapo kampuni hii ya kizalendo imekuwa ikiibuka kidedea. Songoro Marine yenye makao makuu yake Ilemela ...