Skip to main content

Posts

Showing posts from June 29, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

OWM YASISITIZA UJUMUISHWAJI WA WATU WENYE ULEMAVU KATIKA MIPANGO YA TAIFA

 Na Mwandishi Wetu – Dar es Salaam SERIKALI imeendelea kusisitiza dhamira yake ya kuhakikisha Watu Wenye Ulemavu wanapata nafasi sawa katika nyanja zote za maendeleo, ikiwa ni pamoja na kijamii, kiuchumi na kisiasa, kupitia sera, sheria na mipango jumuishi inayotekelezwa nchini. Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) Dkt. Jim Yonazi wakati wa ufunguzi wa kikao kazi kilichowakutanisha viongozi wa vyama vya Watu Wenye Ulemavu na mashirika yasiyo ya kiserikali kujadili utekelezaji wa sera, sheria na miongozo ya ujumuishaji nchini. Amesema hatua kubwa zimeendelea kuchukuliwa katika kuhakikisha hakuna mwananchi anayeachwa nyuma, ambapo Sera ya Taifa ya Watu Wenye Ulemavu ya mwaka 2004 pamoja na Sheria Na. 9 ya mwaka 2010 zimekuwa msingi muhimu wa utekelezaji wa haki na usawa kwa kundi hilo. “Serikali itaendelea kuhakikisha kuwa kila sera, mpango na huduma inayotekelezwa nchini inazingatia ujumuishaji wa Watu Wenye Ulemavu tangu ha...

INADES-FORMATION TANZANIA YASHIRIKIANA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS KUANDAA MPANGO WA MAZINGIRA WILAYA YA BAHI

  By Prosper Makene  Katika juhudi za kuhakikisha Tanzania inafikia azma ya kuwa nchi ya kijani ifikapo mwaka 2050, Shirika la INADES-Formation Tanzania kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais – Idara ya Mazingira limeandaa kikao kazi cha kuandaa Mpango wa Usimamizi wa Mazingira wa Wilaya ya Bahi, kwa kushirikisha wataalamu kutoka Wilaya za Chemba na Kondoa. Akifungua kikao hicho Leo katika ofisi ya Makamu wa Rais, Mtumba mjini Dodoma, Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais – Idara ya Mazingira, Dk. Paul Deogratius, alisema ushiriki wa Wilaya za Chemba na Kondoa utasaidia kubadilishana uzoefu katika mchakato wa kuandaa mpango huo kwa Wilaya ya Bahi. Alieleza kuwa mipango ya usimamizi wa mazingira katika ngazi ya wilaya ni takwa la kisheria na ni nyenzo muhimu katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za mazingira zinazozikabili halmashauri nchini. "Kitaifa, zimetambuliwa zaidi ya changamoto 13 za mazingira, huku kila wilaya ikiwa na changamoto zake ...

VICE PRESIDENT'S OFFICE, INADES-FORMATION COLLABORATE ON ENVIRONMENTAL PLAN FOR BAHI DISTRICT

 By Prosper Makene  Dodoma – In efforts to ensure Tanzania achieves its goal of becoming a green country by 2050, INADES-Formation Tanzania, in collaboration with the Vice President's Office – Department of Environment, has organized a working session to develop the Bahi District Environmental Management Plan, involving experts from Chemba and Kondoa districts. Opening the session today at the Vice President's Office in Mtumba, Dodoma, the Acting Director of Environment from the Vice President's Office – Department of Environment, Dr. Paul Deogratius, said the participation of Chemba and Kondoa districts will help facilitate the exchange of experience in the process of developing the plan for Bahi District. He explained that environmental management plans at the district level are a legal requirement and are a crucial tool in addressing various environmental challenges facing local councils across the country. "Nationally, more than 13 environmental challenges have bee...

CRDB YAWEKA AFYA YA WAFANYAKAZI KIPAUMBELE ,YAAMINI USTAWI NDIYO MSINGI WA MAFANIKIO

 CRDB Bank imeendelea kuthibitisha kuwa rasilimali muhimu zaidi katika mafanikio ya taasisi ni watu wake, kwa kuendesha programu ya Wellness Day inayolenga kuimarisha afya ya mwili, akili na ustawi wa wafanyakazi, hatua inayotajwa kuwa sehemu ya mkakati wa kujenga nguvu kazi yenye tija, ubunifu na ufanisi. Akizungumza leo jijini Dodoma wakati wa programu hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa CRDB, Edward Mpina, amesema benki hiyo inaamini kuwa mafanikio ya biashara hayawezi kutenganishwa na afya ya wafanyakazi wake, ndiyo maana imeendelea kuwekeza katika mipango inayowalinda na kuwajengea mazingira bora ya kufanya kazi. Mpina amesema dhana ya wellness ni pana zaidi kuliko kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza, kwani inajumuisha afya ya akili, ustawi wa kihisia, uwezo wa kukabiliana na changamoto za kazi na maisha pamoja na kujenga usawa kati ya kazi na familia. Ameeleza kuwa katika mazingira ya kisasa ya kazi, wafanyakazi hukabiliwa na shinikizo la kufikia malengo ya biashara, kutimiza via...

WAZIRI NDEJEMBI AWASILI TANGA KWA ZIARA YA KIKAZI

 Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius J. Ndejembi (Mb.), amewasili mkoani Tanga kwa ziara ya kikazi na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Balozi Dkt. Batilda Burian, leo tarehe 29 Juni, 2026. Akiwa mkoani Tanga, Waziri Ndejembi atatembelea na kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya nishati, ikiwemo Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) katika eneo la Chongoleani, Tanga, unaolenga kusafirisha mafuta ghafi yaliyogunduliwa nchini Uganda kwenda kwenye masoko ya kimataifa. Katika ziara hiyo, Waziri Ndejembi ameambatana na wataalamu kutoka Wizara ya Nishati pamoja na taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo.