Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini mkoani Mara, Mwita Waitara, ameibua hisia kali Bungeni baada ya kuhoji namna ambavyo baadhi ya wananchi wanaendelea kuteseka kwa kukosa huduma muhimu huku fedha za umma zikidaiwa kutafunwa na wachache wasiowajibika. Akichangia Bajeti ya Wizara ya Fedha leo Juni 2, 2026, Jijini Dodoma, Waitara amesema ni jambo linaloumiza kuona wananchi wakihangaika kutafuta fedha za matibabu na dawa hospitalini, wakati ripoti za ukaguzi zinaendelea kuonyesha uwepo wa matumizi mabaya ya fedha za umma katika baadhi ya taasisi za Serikali. Kwa sauti ya msisitizo, Waitara ameeleza kuwa fedha zinazotengwa na Bunge zinapaswa kuwafikia wananchi na kuleta maendeleo yaliyokusudiwa, badala ya kupotea mikononi mwa watu wachache wanaokwamisha juhudi za Serikali na matarajio ya wananchi. “Leo hii kuna mwananchi anaondoka hospitalini bila dawa kwa sababu hakuna fedha za kutosha. Wakati huo huo, ripoti za ukaguzi zinaonyesha kuna watu wamechezea fedha za umma. Hili halipaswi ku...
Marato tv - Sauti ya Jamii