Skip to main content

Posts

Showing posts from October 11, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt.Nchimbi Atua Kigoma Kusaka Kura za Ushindi wa Kishindo za Dkt.Samia

PICHA mbalimbali za Mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Emmanuel Johnn Nchimbi akiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kibondo leo Oktoba 12, 2025 kuendelea na mikutano yake ya hadhara ya Kampeni, kusaka kura za ushindi wa kishindo za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan,Wabunge na Madiwani. Dkt.Nchimbi ataanza mkutano wake mdogo wa kwanza wa kampeni mkoani humo katika wilaya ya Kakonko na baadae wilaya ya Kibondo, ambako  atafanya mkutano wake mkubwa wa hadhara wa kampeni wa kunadi sera na Ilani ya CCM ya mwaka 2025-2030. Balozi Nchimbi anafikia mkoa wa 22 sasa tangu kuzinduliwa kwa kampeni hizo Agosti 28,2025 jijini Dar es Salaam,akiendelea kusaka kura za ushindi wa kishindo za mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi,Dkt.Samia Suluhu Hassan,Wabunge na Madiwani.

Wenye ulemavu wampa tuzo Rais Dkt.Samia

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Oktoba 11, 2025 amepokea kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan tuzo ya kutambua mchango wake katika kusimamia ustawi wa jamii ya watu wenye ulemavu nchini, kwenye hafla iliyofanyika Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu, Oysterbay Jijini Dar es Salaam. Tuzo hiyo imetolewa na taasisi ya Foundation for Disabilities Hope (FDM). Akizungumza kwenye tukio hilo Mheshimiwa Majaliwa amewaeleza kuwa Rais Dkt. Samia yupo tayari kuendelea kufanya makubwa kwa jamii hiyo na ataendelea kuwahudumia. *Taarifa kamili inakuja*

Msama - Watanzania Milioni 25 watampigia kura Dkt.Samia

wa Msama Promotions Ndugu Alex Msama amesema kulingana na utafiti ambao nchi nzima, Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi Dkt. Samia Suluhu Hassan ndiye anayependa zaidi kuliko Wagombea wa vyama vingine zaidi ya 16 vilivyosimamisha Wagombea Urais katika Kampeni za Mwaka huu. Msama amaesema Watanzania zaidi ya Milioni 60 wanampenda Dkt. Samia na wapiga kura zaidi ya Milioni 25 wameahidi kumchagua katika Uchaguzi wa tarehe 29, ila Watanzania Milioni 1 tu ndio wanaojifanga hawampendi mitandaoni kwa sababu ya kusikiliza propaganda za uongo kutoka kwa wasioipenda mazuri nchi yetu.

Serikali Itaendeleakuhakikisha Tunakuwa na Nguvu Kazi ya Kisasa na Yenye Ujuzi-Majaliwa

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kuhakikisha Tanzania inakuwa na nguvukazi yenye ujuzi wa kisasa na inayoweza kushindana katika soko la ajira la kikanda na kimataifa. Amesema lengo ni kuhakikisha nguvu kazi hiyo inakuwa na mchango katika kuchochea ukuaji wa uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla. Amesema hayo leo Jumamosi (Oktoba 11, 2025) wakati alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Ufunguzi wa Kongamano la Kumbukizi ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere lilizofanyika katika ukumbi wa Maktaba Mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. “Mafanikio ya taifa letu katika miaka ijayo yatategemea kwa kiasi kikubwa ubora wa watu wake. Msingi wa maendeleo ya taifa letu ni watu wenye ujuzi, ubunifu, na maadili. Tuweke mbele elimu bora, ujuzi, ubunifu, na uzalendo kama silaha za kujenga taifa lenye ustawi, amani, na maendeleo jumuishi. Amesema kuwa katika kuhakikisha Tanzania inaandaa nguvu kazi imara imetekeleza mipango mbalimbali ikiwemo kuanzisha Program...

Dkt.Samia awaomba kura wananchi wa Maswa

Mgombea nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan,. na Wananchi, Wanachama na Wapenzi wa CCM wa Maswa katika muendelezo wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu kwa Chama hicho Mkoani Simiyu tarehe 11 Octoba, 2025.