Skip to main content

Posts

Showing posts from August 21, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

TANZANIA BADO TUNA FURSA NYINGI ZA UTALII - MAJALIWA

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema bado kuna fursa nyingi hapa nchini ambazo zikitumika vizuri zinaweza kuongeza idadi ya watalii wa ndani na nje. Ametoa kauli hiyo jana usiku (Jumatano, Agosti 21, 2024) wakati akizungumza na mamia ya wadau na washiriki waliohudhuria tukio la USIKU WA UTALII ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za Tamasha la Kizimkazi 2024 lililofanyika kwenye uwanja wa Maendeleo ya Sheria wa Dimbani, Kizimkazi, Zanzibar. Amesema kwa kutumia fursa za utamaduni, wanyama na utalii wa fukwe Tanzania inaweza kuongeza idadi ya watalii kwa kiwango kikubwa ikilinganishwa na hali ilivyo sasa. “Hapa Kizimkazi tuna samaki aina ya pomboo ambaye ana sifa zote za kuingia kwenye utalii. Tuendelee kuimarisha utalii wa fukwe na tuwatumie pomboo kuchochea utalii kama ambavyo wenzetu wa Cuba wanawatumia.” “Cuba ni nchi ndogo lakini inapokea watalii wengi sana. Wanao walimu wa kuwafundisha samaki hawa kucheza na binadamu, wanafundishwa kucheza muziki. Na sisi Tanznaia tunao pomboo wa k...

WAZIRI MKUU ASISITIZA UIMAIRISHAJI WA TAMADUNI NCHINI

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa jana Agosti 21, 2024 alikuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Kizimkazi lililolenga kukuza Utalii Zanzibar, ambalo lilifanyika katika uwanja wa Shekha Dimbani, Zanzibar. Akizungumza katika Tamasha hilo Mheshimiwa Majaliwa aliwasihi Watanzania waendelee kushirikiana, kuimarisha utamaduni na kujenga taifa lenye maendeleo na umoja. Aidha, aliwapongeza Dkt Samia Suluhu Hassan na Rais Dkt Hussein Mwinyi kwa juhudi kubwa za kukuza utalii nchini.

TRA YATANGAZA FURSA KWA WALIPA KODI NCHINI

 

POLISI MKOA WA MWANZA WATANGAZA OPARESHENI YA AINA YAKE ZIWA VICTORIA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limeendelea na jitihada za kuimarisha mifumo ya kiusalama na kutokomeza vitendo vya kihalifu katika fukwe, mialo na visiwa ndani ya Ziwa Viktoria kwa kuishirikisha Jamii. Uzinduzi wa operesheni sambamba na utoaji wa elimu kwa wananchi umefanyika Agosti 20, 2024 katika mwalo wa Igombe, Kata ya Bugogwa Wilaya ya Ilemala mkoani humo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Wilbrod Mutafungwa. Akizungumza na uongozi wa Serikali za Mitaa na wananchi wa kata hiyo baada ya kuwapatia elimu ya usalama majini na ukatili wa kijinsia kutoka kwa Mkuu wa Kikosi cha Wanamaji mkoa wa Mwanza Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Wenceslaus Muchunguzi,   Kamanda Mutafungwa amezindua awamu nyingine ya kusikiliza kero za kiusalama kutoka kwa wananchi. "Katika eneo lenu hili, siku ya leo nimekuja kuzindua awamu nyingine ya kusikiliza kero, changamoto, malalamiko na kupata ushauri kutoka kwa wananchi" amesema Kamanda Mutafungwa. Aidha, Kamanda M...

SERIKALI IMEOMBWA KIASI SHILINGI BILLIONI 1.9 KUKAMILISHA BWENI MISUNGWI

  Chuo cha maendeleo ya Jamii ufundi(CDTI)  Misungwi mkoani Mwanza kinahitaji zaidi ya shilingi billioni 1.9 kwa ajili  ya kukamilisha ujenzi wa bweni la wasichana. Kukamilika kwa ujenzi wa bweni hilo kutakifanya chuo hicho kuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 352 kwa wakati mmoja. Makamu Mkuu wa chuo cha CDTI Misungwi Taaluma DONGO NZORI amebainisha hayo wakati wa ziara ya Naibu katibu mkuu wa wizara ya maendeleo ya Jamii,Jinsia,wanawake na makundi maalum FELISTA MDEMU,ambapo pamoja na mambo mengine amepata nafasi ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo. Mradi wa ujenzi wa bweni hilo unatarajia kugharimu shilingi billioni 2.2  hadi kukamilika kwake ambapo litakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi wa kike 352. Akizungumza wakati wa kukagua mradi wa ujenzi wa bweni hilo,Naibu Katibu Mkuu MDEMU amesisitiza dhamira ya serikali ya kukamilisha ujenzi huo. Aidha ameiasa Jamii kuchangamkia fursa za masomo zinazopatikana kwenye chuo cha maendeleo ya Jamii ufundi Misungwi. Katika kit...