Skip to main content

Posts

Showing posts from June 26, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mkuu: Tanzania Siyo Mahali Salama Kwa Biashara ya Dawa za Kulevya

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa onyo kwa wasambazaji na wauzaji wa dawa za kulevya kwamba Tanzania siyo mahali pa kufanyia biashara zao. Waziri Mkuu ambaye amefunga maadhimisho ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya  Duniani kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema: “Tanzania siyo mahali salama kwa wauzaji, wasafirishaji, walimaji na hata pia watumiaji wa dawa za kulevya. Tanzania tumeiva na sasa tunaenda kukomesha biashara hii.” Ametoa kauli hiyo leo jioni (Alhamisi, Juni 26, 2025) wakati akizungumza na maelfu ya wakazi wa Dodoma wakiwemo wananchi, wadau, viongozi wa Serikali, wa dini na siasa ambao walihudhuria kilele cha maadhimisho hayo kwenye ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma.  “Makamishna na wakuu wa vyombo vya ulinzi fanyeni kazi, imarisheni ulinzi iwe ni kwenye SGR, vituo vya mabasi, bandari na viwanja vya ndege ili tuweze kuokoa vijana wetu. Dawa hizi zina madhara makubwa kwani zinapoteza uwezo wa mwili na uwezo wa kiakili wa kufikiri ma...

Watanzania Puuzeni Video Inayosambazwa,Sina Nyumba Upanga-Msama

 Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama amewataka watanzania kupuuza habari zinazogaa kuwa amefukuzwa kwenye nyumba yake ya Upanga Dar es Salaam, "Video zinazosambaa zinatumika na watu wasio na nia njema na mimi na wana lengo la kunichafua hasa kipindi hichi cha vita za ubunge” Alex Msama

Watanzania Puuzeni Video inayosambazwa Kisiasa Dhidi Yangu-Msama

Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama amewataka watanzania kupuuza habari zinazogaa kuwa amefukuzwa kwenye Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama amewataka watanzania kupuuza habari zinazogaa kuwa amefukuzwa kwenye nyumba yake ya Upanga Dar es Salaam, "Video zinazosambaa zinatumika na watu wasio na nia njema na mimi na wana lengo la kunichafua hasa kipindi hichi cha vita za ubunge” Alex Msama watanzania kupuuza habari zinazogaa kuwa amefukuzwa kwenye nyumba yake ya Upanga Dar es Salaam, "Video zinazosambaa zinatumika na watu wasio na nia njema na mimi na wana lengo la kunichafua hasa kipindi hichi cha vita za ubunge” Alex Msama yake ya Upanga Dar es Salaam, "Video zinazosambaa zinatumika na watu wasio na nia njema na mimi na wana lengo la kunichafua hasa kipindi hichi cha vita za ubunge” Alex Msama

Mbunge Mavunde Azindua Mfumo wa Kidigitali wa Uwasilishwaji Wa Kero za Wananchi Dodoma

▪️Ni mfumo wa uwasilishaji wa taarifa  kwa uharaka kupitia serikali za mitaa ▪️Agawa Simu janja kwa wenyeviti wa mitaa 222 wa Jimbo la Dodoma Mjini ▪️Mfumo unatarajia kuboresha huduma kwa wananchi Dodoma Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde leo amezindua mfumo wa kidigitali wa kupokea taarifa za kero na changamoto za wananchi ambazo zitakuwa zinawasilishwa kupitia uongozi wa Mtaa. Mfumo huo umezinduliwa sambamba na ugawaji wa simu janja(*smart phones)* kwa wenyeviti wa mitaa yote 222 ya Jimbo la Dodoma mjini “Mfumo huu wa uwasilishaji wa taarifa zinazowahusu wananchi utasaidia kuwahudumia wananchi wa Jimbo la Dodoma Mjini kwa ukaribu na uharaka zaidi. Mfumo huu utatumika kusambaza taarifa kwa haraka kwenye ofisini ya Mkuu wa Wilaya, Kwa wasaidizi wangu ofisini kwa Mbunge na kwangu mwenyewe bila hitaji la kupiga simu. Ni mategemeo yangu kwamba simu hizi zitatumika katika kusudio lililolengwa na kusogeza huduma karibu kwa wananchi kwa kuwasilisha changamoto zao kwa wak...

Majaliwa Amwakilisha Rais Dkt. Samia Kwenye Maadhimisho Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Juni 26, 2025 amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Maadhimisho ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani inayofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Jijini Dodoma. Kaulimbiu ya Maadhimisho hayo ni: _“Wekeza kwenye Kinga na Tiba dhidi ya Dawa za Kulevya”._

Waziri Mkuu Aagiza Maafisa Masuuli Wa Serikali Kuzingatia Vipaumbele vya Bajeti ya 2025/2026

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ametoa wito kwa Masuuli katika ngazi zote za umma kuzingatia vipaumbele vilivyoanishwa kwenye Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2025/2026 iliyopitishwa na bunge. Pia, amewaagiza wakamilishe miradi yote ambayo haijakamilishwa sambamba na kutekeleza ahadi za viongozi katika maeneo yao. Amesema hayo leo (Alhamisi, Juni 26, 2025) wakati alipotoa hoja ya kukamilisha shughuli za Bunge la 12, Bungeni jijini Dodoma. Aidha, Mheshimiwa Majaliwa ametoa pongezi kwa Wakuu wa Taasisi, watumishi wote wa umma na sekta binafsi kwa kujituma na kutoa ushirikiano mzuri katika kufanikisha shughuli za Serikali. “Hakika jitihada zenu zimewezesha mafanikio yaliyopatikana katika nyanja mbalimbali ikiwemo kiuchumi na kijamii”. Pia, Waziri Mkuu, amewapongeza wananchi wote kwa juhudi kubwa katika kushiriki kwenye shughuli za uzalishaji mali. “Uchumi wa nchi yetu umeendelea kuwa imara wakati wote. Sina shaka hata kidogo upendo wenu kwa serikali ya awamu ya sita umekuwa msukumo wa k...

Wakimbizi 467 Warejea Nchini Burundi

 Warundi 467 waliokuwa uhamishoni katika kambi za wakimbizi mkoani Kigoma magharibi mwa Tanzania ndio ambao wameripotiwa kurejea nchini mwao kwa hiari ndani ya miezi sita iliyopita. Akizungumza na vyombo vya habari Mkoani Makamba mratibu mipango wa kuwarejesha Warundi kanda ya mashariki mwa Burundi,Antoine Ntirandekura amebainisha kuwa idadi hiyo ni ndogo zaidi ikilinganishwa na ambao walikuwa wanatarajia kuwapokea. Amesema kuwa kwa kiasi kikubwa wamekuwa wakiwapokea wanawake na watoto wanaorejea kutoka katika kambi za Nyarugusu na Nduta,akitoa kwa Warundi waliopo uhamishoni kurejea nchini mwao kutokana na usalama kuimarika. Warundi walikimbia machafuko ya kisiasa yaliyotokea nchini Burundi, mwezi Aprili mwaka 2015 baada ya aliyekuwa Rais wa Burundi kwa wakati huo, Pierre Nkurunziza kutaka kuwania kwa mara ya tatu uongozi wa nchi hiyo kinyume cha katiba ya Burundi.

Rais Dkt.Samia amekuwa kiongozi wa kufanikisha maendeleo nchini - Majaliwa

  _▪️Asema ni Rais Dkt. Samia ni Mwalimu wa subira na kilelezo cha ujasiri._ _▪️Asisitiza utendaji wa Rais Samia umeiheshimisha Tanzania ndani na nje ya nchi._ _▪️Awapongeza watendaji wa Serikali kutekeleza kwa vitendo maono ya Rais Dkt. Samia_ WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa nguzo ya kuimarisha mshikamano na umoja wa kitaifa na utamaduni maendeleo katika sekta mbalimbali za maendeleo. Amesema kuwa katika kipindi cha uongozi wake, Rais Dkt. Samia ameweza kusimama katika miradi ya miradi ya kimkakati na huduma za jamii, demokrasia, kujenga uchumi na kuimarisha diplomasia. Amesema hayo leo (Alhamisi, Juni 26, 2025) wakati alipotoa hoja ya kukamilisha shughuli za Bunge la 12, Bungeni jijini Dodoma. “Sina shaka nyote mtakubaliana nami kuwa hulka yake na ustahimilivu wake umekuwa faraja kwetu sisi wasaidizi wake, watumishi wote wa umma na Watanzania wote kwa ujumla. Amesema Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa Mwalimu wa subira, kil...