Skip to main content

Posts

Showing posts from January 29, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Tanzania Launches TZS 2 Billion Fund to Support Digital Content Creators

The Government of Tanzania has announced a TZS 2 billion (approximately USD 780,000) fund to support digital content creators across the country. Speaking on January 29, 2026, in Dodoma, the Minister for Information, Culture, Arts and Sports, Hon. Paul Makonda, said the initiative aims to strengthen the creative economy by enabling content creators to improve the quality of their work and generate sustainable income through digital platforms. The fund, provided by President of the United Republic of Tanzania, Her Excellency Dr. Samia Suluhu Hassan, will benefit creators in sectors including tourism, sports, media, social development, music, film, and other creative arts. Registration for eligible applicants will run from January 30 to February 15, 2026.

Fursa Mpya Kwa Vijana: Bilioni 2 Kwa Watengenezaji wa Maudhui

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Paul Makonda, amesema Wizara imepatiwa kiasi cha TZS bilioni 2 itakayowawezesha watengenezaji wa maudhui mbalimbali mitandaoni kuimarisha kazi zao na kuwaongezea kipato kupitia majukwaa ya kidijitali. Amesema hayo Januari 29, 2026 jijini Dodoma na kubainisha kuwa, fedha hizo zimetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa lengo la kuyawezesha makundi yote ya watengeneza maudhui ikiwemo katika Sekta ya Utalii, Michezo, Habari, Jamii, Muziki, Filamu na sanaa nyinginezo.  Amebainisha kuwa, zoezi la uandikishaji wa walengwa linaanza rasmi Januari 30 hadi Februari 15, 2026, ambapo watengenezaji wa maudhui wanatakiwa kufika katika ofisi za Halmashauri za Wilaya, Manispaa za Miji na Majiji kupitia vitengo vya habari, ili kuchukua na kujaza fomu za maombi, zikiainisha taarifa binafsi pamoja na shughuli wanazozifanya.

Bil 73.8 kupeleka umeme vitongoji 527 mkoa wa Ta

📌 *Wakandarasi wasisitizwa kujiepusha na vitendo vya rushwa, lugha za kuudhi* 📌*Mradi wa umeme kwenye vitongoji kufungua zaidi fursa za kiuchumi* Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inatekeleza mradi wa shilingi bilioni 73.8 wa kusambaza umeme katika vitongoji 527 mkoani Tanga. Hayo yamebainishwa leo Januari 29, 2026 Jijini Tanga na Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mha. Hassan Saidy wakati wa kuwatambulisha Wakandarasi waliuoshinda zabuni ya kutekeleza mradi huo, Kampuni ya Giza cable industries pamoja na Energy service Limited katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo. “Leo tuko hapa kwako kutambulisha Wakandarasi ambao watakuja kutekeleza mradi mkubwa wa kupeleka umeme katika vitongoji 527 katika Mkoa wa Tanga. Wakati tunafanya nao majadiliano kuna maagizo mahususi tuliwapa na tungependa kama kiongozi wetu wa Mkoa uyafahamu. Moja tumewaelekeza wawe na timu ya kufanya kazi karibu kila Wilaya,” amebainisha Mhandisi Saidy. Ameongeza pia, Wakandarasi hao wanatakiwa kujiepusha na vitendo vy...

MAJIKO BANIFU MKOMBOZI WA AFYA NA MAZINGIRA SIMIYU* .

  📌 *Majiko banifu 6,236 kusambazwa na kuuzwa kwa bei ya ruzuku*  📌 *Jiko moja kuuzwa kwa bei ya ruzuku TZS 6,195* . 📍 *SIMIYU*  Wakazi wa mkoa wa Simiyu waaswa kuunga mkono jitihada za Serikali katika utunzaji wa mazingira kwa kutumia nishati safi na salama ya kupikia. Rai hiyo imetolewa  tarehe 29 Januari , 2026 na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anamringi Macha wakati wa upokeaji wa mradi wa usambazaji na uuzaji wa majiko banifu kwa bei ya ruzuku mkoani hapo. "Kinachofanyika leo ni kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za upatikanaji na uhamasishaji wa matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia katika kutunza na kuhifadhi mazingira" alisema Mhe. Macha. Mradi huu unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), ni muendelezo wa  juhudi za serikali  katika kutunza mazingira na kuboresha afya za  wananchi kwa kuhakikisha wananchi wanapata elimu ya kutosha ya umuhimu wa matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia Aliendelea k...

Balozi Dkt Nchimbi Akagua Ukarabati wa Jengo La Ofisi ya Makamu Wa Rais

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi leo tarehe 29 Januari 2026, ametembelea na kukagua ukarabati wa Jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais iliyopo Mtaa wa Luthuli, Posta Jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais ambaye yupo Jijini Dar es Salaam kwa shughuli mbalimbali za kikazi amekagua maendeleo ya ukarabati pamoja na uwekaji wa vifaa na samani katika ofisi mbalimbali zilizopo katika jengo hilo. Baada ya ukaguzi huo, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Richard Muyungi, amemuhakikishia Makamu wa Rais kwamba ukarabati huo umekamilika kwa asilimia mia moja na Jengo litakuwa tayari kwa matumizi kuanzia tarehe 04 Februari 2026.

Benki ya Azania Mdhamini Mkuu Bunge Azania Bonanza 2026 "Yanga na Simba" Kuchuana Jan 31 Dodoma

WAZIRI Mkuu Dk Mwigulu Nchemba, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika bonanza maalumu la Bunge la mashabiki wa Simba na Yanga Jumamosi Januari 31, 2026 ambapo Banking ya Azania ndio wazamini wakuu katika Bonanza hilo. Mwenyekiti wa Klabu ya Michezo ya Bunge, Festo Sanga, ametoa kauli hiyo leo wakati akitambulisha bonanza hilo katika mkutano na waandishi wa habari, ambapo pia amekabidhi vifaa kutoka Benki ya Azania huku akiipongeza Bank hiyo Kwa ushirikiano mkubwa wanaoonyesha. Amesema Bank ya Azania imekuwa ikionesha ushirikiano mkubwa Kwa Serikali Kwa miaka minne mfululizo. "Kwa niaba ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mussa Azzan Zungu tunaishukuru sana Azania Bank Kwa kuendelea Kutoa ushirikiano wao katika sekta ya Michezo". Amesema  Kwa upande wake Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Benki ya Azania, Elizabeth Nyattega amesema benki yao itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kusaidia sekta ya michezo. "Azania Bunge Bonanza tumewza kudhamini...

Makoi Amweleza Waziri Wa Ujenzi Changamoto ya Barabara Moshi Vijijini

  DODOMA. Licha ya Serikali ya awamu ya sita kuendelea kujenga Miundombinu Mizuri ya Barabara hapa nchini, Mbunge wa Jimbo la Moshi vijiji Mhe. Morris Makoi amekutana na kufanya Mazungumzo na Waziri wa Ujenzi Mhe. Abdallah Ulega kuhusiana na Kusuasua kwa Miradi ya ujenzi katika Jimbo hilo. Mhe. Makoyi ametaja barabara hizo ikiwemo barabara ya Rau Madukani- Mamboleo Materuni yenye urefu wa kilomita 9.99 ambapo urefu uliokamilika ni 2.9. Akizungumza na Waziri wa Ujenzi Mhe. Ulega Mara baada ya kukutana na Kufanya Mazungumzo Mhe. Makoi amesema barabara hizo zimekuwa changamoto hivyo ni vyema serikali ikafanya mchakato kukamilisha ujenzi ili wananchi wapate Kutumia barabaraza hizo. "Barabara ya chekereni-Kahe- Mabogini yenye urefu wa kilomita 31.25, kiboriloni- Mbokomu kilomita 14.34, Moshi International school- kibosho kati-Raphael kilomita 13.9, Samanga Chemchem kilomita 9.91, Mamboleo Shimbwe kilomita 10.3 pamoja na barabara ya Kidia road(usuduni-Kidia) kilomita 9.92". Amezita...