Skip to main content

Posts

Showing posts from December 26, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Kassim ashinda Pambano la Knockout ya Mama

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimvisha Salmin Kassim Mkanda wa ubingwa wa WBF baada ya kushinda pambano dhidi ya mfilipino, Adrian Lerasan kwenye tukio maalum la pambano la ngumi la ‘Knockout ya Mama’. Pambana hilo ls kuvutia ambalo lilifuatiliwa pia na Rais Samia Suluhu Hassan limenyika katika ukumbi wa Super Dome, Masaki jijini Dar es Salaam, Desemba 26, 2024.

Waziri Mkuu amewataka sasa mabondia kunufaika na vipaji vyao

  Rais Dkt. Samia apiga simu, awataka mabondia Watanzania kuibeba bendera ya Tanzania kwenye tukio hilo_ WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo kuhakikisha inaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuwawezesha mabondia kunufaika na vipaji vyao. Ametoa Wito huo jana (Alhamisi, Desemba 26, 2024) wakati wa tukio maalum la pambano la ngumi la ‘Knockout ya Mama’ linalofanyika katika ukumbi wa Super Dome, Masaki jijini Dar es Salaam. “Awali michezo hii ilikuwa ni ridhaa, lakini kwasasa tumeweka sheria ambazo zinataka mchezo huu uwe wa kulipwa, ambayo mchezaji akiitwa na kuweka mikataba ni lazima apate maslahi” Aidha, Mheshimiwa Majaliwa ameitaka Wizara hiyo kwa kushirikiana na wadau wa mchezo wa ngumi kuendelea kuhakikisha wanatoa mafunzo bora kwa makocha na wachezaji. “Hii itawezesha kuwa na uhakika kwamba mabondia wa Kitanzania wanapata ujuzi wa kisasa na wanaendelea kufanya vizuri zaidi”. Katika Hatua Nyingine, Waziri Mkuu ameitaka Wizara hiy...

Rais Samia ampigia Simu Waziri Mkuu Juu ya Mchezo wa Ngumi

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza kwa njia ya Simu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan alipopiga simu kuzungumza na wadau na Mashabiki wa mchezo wa ngumi, wakati wa tukio maalum la pambano la ngumi la ‘Knockout ya Mama’ linalofanyika katika ukumbi wa Super Dome, Masaki jijini Dar es Salaam, Desemba 26, 2024  

Rais Samia ampigia Simu Waziri Mkuu Juu ya Mchezo wa Ngumi

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza kwa njia ya Simu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan alipopiga simu kuzungumza na wadau na Mashabiki wa mchezo wa ngumi, wakati wa tukio maalum la pambano la ngumi la ‘Knockout ya Mama’ linalofanyika katika ukumbi wa Super Dome, Masaki jijini Dar es Salaam, Desemba 26, 2024  

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...