Skip to main content

Posts

Showing posts from June 1, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

MWAHUTA YAGAWA NYAMA KWA WENYE UHITAJI, YACHINJA NG’OMBE 700 MWAKA HUU

Mwenyekiti wa Taasisi ya Mkono wa huruma Tanzania (MWAHUTA), Araphaty Japhary Mayala amesema taasisi hiyo imefanikiwa kuchinja takribani ng’ombe 700 mwaka huu kwa ajili ya kugawa nyama kwa makundi mbalimbali yenye uhitaji, ikiwa ni sehemu ya kuendeleza huduma za kijamii na kusaidia wananchi wasiojiweza. Matendo hayo ya huruma ni kutokana na mafundisho ya dini ya kiislamu kama anavyosema Mwenyezi Mungu katika QUR'AN tukufu inapofika sikukuu ya Eid ul-Adha ni vema kuchinja Mnyama ili Kutoa sadaka Kwa jamii inayokuzunguk Akizungumza jijini Dodoma, wakati akitekeleza ibada ya kuchinja Mayala amessema mafanikio hayo yametokana na ushirikiano mkubwa kutoka kwa wadau, viongozi wa serikali, viongozi wa mitaa na wananchi walioshiriki kufanikisha zoezi hilo muhimu. Mayala pia Ametoa shukrani za dhati kwa viongozi wote waliowaunga mkono, hususan Mkuu wa Wilaya ambaye alisema amekuwa mstari wa mbele kutoa ushirikiano ikiwemo kuhakikisha upatikanaji wa ulinzi na huduma za madaktari kwa ajili ya...

WANAFUNZI 246,197 WALIOPANGIWA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO WANAPASWA KURIPOTI SHULENI JULAI 04, 2026 - PROF. SHEMDOE

Na OWM - TAMISEMI, Dar es Salaam Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) Mhe. Prof. Riziki Shemdoe amesema jumla ya wanafunzi 246,197 wakiwemo wasichana 114,102 na wavulana 132,095 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano mwaka 2026 wanatakiwa kuripoti shuleni kuanzia Julai 04, 2026 hadi Julai 31, 2026 kwakuwa muhula wa kwanza wa masomo utaanza Julai 06, 2026.  Prof. Shemdoe amesema hayo leo Juni 01, 2026 katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi Ndogo ya Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI Magogoni Jijini Dar es Salaam, wakati akitoa taarifa kwa umma kuhusu wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya elimu ya ufundi kwa mwaka 2026. “Wanafunzi 172,114 sawa na asilimia 69.9 wakiwemo wasichana 85,987 na wavulana 86,127 wenye sifa wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano katika shule  za sekondari za Serikali 856 zikiwemo shule za bweni 825, kutwa 25 na kutwa na bweni sita (06),” amefafanua Prof. Shemdoe. Aidha, Prof. S...

RAIS SAMIA ATOA NDEGE YA KUWACHUKUA MASHUJAA SERENGETI BOYS WALIOFIKA FAINALI YA AFCON U-17

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa usafiri wa ndege kwa ajili ya kuwachukua mashujaa wa Timu ya Taifa ya Vijana chini ya umri wa Miaka 17 (Serengeti Boys), baada ya kufuzu kucheza fainali ya Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Vijana (AFCON U-17, 2026) Ndege hiyo itaondoka leo, tarehe 01 Juni 2026, majira ya saa 5:00 usiku, kuelekea nchini Morocco, na itarejea Jumatano tarehe 03 Juni 2026. Msafara huo utaongozwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda (Mb.) akiwa ameambatana na viongozi wa Serikali pamoja na Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu (Taifa Stars), lengo ikiwa ni kuongeza nguvu, morali na hamasa kwa Serengeti Boys katika hatua hiyo muhimu. Waziri Mhe. Makonda amemshukuru Mhe. Rais Samia kwa kuendelea kuwekeza katika maendeleo ya michezo nchini pamoja na uamuzi huo wa kurahisisha safari ambayo itaongeza hamasa kwa vijana na kuimarisha uzalendo. Pia amewasisitiza Watanzania kuendelea kuiunga mkono, ...

DKT. MWIGULU ASHIRIKI IBADA YA MAZISHI YA DIWANI AGNES NASANIA WILAYANI IRAMBA

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Jumatatu Juni 1, 2026 ameshiriki ibada ya mazishi ya Diwani wa Kata ya Shelui, Mhe. Agnes Nasania, iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Shelui, wilayani Iramba mkoani Singida. Akizungumza katika ibada hiyo, Dkt. Mwigulu amesema marehemu Agnes Nasania alikuwa kiongozi jasiri, mkweli na mwenye msimamo katika kusimamia maslahi ya wananchi wa Kata ya Shelui. “Agnes alikuwa kiongozi aliyekuwa tayari kusimamia jambo aliloamini ni sahihi kwa manufaa ya wananchi. Alikuwa na ujasiri wa kusema ukweli na kusimamia maendeleo ya watu wake bila kuyumbishwa,” amesema Dkt. Mwigulu. Amesema mchango wa marehemu katika maendeleo ya Kata ya Shelui utaendelea kukumbukwa na wananchi pamoja na viongozi aliowahi kufanya nao kazi. Katika hatua nyingine, Dkt. Mwigulu ameahidi kuendelea kuwa karibu na familia ya marehemu na kusaidia ustawi wa watoto wake ili kuhakikisha wanaendelea na masomo na kutimiza ndoto zao. Aidha, amewataka w...

RC TANGA AUNDA KAMATI UBOMOAJI NYUMBA ZA KAYA 67

 Na Mwandishi Wetu, Tanga MKUU wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Balozi Dkt. Batilda Burian, ameunda Kamati Maalum ya dharura kuchunguza sakata la uvunjaji wa nyumba za wananchi Kijiji cha Msakangoto kilichopo kata Kigombe wilayani Muheza. Uamuzi huo umekuja kufuatia msukumo mkubwa wa kisiasa na kibinadamu uliowekwa na Mbunge wa Muheza na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma (MwanaFA), ambaye aliahirisha majukumu ya kitaifa na kupiga kambi kijijini hapo kushughulikia dharura hiyo. MwanaFA, ambaye alifika katika Kitongoji cha Maisha Plus Mei 26 na kurejea Mei 28, alionyesha kukerwa na kitendo cha Kampuni ya Amboni Plantation kubomoa nyumba za kaya 67 kienyeji na kuwaacha wananchi wakilala nje, hatua iliyomfanya amfuate RC ofisini kwake na kuweka mikakati ya kuwajibisha waliohusika. Ubomoaji wa Siri Bila Polisi Kujua Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa leo Juni 1, 2026, Balozi Batilda amesema Serikali inahitaji ufafanuzi wa kina kuhusu mchakato huo,...

TADB YAWEZESHA WAFUGAJI WADOGO 92,831

 Na Mwandishi Wetu JUMLA ya wafugaji wadogo 92,831 na wadau wa mnyororo wa thamani wa maziwa wa Tanzania Bara na Visiwani-Zanzibar wamenufaika na Mradi Shirikishi wa Wasindikaji na Wazalishaji wa Maziwa (TI3P) tangu ulipoanzishwa mwezi Machi mwaka 2022, ambapo asilimia 30 ya wanufaika hao ni wanawake. Mradi huo wa miaka minne unafadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania - TADB pamoja na Bill & Melinda Gates Foundation huku ukitekelezwa kwa kushirikiana na Heifer International, Land O’Lakes Venture37 pamoja na Tanager. Akizungumza wakati wa maonesho ya Wiki ya Maziwa Mkoani Iringa, Mratibu wa Mradi wa TI3P, Joseph Mabula, alisema mradi huo unalenga kutatua changamoto mbali mbali zilizopo kwenye mnyororo wa thamani wa sekta ndogo ya maziwa ili kuongeza uzalishaji, na kuboresha kipato cha wafugaji wadogo wa maziwa nchini. Aliishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuipa uzito mkubwa sekta ndogo ya maziwa. Mabula alisema tangu k...

MWENYEKITI CCM MKOA WA TANGA MFANO WA KUIGWA

Na Mwanamkuu Mwandoro, Tanga. Viongozi mkoani Tanga wametakiwa kuiga mfano kutoka Kwa mwenyekiti wa CCM Mkoa na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa Rajabu Abdarahman ambapo hujali,kuasidi na kusikiliza bila ubaguzi wa aina yoyote. Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyinga ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa CCM Mabala Mlolwa wakati wa dua ya kuwaombea waliotangulia mbele ya haki iliyofanyika wilayani Pangani Kijiji Cha Stahabu pwani na kuwakutanisaha wanazuoni kutoka katika wilaya zote za mkoa wa Tanga. Aidha Mlolwa aliongeza kuwa ili kupata mafanikio katika uongozi ni lazima kuwa mtu wa watu na ukiweka maslahi binafsi mbele, ubaguzi ama majivuno ni ngumu kufanikiwa. "Nimpongeze ndugu yangu Rajabu kwa jambo hili kwani sio jambo dogo kuwakutanisaha wananchi kutoka wilaya zote za mkoa,kweli hapa umeweza kudhihirisha kuwa wewe ni kiongozi wa mkoa na unayejali", Mlolwa. Kwa upande wake Mwenyekiti Rajabu amefanikiwa kuwashika mkono vijana wa Ahlu zaaman ...

RUTO AOMBA RADHI KWA WAKAZI WA KASKAZINI MWA KENYA, AAHIDI ENZI MPYA YA MAENDELEO

Wajir, Kenya Rais wa Kenya, William Ruto, ameomba radhi kwa wakazi wa Kaskazini mwa Kenya kwa kile alichokitaja kuwa ni miaka mingi ya kutengwa na kusahaulika katika mgao wa maendeleo, huku akiahidi kwamba serikali yake imejizatiti kurekebisha hali hiyo kupitia uwekezaji mkubwa katika miundombinu, elimu na huduma za kijamii. Ruto alitoa kauli hiyo wakati akiongoza maadhimisho ya miaka 63 ya Madaraka Day yaliyofanyika katika Wajir County, tukio lililoingia katika historia ya Kenya kwa kuwa ni mara ya kwanza kwa sherehe hizo za kitaifa kufanyika katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa nchi. Akihutubia maelfu ya wananchi waliojitokeza katika Uwanja wa Wajir, Rais huyo alisema serikali zilizopita zilifanya makosa kwa kuyatenga maeneo ya Kaskazini katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo, jambo ambalo limesababisha wananchi wengi kukosa fursa muhimu za kiuchumi na kijamii. “Tunatambua kuwa wananchi wa eneo hili wamepitia changamoto nyingi kutokana na kutengwa kwa muda mrefu. Leo ninaomba ra...