Skip to main content

Posts

Showing posts from August 4, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Wanachama na Mashabiki wa Timu ya Yanga Igunga Waadhimisha Wiki ya Mwananchi Kwa Kutoa Msaada

Na Lubango Mleka, Igunga. WANACHAMA na Mashabiki wa Timu ya Yanga Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora wameadhimisha wiki ya Mwananchi kwa kutembelea wodi ya Watoto katika Hospitali ya wilaya ya Igunga na Gereza la Wilaya ya Igunga na kutoa mahitaji mbalimbali. Kilele hicho kimeanza kwa maandamano ya amani kutokea uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine uliopo Mamlaka ya mji mdogo wa Igunga na kuelekea katika Hospitali ya wilaya ya Igunga na kuwafariji Wazazi na Watoto ambao ni wagonjwa kwa kuwapatia juisi, maji ya kunywa, sabuni za unga na vipande, dawa za miswaki, mafuta pamoja na pampasi.  Wamehitimisha maadhimisho hayo kwa kutembelea Gereza kuu wilaya ya Igunga ambapo wametoa kiasi cha sh. 30,000 kwa ajili ya kununua kifurushi cha Azam ili Wafungwa na Mahabusu wapete fursa ya kufuatilia kilele cha wiki ya Mwananchi, aidha wametoa sabuni za unga na vipande, viwembe, maji ya kunywa na mipira miwili kwa ajili ya kufanya mazoezi.  Mkaguzi Msaidi I. R. Ntandu kwa niaba ya Mkuu wa gereza la w...

Kampeni ya Msaada wa Kesheria ya Mama Samia Inapatikana Kwenye Maonesho ya Nane Nane

Na Mwandishi Wetu BAADA ya kusaidia maelefu ya Watanzania kupitia maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam(DITF), Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia au maarufu kama Mama Samia Legal Aid Campaign, sasa iko katika maonesho ya nanenane jijini Dodoma. Kampeni hiyo ambayo tangu kuzinduliwa kwake mwaka jana, imekuwa ikitumia wabobezi katika tasnia hiyo ya sheria kutatua migogoro mbalimbali inayotokea kwenye jamii katika mikoa mbalimbali wanakopita iko katika maonesho hayo kutoa msaada huo wa kisheria kwa wananchi wanaotembelea maonesho hayo ya nanenane. Mbali na kurejesha tabasamu kwa wananchi wenye migogoro mbalimbali, pia kampeni hiyo imefanyika kama darasa la kutoa elimu kuhusu masuala ya sheria na namna haki inavyoweza kupatikana kwa kutumia sheria hizo. Kampeni hiyo ya Mama Samia Legal Aid Campaign katika maonesho hayo, pia inalenga kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma za ushauri na ufumbuzi wa matatizo mbalimbali ya kisheria wanayokumbana nayo k...