Skip to main content

Posts

Showing posts from June 28, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt.Doto Biteko Mashaka achukua fomu Jimbo la Bukombe

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Mashaka Biteko aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Bukombe amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kutetea Ubunge katika Jimbo la Bukombe. Dkt. Biteko amechukua fomu hiyo na kuirejesha kwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Bukombe, Ndugu. Leonard Yesaya Mwakalukwa mapema leo Juni 29, 2025. Zoezi la uchukuaji fomu katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) linaendelea nchi nzima ambapo watia nia tofauti wameendelea kujitokeza kwa ajili ya kuchukua fomu za Ubunge na Udiwani.

Majaliwa Amwakilisha Rais Dkt. Samia Kwenye Kongamano la Amani, Mwanza

  WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Juni 29, 2025 amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye kongamano la Afrika Mashariki la Amani lililoandaliwa na The Islamic Foundation pamoja na Safina Islamic Foundation, katika viwanja vya shule ya msingi Mirongo jijini Mwanza.  Kongamano hilo ni jukwaa muhimu la kuwaleta pamoja viongozi wa dini, wataalamu, vijana, wanawake na wadau wa maendeleo kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika Mashariki ili kujadili masuala ya msingi yanayogusa jamii kwa ujumla. Kongamano lina kaulimbiu isemayo *_Amani, Imani na Mshikamano_*

Kikongwe cha miaka 85 abeba fomu ubunge Tarime mjini

Tarime, Juni 28, 2025 Katika hali ya kusisimua na ya kipekee kabisa, Mzee Geregole Mgendi Nyanchini mwenye umri wa miaka 85 ameandika historia mpya leo baada ya kuchukua rasmi fomu ya kuwania ubunge wa Jimbo la Tarime Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Mzee Nyanchini, ambaye ni mkazi wa muda mrefu wa Tarime na mkongwe aliyejikita katika siasa na maendeleo ya jamii, amesema ameamua kujitosa katika kinyang’anyiro hicho kwa lengo la kutumia busara na uzoefu wake katika kuwahudumia wananchi kwa haki, heshima na maadili ya uongozi wa kizalendo. “Nimeamua kuchukua fomu kwa sababu naamini bado nina uwezo wa kulisemea jimbo hili, kulitumikia kwa moyo mmoja, na kuhakikisha kila mwananchi anapata haki yake ya msingi ya maendeleo,” amesema Mzee Nyanchini akiwa amevalia sare ya kijani ya chama chake. Hatua yake hiyo imeibua hisia mseto kwa wakazi wa Tarime Mjini, wengi wakimtazama kama mfano wa uzalendo na dhamira ya kweli ya kulitumikia taifa bila kujali umri. Wengine wameonyesha kuvutiwa n...

Mzee Geregole Nyanchini ( 85 ) ajitosa ubunge Tarime Mjini

Tarime, Juni 28, 2025 Katika hali ya kusisimua na ya kipekee kabisa, Mzee Geregole Mgendi Nyanchini mwenye umri wa miaka 85 ameandika historia mpya leo baada ya kuchukua rasmi fomu ya kuwania ubunge wa Jimbo la Tarime Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Mzee Nyanchini, ambaye ni mkazi wa muda mrefu wa Tarime na mkongwe aliyejikita katika siasa na maendeleo ya jamii, amesema ameamua kujitosa katika kinyang’anyiro hicho kwa lengo la kutumia busara na uzoefu wake katika kuwahudumia wananchi kwa haki, heshima na maadili ya uongozi wa kizalendo. “Nimeamua kuchukua fomu kwa sababu naamini bado nina uwezo wa kulisemea jimbo hili, kulitumikia kwa moyo mmoja, na kuhakikisha kila mwananchi anapata haki yake ya msingi ya maendeleo,” amesema Mzee Nyanchini akiwa amevalia sare ya kijani ya chama chake. Hatua yake hiyo imeibua hisia mseto kwa wakazi wa Tarime Mjini, wengi wakimtazama kama mfano wa uzalendo na dhamira ya kweli ya kulitumikia taifa bila kujali umri. Wengine wameonyesha kuvutiwa n...

Msama achukua fomu ya kugombea ubunge Jimbo la Ukonga

Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama leo Juni 29, 2025 amefika katika Ofisi za Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala na kuchukua Fomu ya Kugombea Ubunge Jimbo la Ukonga. Amekabidhiwa Fomu hiyo na Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Ilala, Chief Sylvester Yaredi.

Dkt.Matiang'i:Ruto Hanitishi, Nitavua Koti na Kumkabili

ALIYEKUWA Waziri wa Usalama wa Ndani na Utawala wa Kitaifa Nchini Kenya Dokta Fredy Okeng'o Matiang’i Jumamosi, Juni 28,2025 alieleza matumaini yake kuwa atakitwaa kiti cha urais katika uchaguzi mkuu wa 2027.  Dkt Matiang’i pia amedokeza kuwa hivi karibuni ataanza msururu wa shughuli za kisiasa zinazolenga kuimarisha umaarufu wake ili amng’oe Rais William Ruto mamlakani.  Akizungumza alipohudhuria mazishi  eneo bunge la Bomachoge Chache, Kaunti ya Kisii mnamo Jumamosi, Waziri huyo wa zamani alisema Kenya inaelekea pabaya kwa sababu ya kuongezeka kwa mauaji ya wale wanaodhaniwa kukosoa utawala wa Kenya Kwanza na ongezeko la gharama ya maisha.  “Tuiombee nchi yetu kwa sababu kama mnavyoona, mambo si mazuri, tumefikia wakati mgumu. Mliona yale yaliyotokea juzi watoto wetu walipouawa lakini wale walioko madarakani wanadai kuwa wauaji wao walitoka katika jamii moja. Niwaulize nyinyi watu wangu, hamjaona kwamba nchi inaelekea pabaya? Sasa ni wakati wa kuangalia jinsi gani ...

Meja Jenerali Gaguti Ahitimisha Mafunzo Askari Wapya

Mkuu wa Utumishi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Meja Jenerali Marco Elisha Gaguti amehitimisha Mafunzo ya Askari wapya katika Shule ya Mafunzo ya Awali ya Kijeshi iliyopo Kihangaiko , Msata Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani, leo tarehe 28 Juni 2025. Askari waliohitimu Mafunzo wamekula kiapo cha Utii mbele ya Mkuu huyo wa Utumishi Jeshini. Akizungumza wakati wa sherehe hizo, Meja Jenerali Gaguti amewataka Askari wapya kwenda kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia kiapo cha Utii walichokula na kuwa tayari muda wote kuilinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kumtii Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu. Askari hao wametakiwa kuzitunza Afya zao kiakili na kimwili ili wakati wote wawe tayari kuilinda Mipaka ya Tanzania na kulitumikia Taifa. Aidha Meja Jenerali Gaguti amewaasa Askari hao kuzingatia mambo manne kwa Mwanajeshi ambayo ni nidhamu nzuri, Utii, Uhodari na Uaminifu kwani Taifa linawaamini na kuwategemea. Naye  Mkuu wa Shule...

Sekreterieti ya CCM ikitathmini uchukuaji wa fomu

Sekreterieti ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, ikiongozwa na Mwenyekiti wake, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, imekutana katika kikao chake maalum leo Jumamosi tarehe 28 Juni 2025, kufuatilia mchakato wa uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kuwania uteuzi ndani ya CCM.  Kikao hicho kilipokea na kufuatilia kwa karibu taarifa mbalimbali za zoezi hilo la uchukuaji wa fomu za kuwania uteuzi wa kugombea nafasi za uwakilishi katika vyombo vya dola, lililoanza rasmi leo kwa mchakato wa ndani ya CCM, katika maeneo yote nchi nzima.  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa awali, ratiba ya kuchukua na kurejesha fomu hizo za kuwania kuteuliwa ndani ya CCM, imeanza *leo tarehe 28 Juni 2025, saa 2:00 asubuhi na itahitimishwa tarehe 2 Julai 2025, saa 10:00 jioni.* Ratiba hiyo itahusisha uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kuwania uteuzi nafasi za; Ubunge wa Jimbo, Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi, Ubunge wa Viti Maalum, Ujumbe wa Baraza la Wawa...

Waziri Mkuu aagana na Balozi wa Angola aliyemaliza muda wake nchini

_▪️Ampongeza kwa kutumikia nchi yake kwa mafanikio makubwa ya kidiplomasia nchini._ _▪️Balozi de Oliveira asema Angola itaendelea kuwa mshirika wa karibu wa Tanzania._   WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo Juni 28, 2025 amemuaga rasmi Balozi wa Angola nchini Tanzania, Sandro Agostinho de Oliveira, ambaye anamaliza muda wake wa uwakilishi baada ya kutumikia nchi yake kwa mafanikio makubwa ya kidiplomasia nchini.   Mheshimiwa Majaliwa ambaye ameagana na Balozi huyo jijini Dodoma kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu, amempongeza Balozi de Oliveira kwa mchango wake mkubwa katika kuimarisha ushirikiano wa kibiashara, kisiasa na kijamii kati ya Tanzania na Angola.    Mheshimiwa Majaliwa amemweleza balozi huyo kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kuthamini na kuendeleza uhusiano wa kidiplomasia na kidugu kati ya Tanzania na Angola katika nyanja zote muhimu za maendeleo. Balozi de Oliveira ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano mzuri alioupata wakati wote wa uwakilishi ...

Dkt.Samia amuagiza Dkt Kimambo kusimamia weledi na uongozi Muhimbili

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imefanya uwekezaji mkubwa wa vifaa tiba na wataalaam wenye utaalam wa juu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ili iweze kutoa huduma bora zinazokidhi viwango vya kimataifa Rais Dkt. Samia ameyasema hayo leo wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali walioteuliwa hivi karibuni kushika nafasi mbalimbali katika viwanja vya Ikulu, Chamwino mkoani Dodoma. Rais Dkt. Samia amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo kuendelea kusimamia utoaji wa huduma katika hospitali hiyo kubwa na kongwe, kiongozi katika matibabu ya ubingwa bobezi na utalii tiba katika Kanda wa Afrika Mashariki na Kati. “Muhimbili inahitaji professionalism na administative skills, nenda kaendeleze pale alipoishia Prof. Janabi, nimepitia wasifu wa watu wengi lakini nikaona wewe Dkt. Delilah Kimambo ndio unafaa kuiongoza hospitali hiyo, nakutakia kila la heri katika kutekeleza majukumu yako” ameongeza Rais Dkt. Samia. Aidha, Rais Dkt. Sam...

Nsekela awania ubunge Jimbo la Kyer

NSEKELA AWANIA UBUNGE JIMBO LA KYERWA Mjumbe mkutano mkuu wa Taifa anyeiwakilisha Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera Khald Mussa Nsekela amechukua fomu kuomba kuteuliwa na CCM kugombea ubunge jimbo la Kyerwa. Nsekela baada ya kuchukua fomu amesema lengo la kuchukua fomu na kugombea jimbo hilo ni kuchochea maendeleo katika jimbo pia,kuwa yeye ni kada wa Chama hicho hivyo aliona ni vyema kutumia haki yake ya kikatiba ili akifanikiwa aweze kutoa mchango wake katika kulitumikia chama na wana Kyerwa. Mwisho