Skip to main content

Posts

Showing posts from June 15, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

CTI YAPONGEZA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

 Na Mwandishi Wetu SHIRIKISHO la Wenye Viwanda Nchini (CTI), limepongeza Bajeti Kuu ya mwaka 2026/2027 ikisema kuwa kama itatekelezwa vizuri itasaidia kulinda na kustawisha viwanda vya ndani . Shirikisho hilo limesema serikali imechukua asilimia 50 ya mapendekezo ya wenye viwanda na kuyaweka kwenye bajeti kwani kati ya mapendekezo 110 waliyoyawasilisha, 51 yamechukuliwa. Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Shirikisho hilo, Hussein Sufian wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu masuala mbalimbali yaliyomo kwenye bajeti kuu ya serikali. Alisema kwenye bajeti hiyo serikali imejitajidi kwa kiasi kikubwa kuchumua mapendekezo ya wenye viwanda kuhusu kodi mbalimbali ambazo zilikuwa kero kwa wafanyabiashara na wenye viwanda. Alisema CTI inaona kuwa bajeti hii, yenye thamani ya Shilingi trilioni 62.5, inaendana na malengo ya kujenga uchumi stahimilivu kupitia matumizi ya teknolojia ya kidijitali, uwekezaji wa kimkakati na sera endelevu za kifedha. Aidha, alip...