*BARUA YA WAZI KWA MWENYEKITI WA CCM TAIFA* *MH. SAMIA SULUHU HASSAN* YAH. *MAONI YA KUBADILISHA UTARATIBU WA KURUDISHA MAJINA MATATU* Mheshimiwa Mwenyekiti, Husika na kichwa cha barua hapo juu Kutokana na Idadi ya wananchi kuongezeka, Chama chetu pia kimeongeza Idadi ya wanachama wengi wenye sifa na uwezo wa kushika nafasi mbalimbali za Uongozi, Lakini pia idadi ya wasomi nayo imeongezeka hivyo sasa hivi tuna rasilimali watu kubwa, Idadi hii kubwa inapelekea pia kuwa na wanachama wengi wanaowania nafasi za Uongozi, Hapo awali wanachama waliokuwa wakiwania nafasi za Uongozi walikuwa wachache na hata wengine walikuwa wakishawishiwa kuombwa kugombea hivyo ilikuwa ni rahisi kuchuja na kupata majina matatu ya wanachama watakaokwenda kupigiwa kura,Lakini sasa hivi hali imebadilika Imefikia hatua mamia na huenda hata maelfu ya wanachama wakajitokeza kuomba ridhaa ya kuwania nafasi za Uongozi hivyo si rahisi kwa majina matatu tu kutosha kumpata mtu sahihi anayestahili kuongoz...
Marato tv - Sauti ya Jamii