Skip to main content

Posts

Showing posts from May 26, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Diaspora Waongeza Uwekezaji Hadi Billion 11.7 Nchini

Serikali imefanikiwa kuimarisha ushiriki wa Watanzania wanaoishi nje ya nchi (Diaspora) katika uchumi wa taifa, baada ya kuwekeza zaidi ya shilingi bilioni 11.7 kupitia Mfuko wa Uwekezaji wa UTT AMIS hadi Februari 2026, kutoka shilingi bilioni 7.5 zilizowekezwa mwaka uliopita. Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi Leo Mei 26,2026 Bungeni jijini Dodoma, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo ametoa Takwimu hizo kwa mwaka wa fedha 2026/2027, zikionesha ongezeko la imani ya diaspora katika mifumo rasmi ya uwekezaji nchini. Balozi Kombo ameeleza kuwa ongezeko hilo linatokana na jitihada za kimkakati za kuhamasisha taasisi za kifedha kutoa huduma mahsusi kwa Watanzania wa diaspora, lengo likiwa ni kuongeza ushiriki wao katika maendeleo endelevu ya taifa. Katika hatua hiyo, akaunti maalum za diaspora zimeanzishwa katika benki sita ambazo ni TCB, CRDB, NBC, NMB, Azania na Absa, hatua inayorahisisha uwekezaji, utunzaji wa fedha na uhawilis...

BUTIAMA WALIA TAA ZA BARABARANI, SERIKALI YATOA MAJIBU

MBUNGE wa Jimbo la Butiama, Mhe. Dkt. Charles Mahera, ameiiomba Serikali kuharakisha uwekaji wa taa za barabarani katika maeneo mbalimbali ya jimbo hilo yanayopitiwa na barabara ya Mkutano,Natta kupitia Nyamwisuwa. Akizungumza bungeni jijini Dodoma Mei 26, 2026 wakati akiuliza swali la nyongeza, Dkt. Mahera amesema barabara hiyo ilianza kujengwa muda mrefu huku kipande cha Mkutano hadi Nyamwisuwa kikikamilika tangu mwaka 2007, lakini wananchi bado hawajanufaika na huduma ya taa za barabarani. “Barabara hii inapitia maeneo mengi sana ya Jimbo la Butiama lakini maeneo hayo hayana taa kuanzia Nyambange, Nyakanga, Butuguri, Mbusegwe, Kiguri, Kiarano hadi Bisale. Wananchi wa Butiama wanasubiri taa hizi kwa muda mrefu tangu mwaka 2023,” amesema Dkt. Mahera. Dkt. Mahera  ameiomba Serikali kuhakikisha wananchi wa Butiama wanapatiwa huduma hiyo muhimu ili kuongeza usalama pamoja na kuchochea shughuli za kijamii na kiuchumi katika maeneo hayo. Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhan...

MBUNGE MARY AENDELEA KUWAPA TABASAMU WANANCHI WA SERENGETI

 Mbunge wa Jimbo la Serengeti, Mary Daniel Surati, ameendelea kuweka historia ya maendeleo katika jimbo hilo baada ya kutoa na kugawa shilingi milioni 88 kwa ajili ya miradi ya huduma za kijamii. Mary alitoa fedha hizo kupitia Mfuko wake wa Kuchochea Maendeleo ya Jimbo, katika hafla maalum iliyofanyika Mei 20, 2026 wilayani Serengeti na kuhudhuriwa na madiwani wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, viongozi wa serikali na wananchi. Mbunge huyo alisisitiza dhamira yake ya kuhakikisha wananchi wa Serengeti wanapata huduma bora za afya, elimu na maendeleo ya kijamii kwa ujumla. Katika mgao huo wa fedha, kiasi cha shilingi milioni 25 kimetengwa kwa ajili ya kugharimia ukamilishaji wa Zahanati ya Kisaka, mradi unaotarajiwa kuongeza upatikanaji wa huduma za afya kwa wakazi wa eneo hilo na kupunguza adha ya wananchi kusafiri umbali mrefu kufuata matibabu. Mbunge Mary akikabidhi hundi ya mfano ya milioni 25/- Mbali na fedha hizo, Mbunge Mary pia alikabidhi madawati kadhaa yenye thamani ya shilingi...

TRA Mkoa wa Kagera Yakusanya Billions 55

Mamlaka ya mapato Tanzania TRA mkoa wa Kagera kwa kipindi cha miezi mitatu Januari hadi Machi mwaka huu wamevuka lengo la ukusanyaji mapato na kukusanya shilingi bilioni 55. Meneja wa TRA mkoa wa Kagera CPA Joseph Mutalemwa ametoa takwimu hizo Mei 26,2026 katika maonyesho ya elimu ya juu kupitia bodi ya mikopo (HESLB) yanayoendelea katika viwanja vya soko kuu mjini Bukoba. Amesema kuwa, Mamlaka hiyo katika kipindi cha miezi mitatu Januari hadi Machi mwaka huu walipanga kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 51 lakini wamevuka lengo hilo na kukusanya shilingi  bilioni 55. Ameeleza kuwa, kupanda kwa lengo hilo kumetokana na elimu ambayo wamekuwa wakitoa maeneo mbalimbali mkoani humo ambayo imesaidia wafanyabiashara kulipa kodi yao bila shuruti. Mutalemwa amewashauri wafanyabiashara kuwasirisha ritani zao kwa maana ya hesabu za biashara ili kuangalia kiasi cha kodi wanachokilipa kwa mwaka husika kama kinalingana na kiasi cha kodi wanachopaswa kulipa. “Sheria imeweka uhuru kwamba kabla y...

NIDA YAWAPA ELIMU HII WANANCHI WA BUKOBA

Na Angela Sebastian ;Bukoba Afisa habari wa Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) makao makuu Alfan Mlacha amewashauri wananchi wa mkoa wa Kagera kupuuza jumbe ambazo zimekuwa zikitumwa na wezi wa mitandaoni zikiwataka  kulasimisha laini zao. Mlacha ameyasema hayo leo katika maonyesho ya elimu ya juu kupitia bodi ya mikopo (HESLB) yanayoendelea katika viwanja vya soko kuu mjini Bukoba ambapo amesema kuwa, kuna watu wanaojihusisha na utapeli wa kutumia simu za mkononi ambao wamekuwa wakituma jumbe za kawaida wakidai wao ni Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) na kuwa jumbe hizo zipuuzwe. Mlacha ameeleza kuwa, jumbe hizo zinazotumwa kupitia simu za mkononi za watu binafsi zinapaswa zipuuzwe, kama kuna mtu ana jambo lolote kuhusu vitambuliaho vya taifa (NIDA) awasiliane na kituo chao cha huduma kwa wateja kupitia namba 0232210500. “Ukiona watu wanadukua kitu fulani au huduma fulani ujue huduma hiyo ni ya muhimu sana kwa jamii kwahiyo NIDA ni sehemu ya muhimu kwa wananchi  ...

Tume ya Madini Yatoa Wito wa Uhakiki wa Taarifa za Leseni za Madini

📍Dodoma Tume ya Madini imewataka wamiliki na waombaji wote wa leseni za utafiti na uchimbaji wa madini nchini kuhakiki taarifa zao za leseni na maombi kabla ya Juni 25, 2026, ili kuboresha mfumo wa usimamizi na utoaji wa leseni za madini nchini. Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na Tume, zoezi hilo linahusisha wamiliki wa leseni za utafiti, uchimbaji mdogo, wa kati na mkubwa wa madini pamoja na waombaji wa leseni mbalimbali za madini. Taarifa zinazotakiwa kuhakikiwa ni pamoja na anuani zinazojumuisha sanduku la posta, barua pepe, namba za simu pamoja na jina na namba za simu za msimamizi wa mfumo wa portal. Vilevile, wahusika wanatakiwa kuwasilisha namba ya mlipa kodi (TIN), nakala ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au pasi ya kusafiria, pamoja na nyaraka za kampuni ikiwemo Brela Search au MEMART endapo kutakuwa na mabadiliko ya wakurugenzi. Aidha, Tume imeeleza kuwa nguvu ya kisheria (Power of Attorney) ya msimamizi wa portal nayo ni miongoni mwa nyaraka muhimu zinazopaswa kuwasilishw...

Mining Commission Calls For Verification Of Mineral Licence Information

📍Dodoma The Mining Commission has called upon all holders and applicants of mineral prospecting and mining licences across the country to verify their licence and application information before June 25, 2026, in a move aimed at strengthening the management and administration of mineral licences nationwide. According to a public notice issued by the Commission, the verification exercise covers applicants and holders of prospecting licences, primary mining licences, mining licences and special mining licences. The Commission said the exercise is intended to ensure that all records contained in the mineral licensing database remain accurate, complete and up to date. Information required for verification includes contact details such as postal addresses, email addresses, telephone numbers, and the names and contact details of portal administrators. Stakeholders will also be required to submit their Taxpayer Identification Number (TIN), copies of National Identification Authority (NIDA) ca...

Waziri Mkuu Ateta na Rais wa Benki ya Afdb

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amefanya mazungumzo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dkt. Sidi Ould Tah kando ya Mkutano wa 61 wa Mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika unaofanyika leo Jumanne Mei 26, 2026 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kintele (Kintele Congress Centre) jijini Brazzaville, Jamhuri ya Kongo. Mazungumzo hayo yalijikita katika masuala mbalimbali ya maendeleo pamoja na ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na taasisi hiyo. Dkt. Mwigulu anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mkutano huo unaowakutanisha viongozi mbalimbali wa Afrika pamoja na wadau wa maendeleo kujadili masuala ya uchumi, uwekezaji na maendeleo ya bara la Afrika.

Makuruma asema Uwanja wa ndege Serengeti kuanza ujenzi

Na Godfrey Marwa, Serengeti  Mwenyekiti wa baraza la madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Ayubu Mwita Makuruma amebainisha kuwa uwanja wa Kimataiafa wa Serengeti umepata mwafaka kwa msaada wa Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na tayari serikali imeanza hatua mbalimbali rasmi kuanza utekelezaji wa mradi huo uliosubiliwa kwa miaka mingi ili kuchochea mageuzi ya kiuchumi na kijamii kupitia utalii  Aliyasema hayo katika kikao cha baraza hilo cha robo ya tatu kuanzia Januari hadi Machi, 2026,kilichofanyika jana Mei,20,2026, kupokea taarifa za maendeleo kutoka katika kamati za Halmashauri hiyo pamoja na taasisi za serikali na mashirika. "Suala la uwanja wa ndege limepata mwafaka kwa msaada wa Dkt.Samia Suluhu Hassan,mbunge peleka salaam,tunafurahi mambo yanavyoendelea hivi karibuni timu maalu inakuja Serengeti kuhakikisha ujenzi unaenda kuanza,, Kwa upande mwingine madiwani wa baraza hilo wameshiriki hafla ya  kupokea mgawanyo wa fedha milioni 88,za mfuk...

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Akaribisha Wadau wa Maendeleo

  Na Mwanamkuu Mwandoro, Tanga. Mkuu wa mkoa wa Tanga Balozi Batilda Buriani afungua milango Kwa wadau wanaopenda maendeleo kuchangia ujenzi wa kituo cha tiba ya moyo KCMC. Ametoa Rai hiyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake akiwaalika wadau katika hafla ya chakula Cha jioni kitachofanyika katika hoteli ya Tanga beach resort,wadau hao ni wafanya biashara,wawekezaji na sekta ya afya. Balozi Batilda amesema kuwa ujenzi wa kituo hicho Hadi kukamilika kwake utagharimu kiasi Cha shilingi bilioni 25 na mpaka sasa zilizopatikana ni shilingi bilioni 22 na kufemea shilingi bilioni 3. "Ujenzi wa kituo hicho ni neema Kwa wagonjwa wa ukanda huu wa kaskazini kwani kumekuwa na wangonjwa wengi wanaoshindwa kufika muhimbili kupatiwa matibabu kutokana na hali,hivyo basi niwaombe wafanya biashara na wadau wengine kuchangia ili kisaidia upatikanaji wa vifaa tiba kwani pesa iliyopatikana ambayo shilingi bilioni 22 inatarajiwa kukamilisha jengo lote na zinahitajika bilioni 3 Kwa...

Dkt. Yonazi Aupongeza Ubalozi wa Tanzania Nchini Msumbiji Kuimarisha Diplomasia

Na, mwandishi wetu - Msumbiji Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu Dkt. Jim Yonazi ameupongeza Ubalozi wa Tanzania nchini Msumbiji kwa namna unavyoendelea kutekeleza majukumu yake na kuimarisha mahusiano baina ya nchi hizo mbili. Ametoa pongezi hizo alipotembelea ofisi hizo pamoja na ujumbe alioongozana nao kwa lengo la kushiriki katika ziara ya kubadilishana uzoefu kati ya Tanzania na Msumbiji kuhusu hatua za mapema kabla ya majanga unaoendelea kwa siku tano kuanzia tarehe 25 hadi 29 Mei, 2026 Mjini Maputo Msumbiji. Dkt. Yonazi amezungumza na watumishi wa ubalozi huo na kupokea taarifa fupi ya utekelezaji wa majukumu ya Ubalozi iliyotolewa na Mwambata fedha Bw. Samson Marwa kwa niaba ya Mhe. CP. Hamad Khamis Hamad, Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji ambaye alikuwa katika majukumu mengine. Aidha, amewashukuru watumishi wa ubalozi huo kwa namna wanavyoendelea kutekeleza majukumu ya msingi huku wakiiwakilisha nchi na kute...