Skip to main content

Posts

Showing posts from May 27, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Majaliwa Akutana na Viongozi Wizara ya Ardhi ya Japan Pamoja na Shirikisho La Wawekezaji (Jaida)

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa Mei 27, 2025, alikutana na Waziri wa Ardhi, Miundombinu, Usafirishaji na Utalii wa Japan,  Mheshimiwa Hiromasa Nakano  kwenye Makao Mkuu ya Wizara hiyo Tokyo Japan.  Aidha, Mheshimiwa Majaliwa alifanya mazungumzo na Rais wa Shirikisho la Wawekezaji katika Sekta ya Miundombinu la Japan (JAIDA)  Miyamoto Yoichi pamoja na ujumbe wake ambapo walijadiliana kuhusu masuala mbalimbali ya uwekezaji kwenye sekta za Ardhi, Miundombinu pamoja na Usafirishaji.

Chadema Yapata Pigo

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi, kwa mamlaka aliyonayo ameamua kusitisha kuwapa ruzuku CHADEMA hadi watakapotekeleza maelekezo ya Msajili wa Vyama vya Siasa, kwa sababu chama hicho hakina viongozi wanaoweza kusimamia mapato, matumizi na marejesho ya fedha hizo za umma. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa hii leo Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imewakumbusha wanachama na viongozi wa CHADEMA kuwa, kwa mujibu wa kifungu cha 19 cha Sheria ya Vyama vya Siasa Msajili anayo mamlaka ya kusimamisha usajili wa chama hicho, endapo kitaendelea kuwatambua wanachama waliotajwa kuwa ni viongozi wa chama hicho.  Aidha Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imesisitiza kuwa John Mnyika, Amani Golugwa, Ali Ibrahim Juma, Godbless Lema, Dkt. Rugemeleza Nshala, Rose Mayemba, Salima Kasanzu na Hafidhi Ali Salehe sio viongozi wa CHADEMA pamoja na watendaji wengine wote walioteuliwa katika kikao cha Baraza Kuu la Januari 2025. Msajili huyo pia amebainisha kwamba endapo CHADEMA wataen...

Dkt. Biteko Akutana na Mtendaji Mkuu Wa Puma Duniani

  📌 Tanzania na PUMA kuimarisha ushirikiano 📌 PUMA kuendelea kuwekeza zaidi Tanzania Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amekutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Nishati ya PUMA Energies, Duniani Bw. Mark Russell. Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Mei 27, 2025 jijini Dodoma, Dkt. Biteko ameipongeza Kampuni ya PUMA Energies kwa kuwekeza nchini na kutoa huduma ya viwango vya juu katika bidhaa zake pamoja na kuzingatia wazawa katika nafasi za juu za utendaji za Kampuni hiyo nchini.  Vilevile, ametoa rai kwa PUMA Energies kuendelea kuwekeza zaidi nchini na kusema kuwa Kampuni hiyo inaweza kujenga vituo zaidi vya kuweka gesi kwenye magari ili kusaidia upatikanaji wa huduma kwa wananchi.  Kuhusu nishati safi ya kupikia, Dkt. Biteko ametoa wito kwa Kampuni ya PUMA kuwekeza katika eneo hilo na kusema kuwa Serikali itaendelea kuimarisha ushirikiano wake kwa Kampuni hiyo. Naye, M...

Lesotho Wavutiwa na Rea

📌Wampongeza Rais Samia katika suala la uhamasishaji wa nishati safi ya kupikia 📌Watoa mwaliko kwa wataalam wa REA kutembelea Lesotho kuwapatia uzoefu Serikali ya Lesotho imevutiwa na namna ambavyo Serikali ya Tanzania kupitia Wakala wa Nishati Vijijiji (REA) imepiga hatua katika suala zima la usambazaji wa nishati safi maeneo ya vijijini. Hayo yamebainishwa Mei 27, 2025 Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Nchini Lesotho, Tankiso Phapano akiwa ameambata na ujumbe wa wataalam katika Sekta ya Nishati nchini humo. "Tumefuatilia kwa karibu katika suala la Nishati, Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizopiga hatua na zilizofanikiwa kwa upana wake na tupo hapa leo hii kubadilishana uzoefu na kujifunza siri hii ya mafanikio iliyowafikisha hapa," alisema Phapano. Alipongeza jitihada binafsi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika suala la uhamasishaji wa matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa wananchi wake. Akizungumzia hal...

Dar Kinara Makusanyo ya Maduhuli

_Soko la madini, madini ya ujenzi na viwandani yaibeba_ 📍*DAR ES SALAAM* Mkoa wa Dar es Salaam umeendelea kufanya vizuri katika ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali kupitia Sekta ya Madini kwa mwaka wa fedha 2024/2025, baada ya kufanikisha makusanyo ya Shilingi Bilioni 23.02 kufikia mwezi Mei, sawa na asilimia 125 ya lengo la mwaka. Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa huo ilipangiwa kukusanya Shilingi Bilioni 18.36, lakini hadi kufikia Machi mwaka huu tayari ilikuwa imetimiza lengo hilo, na sasa imevuka kwa kiasi kikubwa. Akizungumza jijini Dar es Salaam, Afisa Madini Mkazi wa Mkoa huo, Mjiolojia Lameck Gabote amesema mafanikio hayo yametokana na usimamizi thabiti wa vyanzo mbalimbali vya maduhuli ikiwemo mrabaha, ada na tozo mbalimbali. “Mwaka ujao wa fedha 2025/2026 tumepangiwa kukusanya Shilingi Bilioni 24. Tuna imani kubwa kwamba tutafikia na kuvuka lengo hilo. Mkoa wa Dar es Salaam uko ‘active’ kukusanya maduhuli, hatulali,” amesema Gabote kwa msisitizo. Ameeleza kuwa licha ya Dar ...

Waziri Masauni Atoa Onyo Uzalishaji na Matumizi Bidhaa za Plastiki

Na Ada Ouko, GMTV Dodoma. Serikali imetoa onyo kali dhidi ya watu na kampuni zinazoendelea kuzalisha bidhaa za mifuko ya plastiki iliyopigwa marufuku na kuingiza katika matumizi kwa njia za panya. Imesema itaendelea kufanya doria za kushtukiza katika viwanda, viwanda bubu na masoko ili kuwabaini na kuwachukulia hatua wahusika wote wanaojihusisha na biashara hiyo. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amesema hayo leo Mei 27, 2025 jijini Dodoma wakati akitoa tamko la Serikali kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo kilele chake kitafanyika jijini Dodoma na kwamba mgeni rasmi anatarajia kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Hatua hiyo inakuja kutokana na kujitokeza kwa changamoto ya matumizi ya vifungashio vya plastiki aina ya tubings inayotumika kama vibebeo na vifungashio ambavyo havina sifa na kutokukidhi matakwa yaliyowekwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS). Kufuatia ...

Dc Bukoba Ampa Tano Rais Samia Suluhu Hassan

 Na Angela Sebastian; Bukoba  Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Erasto Sima, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa kutoa fedha zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya kuendeleza miradi mikubwa ya soko jipya la kisasa na stedi ya mabasi yaendayo mikoani. Sima ametoa shukrani hizo Mei 27 mwaka huu wakati akikagua maeneo ya mradi wa ujenzi wa soko ambao uko katika hatua za mwanzo ambapo ni ubomoaji wa majengo ya zamani na kusafisha eneo lilipokuwa soko la zamani ili kuwa tayali kwa kuanza ujenzi rasmi. "Ujenzi huu wa soko umekuwa kizunguzungu kwa miaka mingi lakini kutokana na upendo kwa wananchi anaouonyesha Dk.Samia Suluhu Hassan kutaka kuupendezesha mji wa Bukoba na kuleta huduma karibu kwa wananchi ametuletea shilingi bilioni 19 ili soko hili likamilike na standi kuu tunamshukuru sana" amesema Sima Amesema kuwa miradi hiyo ni moja ya miradi ya Tactics ambayo inajengwa nchi nzima na sasa mradi wa soko kuu mkandarasi mshauri tayali anaende...

Watumishi Wampongeza Dkt.Nyansaho Kwa Kuteuliwa na Dkt.Samia

Na Shomari Binda-GMTV  WATUMISHI wa umma na wananchi wamepongeza uteuzi wa Dkt. Rhimo Nyansaho kuwa Mkurugenzi wa Mfuko wa Utumishi wa Umma ( PSSSF) uliofanywa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan. Uteuzi wa Dkt.Nyansaho aliyekuwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara ya Benki ya Azania ulifanyika jana mei 26,2025. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na GMTV wananchi na watumishi wa umma wamesema Dkt.Nyansaho anaonyesha usimamizi mzuri wa kile achokisimamia hivyo atafanya vizuri kwenye nafasi hiyo. Wamesema kwa kupitia taasisi yake ya Nyansaho Foundation amekuwa akiifikia jamii na kuisaidia na kuwa msikivu hivyo hata nafasi hiyo ataitendea haki. Mmoja wa watumishi wa umma wilayani Serengeti ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema ana imani Dkt.Nyansaho atakwenda kufanya kazi nzuri kwenye mfuko huo wa watumishi. Amesema uwajibikaji wa majukumu yake bila shaka ndio uliopelekea Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kumuona na kumteua kwenye nafasi hiyo. " Dkt.Nyansaho ni kiongozi makini na mtulivu at...