Na Angela Sebastian Karagwe WATUMISHI na wanafunzi wa shule ya sekondari jumuishi ya Ruhinda iliyopo kata ya Nyaishozi wilaya ya Karagwe mkoani Kagera, wameishukuru Serikali kwa kuwafikishia huduma ya Nishati ya umeme kupitia wakala wa Nishati vijijini (REA) pia wameomba kuwaboreshewa miundombinu ya Nishati ya kupikia inayotumiwa na wapishi shuleni hapo kwasasa ni hatari kwa afya zao. Walitoa ombi hilo jana wakati bodi ya REA ikiongozwa na mwenyekiti wake balozi meja jenerali mstaafu Jacob Kingu ilipofanya ziara shuleni hapo kwa lengo la kujionea maendeleo ya miradi ya REA vitongojini inayoendelea kutekelezwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini, ambapo shule hiyo ni miongoni mwa wanufaika. Katika taarifa ya mkuu wa shule hiyo Ambrose Katorogo na shairi kwa niaba ya wanafunzi lililoimbwa na mwanafunzi mwenye uoni hafifu Asifiwe Erasto walisema kuwa kupitia Nishati ya kuni wanayotumia wapishi wa shule hiyo kwa sasa inawaathiri kiafya. Mwalimu Katorogo ameongeza k...
Marato tv - Sauti ya Jamii