Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa maendeleo katika sekta ya elimu ndio mkombozi na mafanikio ya Taifa lolote duniani. Amesema kwa kutambua hilo, uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan uliamua kuwekeza katika sekta hiyo ili kuhakikisha watoto wa kitanzania wanapata elimu bora katika ngazi zote. Amesema hayo wakati alipozungumza na wanafunzi na walimu wa shule ya sekondari ya Wasichana ya Lucas Malia iliyopo Ruangwa mkoani Lindi, wakati wa hafla ya kuwapongeza wanafunzi wa kidato cha sita waliofanya vizuri katika mitihani ya kitaifa iliyofanyika mwaka 2025. “Mliopo shuleni na mnaokuja, tambueni kuwa tuna maeneo muhimu ya kuwaelimisha, mtapata elimu iliyobora na imara itakayowapa maarufa na ujuzi ili muweze kukabiliana na changamoto mbalimbali za kijamii na kiuchumi” Amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita imefanya maboresho ya mitaala kwa lengo la kukabiliana na mabadiliko ya kiuchumi yaliyopo duniani ikiwemo mahitaji makubwa ya ajira kwa vijana. “Mabadiliko haya yameifanya mitaa...
Marato tv - Sauti ya Jamii