*Prof. Mkenda ahamasisha vijana kutumia fursa za mafunzo ya ufundi stadi kutimiza ndoto zao* Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amewahimiza vijana kutumia fursa za elimu na mafunzo ya ufundi stadi ili kuendeleza vipaji vyao na kutimiza ndoto zao. Prof. Mkenda ameyasema hayo jana, tarehe 10 Oktoba 2026 wakati wa ufunguzi wa Wiki ya Vijana Kitaifa katika Viwanja vya Shule ya Msingi Ndua, mjini Sumbawanga, mkoani Rukwa, alipomwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba. Profesa Mkenda amesema Serikali inaendelea kuwekeza katika elimu na Mafunzo ya ufundi stadi, mafunzo ya uanagenzi na uzoefu kazini ili kuwaandaa vijana kukidhi mahitaji ya soko la ajira sambamba na kuweka mifumo inayorahisisha upatikanaji wa taarifa, mitaji na masoko. Ameongeza kuwa juhudi za kujenga vyuo vya VETA katika kila wilaya zinalenga kupanua upatikanaji wa mafunzo hayo na kuwawezesha vijana kupata ujuzi wa kuanzisha biashara, kutumia teknolojia na ku...
Marato tv - Sauti ya Jamii