Skip to main content

Posts

Showing posts from September 11, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt.Nchimbi Awasili Jijini Arusha Kuendelea na Mikutano yake ya Kampeni

MGOMBEA Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John  Nchimbi, amewasili mkoani Arusha leo Ijumaa Septemba 12,2025 na kuendelea na mikutano yake ya kampeni akitokea  Mkoa wa Katavi. Mara baada ya kuwasili jijini humo,Balozi Dkt.Nchimbi ataelekea Wilayani Longido,Jimbo la Longido  ambako atawahutubia Wananchi wa jimbo hilo na kuwanadi Wagombea Ubunge wa majimbo ya  Mkoa huo,akiwemo mgombea Ubunge wa jimbo la Longido ,Dkt Steven Lemomo Kiruswa pamoja na Madiwani. Dkt. Nchimbi ameendelea kuinadi Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030,ambayo kimsingi imelenga kwenda kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa Maendeleo katika miaka mitano ijayo. Aidha,amekuwa akitumia  nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais wa CCM,Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan, Wabunge na Madiwani wa Chama hicho kwa kura za kishindo ifikapo Oktoba 29,2025

Rc Mtambi, Awakaribisha Wananchi Kwenye Maadhimisho ya Mara Day

MUSOMA – Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi, ametoa wito kwa wananchi wote wa Mkoa wa Mara na wadau mbalimbali kujitokeza kwa wingi kushiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Mto Mara (Mara Day) yanayotarajiwa kufanyika kuanzia kesho Septemba 12 hadi Septemba 15 mwaka huu katika Viwanja vya Mwenge Wilayani Butiama. Akizungumza na vyombo vya habari leo Septemba 11, 2025 Mhe. Mtambi amesisitiza kuwa, lengo la maadhimisho hayo ni kuhamasisha umma juu ya umuhimu wa kuhifadhi vyanzo vya maji na ikolojia ya Mto Mara na kuongeza kuwa mto huo ni rasilimali muhimu si tu kwa Mkoa wa Mara na Tanzania, bali pia kwa mamilioni ya viumbe hai wakiwemo wanyama wanaohama kila mwaka kutoka Hifadhi ya Taifa ya  Serengeti hadi Maasai Mara nchini Kenya huku akisisitiza kuwa uhai wa bonde hilo unaenda sambamba na uhai wa jamii na uchumi wa nchi. Aidha, Mhe. Mtambi ametoa rai kwa wakazi wa Wilaya zote za Mkoa wa Mara zinazozunguka bonde la mto Mara na zile zisizopakana na mto huo, kujitoke...

Wananchi Wa Kata Ya Mtabira Wilayani Kyerwa Waipongeza Serikali Kwa Kuwajengea Barabara

Na Angela Sebastian; Kyerwa Wananchi wa kata Mabira Wilayani  Kyerwa wameipongeza serikali  kwa kuanza ujenzi wa  Barabara ya Nkwenda - Mabira  kwa kiwango Cha Lami  ambapo wamesema kuwa mradi huo  ukikamilika  wataongeza wateja  wa kununua  mazao yao na kurahisisha usafirishaji wa mazao. Ramadhan Robert na Bosco Gabriel wakazi wa Mabila wamesema wamekuwa wakikutana na Athari za vumbi na  mali zao kuchafuka hali inayosababisha  kukosa soko  hasa mazao yakijaa vumbi,ujio wa mradi huo kama wafanyabiashara umewapa matumaini ya kuuza bidhaa zao zikiwa safi. Meneja wa TARURA wilaya ya Kyerwa Yezron mbasha amesema kuwa mradi huo umegharimu kiasi Cha shilingi Milioni 471.3 ikiwa ni fedha ya Serikali inayotokana na Tozo za Mafuta. Amesema kukamilika kwa Mradi huo kutaongeza Adhi ya mji wa mabira na Kusaidia usafirishaji wa mazao kutoka katika eneo hilo hadi maeneo mengine ya wilaya hiyo na wilaya jirani. Kiongozi wa mbio za mwenge wa u...

Mwenge wa Uhuru Wazindua Tawi la Crdb Nyakatuntu

 Na Angela Sebastian  Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Ismail Ali Ussi amewashauri wananchi wa kata ya Nyakatuntu Wilayani Kyerwa mkoani Kagera kuacha tabia ya kutunza fedha majumba ili kuondokana na mivutano inayoweza kuhatarisha usalama na amani katika jamii. Mwenge wa uhuru mwaka 2025 umezindua tawi la benki ya CRDB la Nyakatuntu ambalo limegharimu shilingi milioni 358 ambapo litahudumia wananchi wa zaidi ya kata 10 za Wilaya hiyo. Akiongea na wananchi waliofika katika eneo hilo kwa ajili ya kusikiliza ujumbe wa mwenge,Ussi amesema kuanzishwa kwa tawi hilo ni kuunga mkono jitihada za Serikali ya hawamu ya sita kwani Crdb wameisha wekeza katika miradi kama hiyo maeneo mbalimbali ya nchi, ambapo lengo ni kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa kuwasogezea huduma hiyo karibu  Amesema zile asilimia 10 zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya uhaulishaji kwa wananchi zinapitia kwa wenzetu wa Crdb kwani wao ndiyo wameweza kufunga mikataba na Serikali hivyo hakuna mwananchi atakaye...

Kigoma: Ukarabati MV Liemba wafikia asilimia 32-TASHICO

  Na Mwandishi Wetu UKARABATI wa meli kongwe zaidi ya abiria Duniani, MV Liemba wenye lengo la kuirudisha kama ilivyokuwa wakati ikianza kazi mwaka 1915 unaendelea vyema ambapo hadi kufikia tarehe 9 Septemba 2025 mradi ulikuwa umefikia asilimia 32 ya utekelezaji. Akizungumza muda mfupi mara baada ya kutembelea ukarabati wa meli hiyo kongwe mkoani Kigoma, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Meli Tanzania (TASHICO) Eric B. Hamissi alisema kuwa maendeleo ya ukarabati wa meli hiyo ya kihistoria ambayo ni tegemeo muhimu kwa jamii iliyopo pembezoni mwa Ziwa Tanganyika unaendelea vizuri ambapo kwa saa umekamilika kwa asilimia 32. "Niko hapa kuangalia maendeleo ya ukarabati wa meli ya MV Liemba ambayo sasa imekamilika kwa asilimia 32 na ukarabati huu mkubwa ni kuhakikisha inaendelea kufaya kazi kwa ufanisi mkubwa katika Ziwa Tanganyika," alisema. Mkurugenzi Mkuu wa TASHICO amesema kuwa MV Liemba ni tegemeo muhimu kwa wakazi walipo jirani na Ziwa Tanganyika ambapo ukarabati wake utabore...