Skip to main content

Posts

Showing posts from April 19, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Salamu na Ujumbe Wa Rais Dkt,Samia Suluhu Hassan Kwenye Sikukuu ya Pasaka Leo April 20,2025

Nawatakia nyote kheri ya Sikukuu ya Pasaka ambapo ndugu zetu Wakristo wanaadhimisha kumbukizi ya kufufuka kwa Yesu Kristo.  Siku hii njema ikawe pia ya tafakari kwetu sote juu ya upendo wetu kwa Muumba wetu na wenzetu;  juu ya kujitoa kwa bidii na weledi katika utekelezaji wa majukumu yetu popote pale tulipo; juu ya kuendelea kujenga jamii inayoishi katika kweli; na juu ya haki ambazo daima huambatana na wajibu kwetu sote. Kwa pamoja, tuendelee kuliombea Taifa letu kheri, huku tukiishi na kutenda yale yanayoiwezesha nchi yetu kuendelea kubaki kuwa moja, imara, yenye amani na utulivu.

Waziri Mkuu Majaliwa Atoa Rai Kwa Viongozi wa Dini Kuombea Uchaguzi Mkuu 2025

Dodoma WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ametoa rai kwa viongozi wa dini kuendelea kuliombea Taifa pamoja na uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.. Hayo yamesemwa leo  (Aprili 19, 2025) Jijini Dodoma wakati wa  Ibada takatifu ya  kusimikwa kwa Askofu Mkuu  Dkt. Evance Lucas Chande wa Karmeli Assemblies of God(KAG) ambapo Mh. Waziri Mkuu Majaliwa amewakilishwa na  Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde “Serikali ya awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mh. Rais Dkt . Samia Sukuhu Hassan imefanya kazi kubwa kuhakikisha nchi yetu inaendelea kuishi katika misingi ya amani,umoja na mshikamano. Nichukue fursa hii kutoa rai kwa viongozi wote wa dini zote kuliombea Taifa katika kipindi hiki tunapoelekea katika uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani ili Tanzania iendelee kubaki moja, yenye amani na utulivu daima “Baba Askofu Mkuu Dkt. Chande ni mmoja wa viongozi ambaye yupo karibu sana na jamii na amekuwa akijitoa sana kuwajali watu wengi wenye mahitaji, hivyo ...

Jwtz Yajivunia Mazoezi ya Pamoja Katika Ulinzi wa Bahari

Jeshi la Ulinzi wa Wananchi Tanzania  JWTZ  limesema zoezi la pamoja la ‘AIKEYME’ limekuwa na mafanikio makubwa katika kupambana na changamoto mbalimbali za Bahari hasa katika ukanda wa bahari ya hindi. Hayo yamebainishwa Aprili 18 Mwaka 2025 na Meja Jenerali Marco Elisha Gaguti ,wakati  akizungumza kwenye hafla fupi ya ufungaji wa zoezi la pamoja la ulinzi wa Bahari maarufu kama ‘AIKEYME’ alipomwakilisha Mkuu wa Majeshi nchini Jenenerali Jacob John Mkunda, katika zoezi lililoandaliwa na Tanzania na India huku likishilikisha mataifa mengine tisa. Aidha, Meja Jenerali Gaguti amempongeza Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan na Waziri wa Ulinzi wa nchini India kwa kuandaa zoezi hilo na huku akisema kuwa lengo kuu la zoezi hilo la pamoja ‘AIKEYME’ ni kujifunza mbinu mbalimbali za kukabiliana na changamoto baharini na kubadirishana uzoefu pamoja na kutengeneza mfumo wa kusaidiana katika ukanda wa Bahari ya hindi. Hata hivyo, Meja jenerali Gaguti amesema kuwa kw...

Dkt Tulia Akabidhi Gari La Wagonjwa Kituo Cha Afya Mwakibete- Mbeya

 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 19 Aprili 2025, amezindua gari la kubebea wagonjwa (ambulance) lililotolewa na Serikali kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Mwakibete, jijini Mbeya. Uzinduzi huo unalenga kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa wakati kwa wakazi wa Jiji hilo. Akizungumza katika hafla hiyo, Dkt. Tulia amewashukuru Viongozi wa Serikali kwa kuendelea kupeleka huduma muhimu kwa wananchi, huku akiwataka wakazi wa Jiji la Mbeya kujitokeza kwa wingi katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 na kumpigia kura kwa kishindo Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kama ishara ya kutambua na kuunga mkono kazi kubwa na nzuri anayoifanya katika kuboresha maisha ya Watanzania.